#JE, MWANAMKE UNAJUA LIMBWATA LISILO DAWA KWA MUMEO AU MPENZI WAKO?

Mpenzi msomaji wa makala hii, bila shaka utakubaliana na Mimi kwamba Mapenzi ndio kila kitu katika Dunia. Bila kujali kwamba yanatoka kwa nani yakienda kwa nani lakini ukweli unabakia pale pale kwamba hakuna asiyetaka kupendwa hata yule Ajuza anayetembea kwa Gongo pia anahitahi Mapenzi.

Asilimia kubwa ya wasanii wanakijita katika utunzi na uimbaji wa Nyimbo za Mapenzi kwa sababu ndizo zinazotawala soko. Kuna wanaofanya kazi kwa ajili ya wapenzi wao, Kuna wanaosoma kwa ajili ya wapenzi wao, wengine wanafanya biashata kwa ajili ya wapenzi wao ilimradi tu kila mmoja anajaribu kufanya kitu au jambo Fulani kwa ajili ya mpenzi wake. Kuna walionunua Majumba, Magari au hata viwanja kwa ajili wapenzi wao n.k


 Yanasemwa mambo mengi sana kila siku kuhusiana na Mapenzi, kila mara kwenye mitandao, kwenye runinga au Redio utakutana na mada za Mapenzi. Hata makanisani siku hizi Wachungaji wengi hutumia mada zinazohusiana na Mapenzi ili kuivutia hadhira ya waumimi wao.

Lakini kinachosumbua hasa huwa si kupenda na Wala si kupata wa kupenda, ila shida kubwa ni kuliendeleza lile penzi, tatizo kubwa hasa ni kudumisha mahusiano kati ya wapenzi au mume na mke, na inapofikia hapo kila mtu anaongea lake. 

Tutajaribu kujadili mada hii katika makala zetu zijazo. Lakini leo hebu tuangalie tu kiduchu kwamba wewe mdada unayesoma makala hii unadhani nini hasa unachotakiwa kufanya ili kulinda mahusiano yako namaanisha kumdhibiti mpenzi wako?

Katika swali hili unaweza kupewa majibu mia ila Mimi nakupatia jibu moja tu. Kiungo kikubwa katika mahusiano ni tendo la ndoa au tendo la kujamiana. Hayo mengine yote ni ziada tu. Endapo katika mahusiano yako, kutokana na sababu yeyote Ile tendo hili halifanyiki kwa dhati ya wapenzi wote, halifanyiki kwa kuridhishana, basi penzi lililo katika hali hiyo liko hatarini.

Sasa unafikiaje huko? Wewe mwanamke una nafasi yako na mwanaume pia ana nafasi au jukumu lake. Sasa tendo la ndoa linafanyika wapi? Bila shaka ni chumbani ambapo wote mnakiwa huru kila mmoja kuweza kuonyesha utundu wake. Kwako wewe mwanamke unaweza kupata ufanisi ukizingatia mambo haya machache ambayo ni limbwata lisilo dawa:-

1. Vaa mavazi yanayomsisimua mume au mpenzi wako ((Sexy pants or Sexy night dresses) ili kumpagawisha, Wanaume wameumbwa kupenda kwa kuona kabla ya kusikia au kutendewa.

2. Uweke mwili wako sawa kwa kutumika mafuta ya cream au Lotion za kawaida si lazika ziwe za gharama, ongeza marashi au manukato ya kadiri, Wanaume wengi hawapendi Maradhi yenye harufu kali isipokuwa tu kama yeye mwenyewe atakuruhusu kuyatumia. Hii inasaidia kuuongezea thamani mwili wako mwili wako 

3. Vaa heleni, bangili au mkufu, na kama mume au mpenzi wako anapenda unaweza kuvaa shanga za kiunoni pia.

4 Zingatia usafi wa kitanda, .Andaa kitanda mapema na kukiweka kiwe na mvuto mfano tandika shuka zenye maua mazuri au hata nyeupe

5. Kitanda kiwe katika hali nzuri, ukubwa wa kitanda si hoja, Kuna baadhi hufikiri kitanda kikubwa huongeza starehe lakini ukweli ni kwamba kitanda kidogo ni Bora zaidi kwa sababu kinawaleta karibu zaidi. Hakikisha kitanda hakipigi kelele wakati wa tendo.

6. Zingatia usafi wa hali ya juu wa mwili wako. Oga walau kutwa mara mbili na kujipaka mafuta, na si lazika utumie lotion au cream za gharama. Wanaume wengi hawapendi mwanamke anayenuka jasho kitandani.

7. Piga mswaki kabla ya kulala, usiingie kitandani ikiwa unanuka mdomo au ikiwa na punje za wali kwenye magegu 

8. Jifunze kuwa mchokozi unapokuwa chumbani, usijikalie tu au kwamba wewe ndoa wale ambao mwanaume asipokuanza kaa kimahaba zaidi.

9 . Usianze mapema kujadili matatizo yenu au changamoto zenu kabla ya kuliwazana na kufanya mapenzi.

10. Ukigundua mumeo/ mpenzi wako hayuko sawa au hana amani jaribu kujua tatizo lake au yaliyomsibu, jadili naye kwa kumtia moyo na kumpa ujasiri.

Endapo utayafanya yote haya niliyokudonolea kwa dhati kabisa bila kupuuza ni lazima mahusiano yako yatadumu na utaishi kuyafaidi bila kusubiri siku ya Idi.https://www.blogger.com/blog/post/edit/3207865657537994030/2415855557004399613

Post a Comment

Previous Post Next Post