ROSTAM AZIZI ATEKA TASNIA YA HABARI

Hivi majuzi ulishuhudiwa Mwisho wa Enzi ya Miaka 66 ya Umiliki

wa Aga Khan Fund For Economic the ( AKFED) katika Nation Media Group

Tarehe 10 Machi 2026 imeingia katika historia ya tasnia ya habari Afrika Mashariki baada ya kutangazwa rasmi kwa uuzaji wa shirika maarufu la habari, Nation Media Group. Kampuni hiyo iliyokuwa ikimilikiwa kwa muda mrefu na Aga Khan Fund For Economic Development (AKFED), imeuzwa kwa Kampuni ya Taarifa Ltd inayomilikiwa na tajiri Bilionea wa Tanzania, Rostam Aziz.

Uuzaji huo umehitimisha rasmi umiliki wa AKFED uliodumu kwa takribani miaka 66 tangu mwaka 1959, kipindi ambacho Nation Media Group imejijengea sifa kama moja ya taasisi zenye ushawishi mkubwa katika uandishi wa habari, uchapishaji na utangazaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Hata hivyo, hatua hii imeibua maswali makubwa kisiasa, kiuchumi na kitaaluma kuhusu mustakabali wa chombo hicho cha habari.

# Kwa nini Aga Khan Fund For Economic Development imeuza Nation Media Group?

Moja ya maswali makubwa yanayoulizwa na wachambuzi ni kwa nini AKFED imeamua kuuza shirika hili baada ya kulimiliki kwa zaidi ya nusu karne.

Kwa muda mrefu, mfuko huo wa maendeleo umekuwa ukiwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, afya, miundombinu na vyombo vya habari. Hata hivyo, mabadiliko ya kiuchumi duniani, ushindani mkali wa vyombo vya habari vya kidijitali na gharama za uendeshaji wa taasisi za habari huenda ni baadhi ya sababu zilizochangia uamuzi huo.

Aidha, kuna uwezekano kwamba mfuko huo umeona ni wakati muafaka kuhamisha umiliki kwa wawekezaji wapya wenye mtaji mkubwa na mtazamo mpya wa kibiashara katika zama za mabadiliko ya haraka ya teknolojia ya habari.

# Kwa nini mnunuzi si Mkenya?

Swali lingine linalozua mjadala ni kwa nini mnunuzi wa shirika hili si Mkenya, licha ya Nation Media Group kuwa moja ya taasisi kubwa za habari nchini Kenya.

Kwa kawaida, taasisi zenye ushawishi mkubwa katika jamii huwa na mvuto wa wawekezaji wa ndani. Hata hivyo, inaonekana katika mchakato huu wa uuzaji, mwekezaji kutoka nje ya Kenya ndiye aliyeibuka mshindi.

Hali hii imeibua mjadala iwapo kulikuwa na wawekezaji wa Kenya waliokuwa tayari kununua kampuni hiyo au kama kulikuwa na vigezo maalum vilivyompa nafasi mnunuzi kutoka nje ya nchi.

# Je, zabuni ya wazi ilitangazwa?

Maswali makubwa zaidi yanahusu uwazi wa mchakato wa uuzaji.

Je, Aga Khan Fund For Economic Development ilitangaza zabuni ya wazi kwa ajili ya uuzaji wa Nation Media Group?

Ikiwa zabuni ilitangazwa, ilikuwa wazi kwa wawekezaji wote wa ndani na nje? Na kama haikutangazwa hadharani, ni kwa misingi gani mnunuzi alichaguliwa?

Ukosefu wa taarifa wazi kuhusu mchakato wa zabuni umeacha nafasi ya uvumi na maswali mengi katika jamii ya wanahabari na wachambuzi wa uchumi.

# Je, kuna mnunuzi wa ndani nyuma ya pazia?

Katika mijadala inayoendelea, baadhi ya wachambuzi wanauliza iwapo huenda kukawa na wawekezaji wengine wa ndani ya Kenya walio nyuma ya pazia la ununuzi huu.

Katika biashara kubwa za kimataifa, si jambo la ajabu kwa wawekezaji kushirikiana au kutumia kampuni nyingine kama mwavuli wa uwekezaji. Hivyo, uwezekano wa ushirikiano wa kimkakati kati ya wawekezaji wa ndani na wa nje hauwezi kupuuzwa.

# Rostam Aziz ni nani katika nguvu za Kiuchumi na Kisiasa?

Mnunuzi mpya wa Nation Media Group, Rostam Aziz, ni mmoja wa wafanyabiashara wenye ushawishi mkubwa Afrika Mashariki.

Utajiri wake umetokana na uwekezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo madini, nishati, kilimo na biashara za kimataifa. Mbali na nguvu zake za kiuchumi, Rostam Aziz pia ana historia ya ushiriki katika siasa za Tanzania.

Aliwahi kuwa Mbunge wa Igunga mkoani Tabora na pia aliwahi kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC). Kutokana na nafasi hizi, ana mtandao mpana wa kisiasa ndani ya Tanzania.

Aidha, inafahamika kuwa ana mahusiano ya karibu na viongozi mbalimbali wa kisiasa katika ukanda wa Afrika Mashariki, wakiwemo viongozi wa sasa na waliopita madarakani nchini Tanzania pamoja na viongozi wa Kenya.

# Kutakuwa na Athari gani katika uhuru wa chombo hiki Cha habari

Swali kubwa zaidi katika tasnia ya habari ni hili: je, mmiliki huyu mpya ataboresha kwa kiasi gani uaminifunuwazi na uwajibikaji wa Nation Media Group? 

Post a Comment

Previous Post Next Post