Raia mwenye asili ya Kichina amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela nchini Kenya kwa
Kujaribu kusafirisha kwa njia ya magendo zaidi ya mchwa 2,000 kutoka nchini humo. Raia huyo kwa Jina Zhang Kequn alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Nairobi na alikiri kosa la kujihusisha na biashara ya wanyamapori bila kibali baada ya shtaka la kula njama kuondolewa.Inadaiwa kuwa mchwa hao, wanaothaminiwa kwa bei ya hadi dola 100 kila mmoja, walikuwa wakipelekwa China, Marekani na Ulaya.
Mahakama pia imemwamuru Zhang kulipa faini ya dola 8,000 au atumikie kifungo cha ziada cha mwaka mmoja. Mkenya mmoja anayetuhumiwa kuwa msambazaji wa mchwa hao amekana mashtaka na kesi yake inaendelea mahakamani.
Chanzo
DW-Kiswahili
