KILA WILAYA/ COUNTY IWE NA ENEO LA MAZIKO



 Katika kipindi Cha takriban wiki moja iliyopita, Tar 21, Machi 2026 iligundulika miili iliyokuwa imezikwa

kwenye kaburi la pamaoja ndani ya  county ya Kericho.

Taarifa za awali zilisema

kwamba huenda miili hiyo ilisafirishwa kutoka County ya Nyamira ambapo baadaye taarifa hiyo ilithibitishwa na Mkurugenzi/ Mkuu wa upelelezi wa Umma, Mohammed Amin, kuwa za kweli na kwamba miili yote 33 iliyozikwa kwenye kaburi la pamoja ilisafirishwa kutoka County ya Nyamira.

Tukiachana na taarifa za kiupelelezi na mkondo wa Sheria kuhusiana na Mwenendo wa tukio zima hasa  utata kuhusu idadi iliyoidhinishwa na mahakama, au kuzikwa kwenye eneo la makaburi binafsi, kuwepo kwa sehemu za au viungo vya miili, au kujua ni ya akina nani miongoni mwa sababu zingine, tujikite hasa kwa nini miili hiyo ilisafirishwa kutoka Nyamira kwenda Kericho.

Bila shaka sababu kuu ni kwamba County ya Nyamira haina eneo la makaburi ya Umma la kizika watu. Pamaoja na sababu zingine zozote ikiwa ni pamaoja na agizo la mahakama kumruhusu miili Ile kisafirishwa kuzikwa kwingineko nje ya County husika, au idadi iliyoruhusiwa kitofautiana namile iliyozikwa, kiujumla yasingetokea kama County hiyo ingelikuwa na eneo la Umma la maziko.

Zipi sababu za ziada kama msongamano wa miili kwenye Mochari ya County au kuharibika kwa miili husika 

Lakini tujiulize kwamba hili litaendelea hadi lini? Awamu nyingine wataomna kibali kwenda kizika labda kisii au Migori au Bomet.  Katika maisha ya Dunia hii, Binadamu amekuwa kiumbe pekee mwenye thamani kuliko kiumbe kingine chochote. Haijalishi kama mtu amekufa au yu hai, thamani ya utu imesalia daima dawamo.

Sasa pale inapotokea kwamba mtu aliyefariki Jana wa kumdai akamzike kwa heshima zake, Bado ni muhimu kwa yeyote nayebeba jukumu hilo kuzingatia tu wa mtu.  Ndio maana tumeona hata watu wanaofariki nje katika mataifa ya mbali miili Yao hurejeshwa kwa wahusika ili kuizika kwa heshima zao au tamadumi zao.

Ni vema zile County zisizokuwa na maeneo ya kuzika watu wao zitoe vipaumbele kwa kutenga au kuyafuta maeneo hasa kwa kutenga fedha kwenye bajeti zao ili kununua  maeneo ya maziko.

Hili ni muhimu kwa sababu maisha ni Safari. Kwa binadamu kwani kama Hujafa hujaumbika.

Post a Comment

Previous Post Next Post