Waziri wa Habari na Mawasiliano Burundi Gabby Bugaga
amepatikana amefariki kwenye shamba la miwa eneo la Kivoga huko Burundi. Polisi nchini humo inachunguza chanzo cha kifo chake.Gabby ameongoza wizara hiyo tangu Agosti mwaka 2025, akijipatia sifa kwa kuboresha upatikanaji wa mitandao na kuweka utaratibu katika matumizi ya mitandao ya kijamii, hususan YouTube.
Alisifiwa pia na vyombo vya habari vya Rwanda kama kiongozi mwenye busara na hekima.
Tazama vidio hii ujionee.
#dwkiswahili #dwhabari #burundi #gabbybugaga #waziri
Chanzo
DW- Kiswahili
