Hali ya taharuki ilishuhudiwa baada ya Spika wa Seneti, Amason Kingi, kutoa amri ya kukamatwa kwake na kupelekwa kwenye kituo Cha Polisi Cha Bunge, kufuatia gavana huyo kususia mara kwa mara vikao vya Kamati ya Uhasibu ya Seneti (CPAIC) kujibu maswali ya matumizi ya fedha ambapo inadaiwa kwamba baadhi ya nyaraka au stakakabadhi muhimu katika baadhi ya malipo kuhusiana na County yake hazikuwasilishwa.
Mwenendo wa Matukio:
Gavana huyu alionekana ndani ya majengo ya Bunge, kisha maseneta waliokuwa kwenye kikao walipitisha azimio chini ya uongozi wa spika Amason Kingi la kumkamata na kumwasilisha kwenye kituo Cha Polisi Cha Bunge na hatimaye kumfikisha mbele ya kamati hiyo. Ni muhimu kuzingatia baadhi ya mambo hapa:
1. Gavana Jonathan Lati Leleit alikuwa katika majengo ya Bunge,
2. Bunge la Seneti lilipitisha azimio la kumkamata kiraia ' Citizen Arrest '
3. Baada ya kukamatwa alitakiwa kupelekwa kwenye kituo kidogo Cha Bunge kisha kwenye kamati husika ili akajibu hoja zilizomkabili.
4. Ni kweli kwamba alikaidi wito wa kufika mbele ya kamati husika.
Vuta nikuvute ilitokea, huku maseneta wakimzuia na kumshinikiza kuingia ndani ya kituo cha polisi cha Bunge.
Kukaidi kukamatwa
Gavana huyu anajua wazi kwamba alitakiwa kujibu hoja za madai ya ubadhilifi wa fedha. Katika mazingira Yale kwa nini hakukubali kwa hiari kwenda kuhojiwa?
Mazingira ya kumtaka kumkamata
Maseneta waliongozwa na ' Sergeant at arm' walionekana kutumia Nguvu kuliko kiasi kwa kumvuta au kumsukuma hapa na pale ambapo baadaye aliponyoka na kutoroka. Kuna mawazo mbadala kwamba walipaswa kumuagiza kwa wito wa lile azimio la Bunge kwenda kwa hiari yake, hata hivo swali ni je, kama ingelikuwa ni Polisi wao wangembembeleza au wangetumia Nguvu?
Hatimaye, gavana huyo alitoroka na kuingia kwenye gari lake lililokuwa likimsubiri, na kuondoka kwa kasi.
Je, kitendo Cha maseneta kilizingatia Sheria? Kuna Sheria ya Kukamata Mbunge au Gavana Bungeni:
Ndio, kuna sheria zinazoruhusu hatua hiyo.
Ibara ya 125 ya Katiba ya Kenya: Inampa Bunge na kamati zake nguvu za kuwaita watu (ikiwemo magavana) na kuwaamuru kuleta hati au nyaraka.
Sheria ya Nguvu na Marupurupu ya Bunge (Parliamentary Powers and Privileges Act): Sheria hii inatoa mamlaka kwa Bunge kuamuru kukamatwa kwa mtu yeyote (pamoja na magavana) ambaye anadharau au kususia wito wa kamati za Bunge.
Kukamatwa Majengoni:
Ingawa majengo ya Bunge ni maeneo yaliyolindwa, kiongozi kama Gavana anaweza kukamatwa ikiwa kuna wito rasmi (warrant) uliotolewa kwa sababu ya utovu wa nidhamu au kususia kamati.
Spika Kingi aliamuru maafisa wa bunge (Sergeant-at-Arms) kumkamata gavana huyo alipopatikana ndani ya eneo hilo.
Madai ya Kuombwa Rushwa: Kumekuwepo na madai kutoka kwa baadhi ya Magavana, akiwemo Gavana huyo wa Samburu na Gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja, kwamba wanahitajika kutoa hongo au mulungura kwa wajumbe wa Kamati husika wanapoitwa kuhojiwa.
Hata hivo hatujaweza kudhibitisha kawepo kwa taarifa zozote kutoka kwa Gavana yeyote zilizoripotiwa kwenye idara au vitengo vya Serikali vinavyohusika na kupambana na rushwa au kwenye kamati zinazohusika na maadili ya watumishi wa Umma kutoka kwa Magava wanaotoa shutuma hizo.
Inatia shaka kubaini endapo kiongozi mwenye wadhifa wa Gavana anaweza kushindwa Cha kufanya pale anahitajika kutoa rushwa kinyume Cha sheria
Maandamano Samburu
Maandamano Samburu: Hatimaye baadhi ya Wananchi kutoka County ya Samburu walionekana wakiandamana siku iliyofuata Alhamisi Tar 2 April 2026, kupinga na kulaani kile walichokitaja kama udhalilishaji wa Gavana wao. Labda tuwakushe Wananchi wa Samburu kwamba hili sio swala Kisiasa ila ni Uwajibikaji fedha za Umma.
Isitoshe County ya Samburu ni miongoni mwa County zenye miradi mingi iliyokwama ikiwemo Elimu na afya. Sasa pale inapotokea tuhuma za ubadhilifu ni lazima Viongozi wawajibishwe.
Na Kama hiyo haitoshi fedha zinazodaiwa kufujwa hazitokani na mapato ya County hiyo pekee, bali ni mgao kutoka Hazina kuu Ni hao hao hao ambao ni WA kwanza kulalamika pale huduma muhimu zinapokwama.
Ni maoni yetu kwamba Sheria ifuate mkondo wake kwa kila mmoja.UWAJIBIKAJI WA MAGAVANA
