# PENZI LINALOCHIPUKA

PENZI.PEVU#Kulikuwa na kitu cha kipekee katika hewa ya jioni ile. Upepo mwanana ulivuma taratibu ukitokea Magharibi kwenda mashariki ukiwa
ukibeba harufu ya maua yaliyokuwa yamechanua pembeni ya barabara. Amina alisimama kwa muda, akivuta pumzi ndefu kana kwamba anajaribu kuutuliza moyo wake uliokuwa ukidunda kwa kasi isiyo ya kawaida. 

Leo, hatimaye, angekutana naye yule ambaye kwa miezi kadhaa alikuwa akiujaza moyo wake kwa maneno matamu, vicheko vya simu, na ujumbe uliojaa hisia nzito. Jina lake lilikuwa Daniel. Amina alisharidhia pendo kwa Daniel baada ya kujishauri sana mioyoni hadi pale alipokata kauli kwamba hasa alihitaji kuwa mtu... mwanaume wa kumliwaza nafsi yake.

Ni wengi waliokuwa wakimtaka na walijileta mara na zawadi hii ama Ile, lakini hakutaka kula au kupokea vya watu ambao alikuwa wazi kwamba moyo wake haukuridhia.

Alimpenda sana Daniel kwa ukarimu wake hasa katika matukio machache aliyoyakumbuka, Daniel haikuwa mtu wa nipe nikupe, Wala hakuhutaji shukrani au kujivunia kwa jambo lolote.

Amina alijiuliza, *Je, atakuwa vile nilivyomfikiria? Je, nitajizuia vipi mbele yake?* Mawazo yalimgonga kama mawimbi ya bahari yasiyokoma. Kulikuwa na mchanganyiko wa hofu, hamu, na msisimko uliomfanya ajihisi kama yuko ndotoni. Siku hii Amina alikuwa na miadi na mpenzi wake ambaye bila kusita alimkaribisha nyumbani kwake tofauti na siku zingine ambapo walijivinjari viwanjani.

 Lakini sifa moja iliyomfanya Amina kufa na kuoza kwa ajili ya huyu bwana ni kwamba hakutanguliza Mapenzi mbele katika mahusiano yao japo alimsaidia kwa jambo lolote lililomfika hakuwahi kuonyesha kushinikiza Mapenzi dhidi yake.

Siku hii ya leo alimwalika kwake anapoishi. Amina Alisubiria kwa muda kiasi pale nyumbani baada ya kumpigia simu kuwa alishafika kwake alikaribia kukata tamaa mara punde tu baadaye, alimuona akija kwa mbali. Alianza kusogea kuelekea alipotokea kama kumlaki, Walipokaribiana walivamiana na kupigana pambja, na kisha alimkaribisha nyumbani mwake.

Akirini mwake alivuta taswira ya mlolongo mzima wa matukio ya nyuma. Hatua zake zilikuwa za kujiamini, lakini uso wake ulionyesha tabasamu la upole lililomfanya Amina apoteze kabisa utulivu wake. Moyo wake uliruka kama ndege aliyefunguliwa kutoka kwenye kifungo. Alitamani kukimbia—lakini si kwa hofu, bali kwa kumkimbilia.

Waliposogeleana, muda ulionekana kusimama. Hatimaye…” Daniel alisema kwa sauti ya chini, yenye joto.

Amina hakujua aanzie wapi. Alitabasamu tu, macho yao yakikutana kwa mara ya kwanza bila skrini wala umbali. Kulikuwa na nguvu fulani isiyoelezeka—kama vile walikuwa wanajuana tangu zamani.

Alipomsogelea zaidi, walikumbatiana.

Na hapo ndipo hisia zilipobadilika.

Ilikuwa kumbatio la kwanza, lakini lilihisi la kweli zaidi kuliko yote aliyowahi kupata. Moyo wake ulipiga dhidi ya kifua chake, na kwa sekunde ile, alihisi kama dunia yote imenyamaza isipokuwa wao wawili. Kulikuwa na joto la ajabu, utulivu, na wakati huo huo, msisimko uliopita mipaka ya maneno.

Mawazo yake yalichanganyikana—*Je, huu ndio mwanzo wa kitu kikubwa? Je, nimepata yule wa kweli?*

Daniel alimtazama kwa upole, macho yake yakizungumza zaidi ya maneno. Kulikuwa na heshima, mvuto, na ahadi isiyosemwa.

Walikaa pamoja, wakiongea, wakicheka, lakini kila mguso mdogo—vidole kugusana, mabega kukaribiana—ulizua hisia mpya ndani ya Amina. Hisia za kupagawa, za kutaka muda usimame, za kutamani kila sekunde idumu milele.

Huo ulikuwa mwanzo wa penzi pevu linalochipuka.

Penzi ambalo halikuanza kwa kelele, bali kwa ukimya wenye maana. Penzi ambalo lilianza kwa aibu kidogo, lakini likakua kwa haraka ndani ya mioyo yao. Penzi lililojaa matarajio, ndoto, na ule uhondo wa kugundua mtu mwingine kwa mara ya kwanza—kimwili na kihisia.

Sasa alikuwa ndani mwake na kwa mara ya kwanza alihisi kama aliyepo peponi, akaamua haikuwa makosa yake kuumbwa mwanamke bali ni Mungu tu, hasa alihitaji penzi pevu kutoka kwa Daniel.  Amina alijua, ndani kabisa ya moyo wake, kuwa siku ile haikuwa tu ya kukutana. Daniel alipoingia chumba Cha uani, huku nyuma alipunguza baadhi ya nguo zake na kutangulia kitandani...alihitaji tiba ya maradhi ya pendo lililomfika,  mtu pekee aliyehisinalikuwa tabibu wa moyo ni Daniel..


Post a Comment

Previous Post Next Post