#JE, NINI KIFANYIKE KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA ?

      

https://www.blogger.com/blog/post/edit/3207865657537994030/9081263631248039102Kumekuwepo na miito ya mara kadhaa
kwa Serikali ya kenya kuainisha Ukatili wa kijinsia kama Janga la Kitaifa Nchini humo.

Kwa mujibu wa Wanaharakati na watetezi wa haki za wanawake/ Binadamu, hatua hiyo inaweza kuongeza hamasa na mwamko kwa jamii dhidi ya vitendo hivyo. Hata hivyo haijajulikana wazi endapo serikali ya kenya inaweza kuitikia wito huo au lah.

Mara ya kwanza wito huo kutolewa kwa Serikali ya kenya ilikuwa Mwezi Oktoba 2021. Baadaye wito kama huo ulitolewa tena tarehe 3-4, Novemba, 2024, na Hatimaye tena mnamo tarehe 1 Juni, 2026.

Kwanini Serikali imeziba Masikio:

Athari za Kifedha na Kibajeti: 

Kutangaza ukatili wa kijinsia kama janga la kitaifa kisheria kunaishurutisha serikali kutenga na kuelekeza fedha maalum za dharura za nchi (State funds) na rasilimali nyingi kukabili tatizo hilo. Serikali mara nyingi huepuka hili ili kuzuia shinikizo kwenye bajeti kubwa.

Sura ya Nchi Kimataifa: 

Hatua hiyo inaweza kuonesha kuwa nchi imeshindwa kulinda raia wake (hasa wanawake na watoto), jambo linaloweza kuathiri taswira ya utalii na uwekezaji wa kigeni.

Taswira na mtazamo:

 Mara kwa mara, vyombo vya usalama vimekuwa vikitafsiri visa hivi kama "migogoro ya kifamilia au kinyumbani" (domestic disputes) badala ya kuvitazama kama dharura ya kitaifa ya haki za binadamu.

Vipaumbele Vingine vya Kisiasa: 

Idara za upelelezi kama DCI zimekuwa zikilaumiwa kwa kuelekeza nguvu na rasilimali nyingi kuwasaka na kuwadhibiti wapangaji wa maandamano ya kisiasa badala ya kuwakamata wabakaji na wauaji.

Athari na Changamoto Kuu:

Kusua-sua kwa serikali kutangaza swala hili kuwa Janga  kumesababisha mambo yafuatayo:

Ongezeko la Vifo na Ukatili: 

Bila mkakati madhubuti wa kitaifa, takwimu zinaonesha mashirika kama [FIDA-Kenya yanaendelea kupokea kesi nyingi zinazohusika na visa vya Ukatili wa kijinsia.
Zaidi ya wanawake 1,000 wameuawa katika miaka ya hivi karibuni.

Kuporomoka kwa Imani ya Umma:

 Wananchi wanapoteza imani kabisa na mifumo ya sheria, mahakama, na viongozi wa wanawake serikalini ambao wanaonekana kutochukua hatua thabiti.

Kuhujumiwa kwa Sheria na Katiba: 

Ukatili huu unahujumu moja kwa moja haki ya kimsingi ya kuishi na usawa wa kisheria uliopo kwenye Katiba ya Kenya, na kuongeza utamaduni wa wahalifu kutoadhibiwa (culture of impunity).

Wasiwasi na Hofu Kijamii: 

Wanawake na wasichana wengi wanajikuta wakiishi kwa hofu kubwa hata ndani ya nyumba zao wenyewe kutokana na vitendo vya unyanyasaji wa wapenzi wa karibu (intimate partner violence).

Hoja kuu:

Hoja yetu hapa ni kwamba  ni wazi kwamba kuna ugumu kwa Serikali kikubali kutangaza swala hili kuwa Janga la Kitaifa kutokana na sababu tulizozitaja hapo juu. Hata hivyo Bado tunadhani kwamba kutangazwa kwa ukatili wa kijinsia kama Janga la Kitaifa si Suluhu ya kumaliza tatizo hili.

 Kwa maoni yetu tunadhani ipo haja ya kufanyika jitihada za makusudi kukabiliana na tatizo hili kwa njia zinginezo mbali na kutangazwa kuwa Janga la kitaifa. Hatukatai wito huo ila tunadhani kwamba serikali inaweza kuja na sera au mpango mkakati mipya yenye lengo la kuelimisha Umma dhidi ya athari za ukatili kwa jinsia zote katika jamii.


Katika kutekeleza azima hiyo ni lazma chanzo au kiini Cha tatizo kijulikane na hatua madhubuti kuchukuliwa. Tofauti na hivo inawezekana kutangazwa hivo na bado tatizo likaendelea. 

Uchambuzi wa kina:

Ongezeko la ukatili wa kijinsia (SGBV) nchini Kenya huchangiwa na mtandao mgumu wa mambo ya kijamii, kisaikolojia, na kiuchumi. Sababu hizi zimejikita katika ugumu wa maisha, mmomonyoko wa maadili, na ukosefu wa usawa wa kijinsia. 

Hapa kuna ufafanuzi wa sababu kuu;

1. Usaliti na Visasi vya Kimapenzi:

Migogoro ya kimapenzi, usaliti, na wivu uliopitiliza ni miongoni mwa vyanzo vikuu vinavyosababisha ukatili wa kutisha kama vile mauaji ya wanawake au kujeruhiwa vibaya.

Ufafanuzi:
 Watu wengi wanashindwa kukubali kuachwa au kusalitiwa na wenza wao. Hali hii inapojitokeza, baadhi ya watu huamini kuwa njia pekee ya kulipiza kisasi ni kuchukua uhai wa mwenzao au kuwasababishia maumivu ya kimwili kama adhabu. 

Hii inachangiwa na hasira, hisia za aibu mbele ya jamii, na wivu uliokithiri.

2. Ulaghai wa Kimapenzi:

 Tabia ya baadhi ya wanawake (na hata wanaume) kupokea pesa na zawadi kutoka kwa watu wasiowapenda kwa dhati ni tatizo kubwa.
 Hii inachochea kwa kiasi kikubwa migogoro.

Ufafanuzi

Kumekuwepo na mtindo wa "kuchuna" au kutumia watu kifedha. Mtu anapotoa pesa au zawadi, mara nyingi huwa na matarajio ya kurudishiwa upendo au mahusiano ya kimapenzi. Kitendo cha mmoja kugundua kuwa alikuwa akitumika tu na wala hakupendwa huibua hisia za kutapeliwa, kudharauliwa, na hasira kali. Huchochea visasi na ukatili wa kimwili.

3. Uduni wa Maisha, Ukosefu wa Ajira, na hali ngumu ya uchumi:

Hali ngumu ya kiuchumi na ukosefu wa ajira huweka shinikizo kubwa linalosababisha mtandao wa ukatili kwa njia zifuatazo:

Ufafanuzi

Ukosefu wa kipato huwafanya vijana wengi kuingia kwenye vishawishi vya utafutaji wa fedha kwa njia ya mkato, ikiwemo ulaghai wa kimapenzi.

Ukatili wa Kifedha na Kisaikolojia:

Hali ya utegemezi wa kiuchumi huwafanya baadhi ya wanawake wasiweze kutoka kwenye ndoa zenye unyanyasaji kwa sababu hawana uwezo wa kujitegemea.

Unyanyasaji wa Kisaikolojia: 

Ugumu wa maisha huleta msongo wa mawazo. Wanaume wengi wanaposhindwa kutimiza majukumu yao ya kifamilia kama wazazi, hupoteza heshima na utu wao mbele za familia, na matokeo yake huhamisha hasira zao kwa kuwapiga na kuwanyanyasa wenza wao ili kujihakikishia "mamlaka".

4. Mmomonyoko wa Maadili na Utamaduni duni:

Tabia na Kanuni zenye madhara za kitamaduni bado zimekita mizizi ambapo wanaume wengi huamini wana haki ya kumiliki, kudhibiti, au hata kumwaadhibu mwanamke.
 Jamii inaposhindwa kukabiliana na tamaduni hizi, watenda ukatili hujiona wako sahihi na hukwepa mkono wa sheria.

5. Kushindwa Kutatua Migogoro:

 Vijana wengi wamekosa mafunzo ya namna ya kukabiliana na misongo ya mawazo na migogoro katika uhusiano. Badala ya kufunguka, wengi hukimbilia matumizi ya dawa za kulevya na pombe kupita kiasi, mambo ambayo hupunguza uwezo wa kufikiri na kuchochea matendo ya kikatili.


Nini kifanyikie? Hapa Kuna mapendekezo yetu:

i)  Utekelezaji thabiti wa sheria: Kutoa adhabu kali na za haraka kwa wahalifu ili kuondoa utamaduni wa kutoadhibiwa na kuhakikisha vyombo vya usalama vinachukua hatua za dharura mara tu visa vinaporipotiwa.

ii? Uhamasishaji na elimu: Kuelimisha jamii, hususan wavulana na wanaume, ili kubadili mtazamo na mfumo dume unaochochea chuki na unyanyasaji dhidi ya wanawake.

iii? Vituo vya usaidizi: Kuongeza vituo vya kutoa ushauri nasaha na msaada wa kisaikolojia kwa waathiriwa walio katika hatari.

iv) Uwezeshaji wa kiuchumi: Kuwapa wanawake uhuru wa kifedha ili kuepuka utegemezi unaowafanya wanase katika ndoa au mahusiano yenye ukatili.

v) Kutoa taarifa mapema: Jamii inapaswa kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa za siri kupitia namba za dharura za polisi (kama vile 112 au 999) au kupitia mashirika kama vile UNHCR Kenya.

vi) Elimu na ushauri kwa wanawake na watoto wa kike Kuhusu mahusiano hatari ya kilaghai, kuacha kabisa kulihusisha na hahusiano ya hila na ulaghai wa mapenzi, kuacha kupokea pesa na zawadi kutoka kwa Wanaume ambao wanajua wazi kwamba hawawapendi.

vii) Utoaji wa Elimu na Uhamasishaji kwa vijana kuepuka matumizi ya mihadarati vinavyosababisha kufikiwa maamuzi magumu.

viii) Uwezeshaji wa nafasi za ajira kwa vijana na ushauri nasaha kupunguza msongo wa mawazo kwa vijana.

iX) Serikali itumike vyombo vya habari kuhamasisha Umma, mathalani kama kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwenye Matangazo ya ugonjwa wa Ukimw/HIV/AIDS, kila chombo Cha habari kilirusha Matangazo juu ya ugonjwa huo na mabango yaliwekwa kila sehemu za maeneo ya Umma.

(X) Wazazi na walezi wahimizwe kutoa ushauri nasaha kwa watoto wao, na kuchukua hatua za kinidhamu pale inapobidi, utoaji wa Elimu ya kijamii uanzie katika ngazi ya familia.

Kulingana na mashirika ya kutetea haki za wanawake nchini Kenya, hakuna idadi kamili ya kitaifa iliyotolewa na serikali, lakini ripoti zinaonyesha kuwa zaidi ya wanawake 27 waliuawa kikatili katika kipindi Cha miezi mitatu (3) ya kwanza ya mwaka huu 2026. Hata hivyo, makadirio ya Umoja wa Mataifa huweka wastani wa vifo 47 vya wanawake kila wiki nchini Kenya. 

Hapa tumeorodhesha baadhi ya visa vichache kwa kipindi Cha Januari hadi Juni, 2026:

Kisa kilichofungua mwaka 2026 ni Cha Ukatili wa mzazi kwa mtoto kililipotiwa eneo la Dandora, Nairobi,Januari Mosi 2026, Cha mtoto Charlene Nyangweso aliyeadhibiwa kwa kupigwa vibaya na baba yake na kumsababishia kifo, baba yake aliyekuwa ametengana na mama ya mtoto alimwadhibu kwa kosa la kwenda kutembelea mama yake na kuchelewa kurudi.

Visa vinginevyo tulivyoweza kubainishwa taarifa zake ni pamoja na :

#1. Davine Kwamboka (Kaunti ya Migori): Aliuawa kikatili mwezi Aprili, ambapo picha za CCTV zilionyesha mumewe na wanaume wengine wakijaribu kutupa mwili wake.

2. Anita Nyambura (Kaunti ya Nakuru): Aliuawa mwezi Aprili na mumewe ambaye ni mwanajeshi (KDF) mbele ya mtoto wao mchanga.

3. Benedicta Keziah (Kaunti ya Kilifi): Msichana wa umri wa miaka 7 ambaye aliuawa kikatili mnamo mwezi Mei, tukio lililozua hasira kali nchini.

4. Shirley Gatumi (Kaunti ya Tharaka Nithi): Msichana wa miaka mitatu aliyetoweka mnamo Mei na mwili wake kupatikana ukiwa umetenganishwa viungo.

5. Winny: Mwanamke mwenye umri wa miaka 23 aliyepatikana amefariki katika Kijiji cha Kamuga, Nyakach, mnamo Mei 12 baada ya kushambuliwa na mumewe katika mzozo wa nyumbani.

6. Rose Apundi (au Rose Benta Aponia): Mwanafunzi wa miaka 21 wa Riat College ambaye alitoweka Aprili 5, na mwili wake wenye majeraha kupatikana siku chache baadaye ukiwa umetupwa kwenye msitu wa Riat, eneo la Kisumu.

7. Roseline Achieng Odhiambo: Mwanamke wa miaka 37 aliyepatikana Nyumbani mwake, akiwa amefariki na akiwa na majeraha mengi mwilini mwake katika mtaa wa Manyatta 'B' kufuatia shambulio linalohusishwa na unyanyasaji wa nyumbani. 

#8.  Ann Keya Ahuna aliyeuawa 16 Mei 2026 kwa kuchomwa Kisu na mtu anayesadikiwa kuwa mpenzi wake kwa jina Newton Ambeyi.

9. Sheila -- Kutoka Nyamira Ekerenyo Mwanafunzi mwenye umri miaka 16 aliyeuawa na mtu anayesadikiwa kuwa mpenzi wake ambaye alijinyonga baada kutekeleza kisa hicho.

10. Rachel Wandetto: Mwanamuziki aliyefariki mnamo Mei 19, 2026 baada ya kushambuliwa na kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

11. Mercy Nyambura, Mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Sinendet aliyetoweka Mei 18-19,2026 baada ya kutoweka na kupatikana akiwa amekufa kwenye shamba la mahindi.

12.) Abigael Nafula Ogara (32) aliyetoweka Aprili 29,2026 na mwili wake kupatikana kwenye chumba na maiti webuyeMei 22,2026. Inahisiwa kuwa Mwenzi wake askari KDF Bonface Somiyu huenda alihusika na kutoweka kwake, alionekanannaya mara ya mwisho.

13.) Alice Riang'a kutoka Itibo, Suneka Kisii alitoweka Mei 6, 2026, baadaye mwili wake ulipatikana msitu wa Barkowino, Bondo.alizikwa Mei 22, 2026.

14.) Mwanamke kwa jina Jackline Wanjiru (27) alishambuliwa na kumwagiwa Tindikali kwa kile kinachoaminika kama Dhuluma ya kimapenzi, eneo la Kiritili, Embu hatimaye alifariki dunia, Alizikwa Mei 27,2026.

15.) Mwezi wa nne 2026,Mwanamke kwa jina Mercy Awour aliviziwa na kumwagiwa Tindikali na mtu anayesadikiwa kuwa mpenzi wake aliyetumia pikipiki usafiri  na kutoweka baada ya tukio hilo.

16. Tarehe 18 Mei, 2026, Mwanamke kwa jina Maurine Masili anauguza majeraha baada ya kudaiwa kumwagiwa maji ya maharage yaliyokuwa yakipikwa jikono baada ya mzozo kuibuka kuhusiana na ubishi juu ya ongezeko la Bei ya Mafuta na msimamo wake kauli ya ''tutam:

17. Mwezi Mei 26, 2026 Mwanafunzi wa kidato Cha nne (17) huko Nakuru anadaiwa kumwagiwa Tindikali na mwanaume 22) anayedaiwa kumlazimisha awe mchumba wake na baada ya kukataliwa alimvizia binti huyo mapema asubuhi akienda Shule na kumwagiwa Tindikali.

18. Mwezi Mei 27, 2026 eneo la Shieni Kaunti ya kirinyaga Mwanaume wa miaka (45) anadaiwa kumuua mpenzi wake mpenzi wake umri miaka (39) baada ya kuibuka mzozo Naina Yao.

19. Tarehe 02 Juni 2026, mwili wa Mwanamke kwa Jina la Salome Chelagat ulipatikana ukiwa uchi kitandani mwake kwenye nyumba ya kupanga eneo la Mucherwo, Molo Kaunti ya Nakuru.

20. Tarehe 11, Juni 2026, Mwili wa Mwanamke kwa Jina Joy Kwanini Gathu ulipatikana kwenye gunia ukiwa umekatwakatwa vipande na kutupwa huko Nyeri. Mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 25, Muhitimu wa chuo Cha Nyeri Polytechnic.

21. Tarehe 14 Juni, 2026, Mwili wa mwanamke kwa jina Mwanahamisi Juma ulipatikana ukiwa umetupwa kichakani Kijiji Cha Ziwani, eneo la Matuga, kwale kwa kile kinachoaminika alifanyiwa Ukatili kabla ya kuuawa. Mwanamke huyo alikuwa ni bubu.

22..Tarehe 19, Juni 2026, Mwili wa mwanamke kwa jina la Susan Wanjiku Njeri ulitambuliwa na ndugu zake njia alama za vidole na Msimbogeni baada kutoweka kati ya tarehe 11-12, Juni 2026 kutoka eneo la Cieko Kasarani alipokuwa ameanza kazi za ndani (Yaya).

23. Tarehe 23 Juni 2026, mwanamke kwa jina Elizabeth Ngina Mulwa, Umri (2) alikurikana akiwa amekufa, na mwili wake kutenganishwa na kichwa ukiwa uvunguni mwa kitanda kwenye chumba Cha kupanga, eneo la kiang'ombe Thika. Alikuwa Mwanafunzi wa Thika Polytechnic.

24. Tarehe 24 Juni 2026, Mwanaume kwa Jina la Amos Manasseh Nyang'au alishambuliwa na kuuawa na umati wa watu eneo la kerokae, Nyamira, baada ya kusingiziwa kuwa mwizi na mpenzi wake waliokuwa na mgogoro naye. Kijana huyo anadaiwa kwenda kwa mwanamke mpenzi wake kudai mtungi wa gesi alipokuwa ameununua katika mahusiano yao.

25. Tarehe 24, Juni 2026, Msichana mwenye umri wa miaka (17) alishambuliwa Narok na mtu anayemfahamu, na kukatwa mkono na kung'olewa jino (hakufariki ) kwa kile kinachosadikiwa kuwa dhuluma za kingono.

26. Tarehe 30, Juni, 2026, Mwanamke kwa Jina la Teresia Nyokabi alikitikana ameuawa eneo la Gatundu, na mwili wake iliyokuwa uchi ukiwa umetelekezwa.

Hivi ni baadhi ya visa vichache tu lakini uhalisia ni zaidi ya idadi hii.

Toa maoni Yako.....

Post a Comment

Previous Post Next Post