MAKALA/UCHAMBUZI, JE Rais Ruto amepoteza ushawishi Mlima Kenya?

 Je, kwa maoni Yako unadhani Rais Ruto Anapoteza Uungwaji Mkono katika eneo la  Mlima Kenya?

Hadi kufikia kipindi Cha Aprili 2026, Rais William Ruto anakabiliwa na changamoto kubwa za kisiasa katika eneo la Mlima Kenya, huku kukiwa na ishara za wazi za kupungua kwa umaarufu wake. 

1. Hali ya Mlima Kenya

Kukataliwa, Kuzomewa na kususiwa kwa  Kimani Ichung'wah akiwa na Rais kwenye ziara ya kimaendeleo huko kiambu Tar 27, Machi, 2026, ni ishara tosha ya kutoridhika kwa kwa Wananchi wa ngazi katika eneo hili. Lakini pia inaweza kuwa dalili ya kumwonyesha Rais kwamba wale wandani wake ambao yeye anadhani wanampigia upatu kwa Wananchi ndo hao watakaomwangusha.

2. Ushawishi wa Gachagua 

Mgongano kati Rais na Naibu wake wa zamani huko Nyandarua, ambapo Rigathi Gachagua alipata fursa ya kumwonyesha ubabe Rais Ruto kwamba Bado ana Nguvu na anasikilizwa na watu wa jamii yake licha ya kumwondoa kwenye nafasi hiyo.

Akiongea kwenye ibada ya mazishi ya Mbunge wa zamani wa eneo hilo, Gachagua alijipiga kifua kwamba Rais Ruto licha kumwondoa kwenye kitincha Unaibu Rais, hawezi kumwondoa kwenye nyoyo za watu wa mlima Kenya.

Gachagua pia alionekana kumshambulia makamu wa Rais wa sasa Kithure kindiki kwa madai kwamba alikwemda kinyume Cha desturi za jamii hiyo kwa kuanza kuongelea urithi wa nafasi aliyoiacha marehemu kabala hajazikwa.

Na kama vile jaikutosha, Gachagua pia alimvaa Spika wa Bunge la Taifa kwa madai kwamba mara kadhaa aliliruhusi Bunge kujadili bila kuwepo kwa hoja au mswada rasmi iliyowasilishwa kwa ajili ya kumjadili

 3.Msimamo wa John Methu

 Matamshi ya Seneta John Methu huenda yakawa na nguve fulani nyuma yake, hivyo si vema kuyatafsri kwa kumwangalia yeye tu,Seneta huyu alimwambia Rais Ruto hadharani: "Nakuheshimu lakini sikuogopi," na kisha akatoa maelezo marefu kuhusu ahadi za Rais Ruto kuhusu miradi ya maendeleo hasa Barabara katika enoo hilo ambayo ilikuwa haijakamilika huku Mwananchi' wakiitikia kwa kufuatisha. Tunadhani wapo viongozi wengine wa mlima Kenya ambao wapo nyuma yake.

4. Onyo la Raia msitaafu Uhuru Kenyatta

: Hivi karibuni, Rais msitaafu Uhuru akiwa kwenye ibada kwenye kanisa moja huko Kirinyaga aliwaonya wakazi wa eneo hilo la Mlima Kenya dhidi ya kurudia "makosa" ya kumchagua tena Rais Ruto, matamshi hayo ya Uhuru kenyatta yameonekana kutonesha kidonda na kuongeza kasi ya upinzani dhidi ya serikali ya sasa.

Murejesho kutoka kwa Rais Ruto:

Pamoja na kuwepo kwa matukio hayo, Rais Ruto amepuuza madai hayo kwanza kwa kusema yeye anazijia vema siasa za eneo la Mlima Kenya, na kwamba akiwa Rais wa kenya kamwe hawezi kupangiwa mambo/ mipango yake na mtu mwingine. Rais alimjibu Gachagua kwamba asibebe au kuchukua maswala yake binafssi na kuyajumlisha kwa watu wote wa Mlima Kenya. akisisitiza kuwa uhusiano wake na eneo la Mlima Kenya hauwezi kuvunjika kirahisi, na kwamba yeye atapimwa kwa vitendoena si maneno matupu.

Mgawanyiko wa ODM na Kura za Nyanza

Swala lingine ambalo limekuwa likigonga vichwa habari ni mpasuko.wa.cja.cha ODM katika milengo miwili, Linda Ground/Linda Mwananchi: Mgawanyiko ndani ya ODM (chama kilicho katika "serikali ya msingi mpana") kuwa makundi ya 'Linda Ground' na 'Linda Mwananchi' unahatarisha ushirikiano huo. Hii ni kwa Sababu kwanza Mpasuko' huo unaweza kuwafanya wanachama kuwa njia panda, lakini pia unapunguza kura kwa Rais Ruto ifikapo 2027.

Kwa vile chama hicho kimeshiriki uundaji wa serikali ya sasa, huenda Mpasuko' ikawa mapana au mkubwa zaidi baada ya muda serikali ya sasa kumalizika. Kuna tetesi za kuwepo watu/ wajumbe ndani ya Linda Ground ambao huenda wakajiumhanna Linda Mwananchi mbeleni japo kwa sasa' Bado wanatetea kitumbua kisiingie mchanga.

Isitoshe, si wote wanaoonekana kwenye majukwa sasa watastahimili kutetea nafasi zao awamu ijayo mfano Gladys Wanga na Junet Mohammed wanaaminika kwama walipigiwa upatu na Hayati Raila Odinga, hii Ina maana kwamba watakuwa na kibarua kigumu kwenye uchaguzi ujao. 

Wengine ni Simba Arati wa kisii ambaye ushawishi wake kwa sasa unaonekana kushuka ukilinganishwa na alipoingia kwenye nafasi ya ugavana. Lakini pia anakabiliwa na watu wa mlengo wa Fred Matiangi.

Kuna taarifa pia kwamba Oburu Oginga sio tu kwamba hataweza kuchaguliwa ila upo uwezekano wa kutogombea tena kama Seneta wa Siaya na hasa huenda akasalia kuwa kinara wa ODM.

Kutokana hali hii upo uwezekano wa mabadiliko makubwa sananya Kisiasa kwa kadiri siku zinavyosonga.

Eneo la Magharibi

Kitendo Cha kushambuliwa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Seneta wa Vihiga, Godfrey Osotsi ambaye anaunha mkono Mlengo wa Linda Mwananchi kwa sasa zinaonekana kama sehemu ya manyanyaso dhidi ya viongozi wa eneo hilo la magharibi, na zimeonekana kuleta umoja wa Waluhya ambao sasa wanaonekana kusita kumuunga mkono.

  Eneo la Pwani 

Eneo la Pwani pia Lina umaarufu wa chama Cha ODM kilichogawanyika. Endapo makundi haya mawili yatajizatiti au kwa kuzidiana uwezo wa kuwashawishi wapiga kura, ukweli unasalia kwamba kura zitajigawa kutegemeana na milengo au jinsi vyama vitakavyoungana.

Vuguvugu la 'Niko Kadi'

Wimbi la vijana wanaojisajili kupiga kura wanaonekana kuwa mitazamo mipya wengi wao hata hivyo wanadai mabadiliko ikiwa ni pamoja na:

I) Uongozi Bora: Vijana wanatarajia kuchagua viongozi wanaowajibika, wasio na ufisadi, na wanaoweza kuleta maendeleo.

ii) Fursa za Ajira: Matarajio ya kuundwa kwa nafasi za ajira na fursa za kiuchumi ili kuwasaidia kujikimu kimaisha.

iii) Mabadiliko ya Sera: Vijana wanataka sera zinazounga mkono vijana, kama vile elimu bora, mafunzo ya ufundi, na mikopo ya biashara.

iv) Ushiriki katika Uongozi: Vijana wanataka kushiriki kikamilifu katika siasa na uongozi, siyo tu kama wapiga kura, bali pia kama wagombea.

v) Uboreshaji wa Maisha: Matarajio ya kuwa na maisha bora zaidi, ikiwa ni pamoja na huduma bora za afya, miundombinu, na usalama. 

Licha ya matarajio haya, baadhi ya vijana wanaweza kukata tamaa wanapoona kuwa viongozi hawashughulikii mahitaji yao baada ya kuchaguliwa. Hata hivyo, wengi wanaendelea kujisajili kama wapiga kura wakiamini kuwa kura zao zina nguvu ya kuleta mabadiliko. 

Rais Ruto kupoteza Kura

Kwa kuzingatia hali ilivyo mlima Kenya, mgawanyiko wa ODM, na hali ilivyo magharibi mwa Kenya ni wazi kuwa Rais Ruto anaweza kupoteza au kupata kiasi kidogo Cha kura tofauti na ilivyokuwa awali.

Mukhutasari

Matukio haya yanaonyesha kuwa Rais Ruto anapoteza udhibiti na umaarufu na katika eneo la Mlima Kenya mzozo wa Rais  Ruto na Gachagua, na ushawishi wa Uhuru Kenyatta. Hali kadhalika, utulivu wa kisiasa katika maeneo ya Nyanza na Magharibi unatishiwa na mipasuko ndani ya ODM na kuibuka milengo miwili inayokizanzana ni vigumu kuwepo uhakika kwa Rais Ruto kupata kura za pamoja kutoka kwa chama  ODM iliyogawanyika.

Endapo vuguvugu la 'Niko Kadi' litazaa matunda kwa kuongeza idadi ya kura zenye kuleta mabadiliko basi Rais Ruto atakuwa na kibarua kigumu kupata kura zitakazompatia ushindi kwenye uchaguzi ujao.

Inasadikiwa kwamba hata muungano wa Kenya kwanza unaoshikiria serikali ya sasa huenda ukasambaratika hasa kutokana na washiriki muhimu kama Moses Wetangula na Musalia Mudavadi kupoteza umaarufu kwenye maeneo wanayotoka.

Post a Comment

Previous Post Next Post