Kuna wanaosoma mapenzi ni bahari, wengine husema Mapenzi ni msitu na wengine husema Mapenzi hayana mwalimu au mwenyewe. Lakini hapa leo tunakuuliza unadhani maumbile au umbile la mtu huchangia kwa kiasi gani kwenye swala la mapenzi husani kwa wanawake.
Kuna baadhi ya Wanaume husema Mimi nilimpenda mke au mpenzi wangu kwa ajili ya unene, au wembamba, au kwa rangi ya sura awe ni mweusi, mweupe au majinya kunde ilimradi tu walivyoridhishama.
Wakati mwingine unaweza kumpata mtu akishanhaa wengine walivyopendana bila kujiangalia yeye binafsi, ama utakuta anauliza kwani Fulani naye alipenda nini kwa Fulani? Lakini kumbe Kuna wengine pia wanaulizana kumhusu yeye
Mfano Wanaume Wana tabia ya kujadili na kuchambua maumbile ya wanawake, mwingine atakwambia Mimi sipendi mwanamke mwembamna au mwingine atasema Mimi katu mwanamke mnene simpendi kutegemea kila mtu na maoni au utashi wake.
Hata hivyo kila mtu na siri ya moyo wake.Lakini tofauti na Wanaume, wanawake huwa na njia tofauti kabisa kuhusiana na jinsi wanavyopenda au kupendwa na mara nyingi huwa si watu wa kujadili maumbile ya wenzi wao kama walivyo Wanaume. Upendo wa mwanamke huijaza nafsi yake polepole kwa kusikia na kutendewa kile moyo wake unachopenda ilimradi tu aridhike.
Wanaume hupenda kwa Kasi ya kuona kwa kuridhisha macho kabla ya nafsi kisha hukifu haraka kama alivyoanza.
Ndo maana wengine watasema mwanamke mnene ni mzuri kitandani huku wengine wakisema hasa mwanamke mwembamba ndo kila kitu, kumbe Mapenzi ni upepo unaovuma, inategemea uko upande gani, inakotoka au unapokwenda?
Wewe umesimama wapi?
