
Kwa wengine, hii ni hulka ya kupenda, wanafanya hivo kwa makusudi. kama vile mshairi anavyotumia maneno kuumba hisia. Mwanamke anaweza kuona kiuno chake kama uwanja wa sanaa, na mavazi yake kama penseli inayochora hadithi ya kujiamini. Wapo wanaoamini kuwa kuonekana kwa mistari hiyo si aibu bali ni sehemu ya mvuto, kama kivuli kinachofuata mwili bila kuomba ruhusa.
Lakini si kila anayevikwa vazi hilo hulivaa kwa makusudi. Maumbile ya mwanamke yana siri zake; viuno vilivyojaa, makalio yenye umbo la kuvutia—haya yote hufanya wakati mwingine kuwa vigumu kuficha kila mstari. Hapo ndipo mitindo ya chupi, mishono yake, na hata aina ya vitambaa vinavyotumika huingia katika mjadala. Wengine hujinasua kwa kuvaa chupi zisizo na mapindo, lakini si wote wanaojali au kuona hilo kuwa ni jambo la msingi.
Kwa baadhi ya wanawake hii tabia ya kujiaibisha jinsia ya kike na hata wao hushangaa na kusemezana wanapoona mwenzao kavaa hivo. Lakini mbaya zaidi Kuna wanaovaa mavazi Yao kwa jinsia kwamba si hoja mistari ya nguo zao za ndani kuonekana ila hata rangi ya chupi walizovaa.
Hata hivyo, jamii nayo ina macho yake na midomo yake. Midomo haina simile wanaosoma wanasema wenye kunyamaza hufunga midomo yasemavyo maneno ya wahenga. Ni ajabu jinsi mwanamke anavyoweza kuwa jaji mkali kwa mwenzake kuliko hata mwanaume. Hata hivo Kuna wale wanaohoji kwamba kwani kutoona hiyo michoro ya chupi zao Kuna maanisha kwamba hawajavaa? Kwa maana nyingine kuona ramani hizo si hoja ya msingi kwa Enzi hii.
Kwa upande mwingine, wapo wanaume wanaotazama jambo hili kwa jicho la tamaa au burudani. Kwao, ni kama ishara ya siri inayochochea hisia, kama upepo unaovuma na kugusa ngozi kwa upole. Lakini si wote wanaokubaliana na hilo; wengine huona kuwa thamani ya mwanamke haipaswi kupimwa kwa namna anavyovaa bali kwa utu wake na heshima anayojipatia mwenyewe.
Lakini kuwa wale wenye mtazamo kwamba tabia hiyo inamdhalilisha mwanamke na kufanya kukosa staha katika jamii. Lakini ajabu ni ni kwamba Kuna wake za watu pia huvaa hivo na Wala waume waume zao hawahoji.
Hebu tufikirie mazingira ya kazi—mwalimu darasani au nesi hospitalini. Je, mstari wa nguo ya ndani unapokuwa kivutio kuliko ujumbe au huduma, nani hupoteza na nani hunufaika? Hapa ndipo swali la mizani linapojitokeza: uhuru wa mtu binafsi dhidi ya taswira ya kijamii.
FMISITARI YA CHUPIasheni inasema, nenda na wakati, Lakini busara hunong’ona, chagua kinachokujenga. Mwanamke ana haki ya kuvaa apendavyo, lakini pia ana uwezo wa kuamua taswira anayotaka kuacha mioyoni mwa watu na jamii inayomzunguka.
Mwisho wa yote, ukweli unabaki palepale: mwanamke ni zaidi ya mwonekano wake. Kiuno kinaweza kuwa kivutio, lakini thamani yake halisi iko katika heshima, kujiamini, na hekima anayobeba ndani yake. Maana kama wahenga walivyosema, Nguo humvisha mtu, lakini tabia humtambulisha.
Hitimisho:
Baadhi ya wanawake huvaa hivo kwa kupenda na kwa makusudi au kutojali.
Baadhi yao huwa na malengo ya kuchokoza au kuvuta hadhira au hisia za jinsia ya kiume
Hata hivyo baadhi ya wanawake hawapendi tabia hiyo na huiona kama kujidhalilisha.
Kuna sababu asilia zinazotokana na maumbile ya kike
Sababu zingine ni aina ya nguo zenyewe, mtindo wa ushonaji, au malighafi ya vitambaa vinatumika kutengeneza nguo za ndani za kike n.k
Sababu nyingine ni kumomonyoka kwa Mila na desturi za zamani kwa kizazincha sasa, zilizokuwa zikizingatia staha, kuwa aibu ya kitofanya jambo Fulani ambalo ni mwiko.
Wewe je unasemaje? Toa maoni yako