
Rais William Ruto aliwapongeza Wabunge
waliopitisha Mswada wa Fedha (Finance Bill) wa mwaka 2026/27 mnamo Juni 19, 2026. Rais Aliyasema hayo alipohudhuria ibada ya mazishi ya Mama Zipporah Kosgey katika Kijiji cha Kipkoror, Eneo Bunge la Nandi Hills, Kaunti ya Nandi.Kwa upande mwingine,Rais Ruto aliwakosoa na kuwashambulia vikali Wabunge walioupinga mswada huo mnamo Juni 22, 2026. Alitoa kauli hizi alipokuwa ziarani Kianyaga, na kushiriki shughuli za maendeleo kufufua shughuli ya uuzaji na masoko ya kahawa huko Kaunti ya Kirinyaga. Kwenye hotuba hiyo, aliwataka Wabunge hao kuwaheshimu wapiga kura wao badala ya kuupinga mswada huo ambao alisema unaleta rasilimali na kuwasaidia wananchi.
Kuhusu muktadha wa matukio haya mawili tofauti:
Tukio la Kwanza (Nandi): Ruto alieleza shukrani zake kwa Bunge la Kitaifa kwa kupitisha mswada huo licha ya kile alichokitaja kuwa ni fitina, porojo, na propaganda kutoka kwa wanasiasa wa upinzani. Alidai kuwa wanaoupinga walishindwa kuonyesha ni kipengele gani hasa kinachowaumiza Wakenya.
Tukio la Pili (Kirinyaga): Alisema kuwa wabunge waliochagua kuupinga mswada huo hawakuwa na akiri na kwamba walipotoshwa hawakuwa na habari za kweli na walilenga kuupotosha Umma . kwa wananchi. Aliwataka viongozi hao kutumia akili na ukweli katika siasa zao badala ya kusambaza upotoshaji.
Hoja Nyeti:
Lakini hoja hapa ni nani aliyefanya makosa? Ni Mbunge alipepiga kura ya ndiyo au yule aliyepiga kura ya hapana? Je ilitakiwa Wabunge wote wapige kura ya ndio? Katiba ya Kenya pamoja na kanuni za Bunge zinatoa uhuru kwa kila Mbunge kupiga kura kwa hiari yake au kwa kuzingatia uwakilishi wake Bungeni na si kwa shinikizo la aina yoyote. Tunadhani hakupaswi kuwa na wa kulaumiwa. Rais William Ruto anapaswa kuiheshimu Demokrasia. Ni Imani yetu kwamba nyuma ya Wabunge arobaini wasio na mawazo ya kifikiri kwa mujibu wa kauli za Ruto, Kuna kundi kubwa la Wananchi wanaowakilishwa na wao.
Licha kutoonuesha kushwangazwa na idadi mdogo sana ya Wabunge waliohudhuria kikao hicho Cha bajeti kubwa kabisa katika historia ya kenya, yenye lengo la kuwahudimia Wakenya zaidi ya Mil 50, badala yake Rais anawanyooshea vidole Wabunge walioipinga bajeti hiyo. Itoshe kusema hapa Kwamba endapo Wabunge wote wangeliiunga mkono bajeti Ile, taswira ambayo ingejitokeza hapo ni kwamba Kenya si Nchi ya Demokrasia na ni yenye chama kimoja chenye mlengo mmoja. Ni dalaja kubwa kwa Rais Ruto kuwaona Wabunge wote wakipiga kura ya ndio licha ukweli kwamba Kuna mitazamo na milengo tofauti kuanzia kwa wananchi na Wabunge wanaowaeakilisha.
Hali Halisi:
Wabunge wa Kenya walikosekana na hata wengine kususia vikao vya Bunge wakati wa mchakato wa Bajeti ya 2026/27 na Mswada wa Fedha (Finance Bill) kutokana na shinikizo za kisiasa, hofu ya kulalamikiwa na wapiga kura kuhusu kodi ngumu, na mbinu za ki-mkakati za kupinga au kupitisha hoja bila kuwajibika kikamilifu.

1. Sababu za Wabunge Kususia na Kutohudhuria KikaoHofu ya Umma (Public Backlash):
Wabunge wengi walikwepa kuhudhuria hasa wakati wa upigaji kura, ili kutojihusisha moja kwa moja na kuunga mkono kodi ambazo zinaonekana kuwakandamiza wananchi.
Kuwajibika Kiasi (Political Cowardice):
Wengi walitoroka bunge ili wasionekane wanaiunga mkono serikali kupita kiasi, au ili kuwaridhisha wananchi waliotaka miswada hiyo ya kodi ikataliwe.
Ugomvi na Mivutano:
Kulikuwa na mizozo mikali kati ya wabunge wa upinzani na wa serikali, hali iliyosababisha upande mmoja kususia vikao wakidai hawashirikishwi ipasavyo.
2. Kwa nini Wabunge wa Serikali pia Walikosekana?
Shinikizo la Kimaeneo (Grassroots Pressure): Wabunge wengi wanaounga mkono serikali (hasa kutoka maeneo kama Mlima Kenya) waliona ugumu wa kupigia kura mswada wenye kodi nzito mbele ya wananchi wao wanaolalamika.
Mbinu za Kinafiki za Upigaji Kura (Strategic Absence): Wabunge walio wengi waliofika bungeni kufanya uamuzi walikuwa wachache sana ikilinganishwa na idadi kamili. Baadhi walikosekana ili kuepuka kupiga kura za "NDIYOO" hadharani, jambo linaloweza kuwagharimu kisiasa wakati wa uchaguzi.
3. Je, Katiba ya Kenya ndiyo Inayotoa Mwanya wa Wabunge Kuzurura?
Ndiyo, Katiba ya sasa ya Kenya haimlazimishi mbunge kuwepo bungeni kila wakati. Inatoa tu masharti ya idadi ya chini (Quorum) ya Wabunge hamsini (50) Kuwepo Bungeni ili Bunge kuendelea na Vikao halali.
Hata hivyo, Sheria za Bunge (Standing Orders) zinatoa adhabu kwa wabunge wanaokosa vikao mfululizo bila idhini ya Spika.
Kwa maana nyingine, Tatizo si Katiba moja kwa moja, bali ni utekelezaji dhaifu wa sheria za kinidhamu ndani ya Bunge.
4.Je Kuna Ulazima wa Kurekebisha Ibara ya 121 ya Katiba ya Kenya?
Ni maoni yetu hapa Kwamba ipo haja ya kurekebisha ibaranya 121 kutaja wazi Uwepo wa Angalau theluthi mbili ya Wabunge UKUMBINI (2/3 Majority): ili kupitisha miswada nyeti yenye maslahi kwa Taifa.
Kuna haja kubwa na pendekezo hilo kuhakikisha kuwa sheria na miswada nyeti, hususan ya fedha na bajeti, inapitishwa tu kukiwa na akidi ya theluthi mbili ya Wabunge.
Hii itazuia uamuzi wa mambo muhimu ya kitaifa kufanywa na "kikundi kidogo" cha wabunge waliohudhuria, na itawalazimu wabunge wote kueleza msimamo wao bungeni badala ya kujificha.
5. Athari za Hatua hii ya Wabunge kwa Wananchi Walipa Kodi:
Maamuzi yasiyo na Uwakilishi Sahihi:
Sheria na bajeti nzito hupitishwa bila idhini au ushiriki wa wabunge wengi, jambo linaloleta sheria mbovu.
Kupoteza Fedha za Umma:
Wananchi wanawalipa mishahara na marupurupu tele wabunge ili kuwasilisha maslahi yao. Kutohudhuria vikao ni sawa na uhujumu uchumi kwa mlipa-kodi.
Mizigo ya Kodi na Madeni:
Kupitishwa kwa bajeti (kama ya Shilingi Trilioni 4.8 na kuendelea) bila mjadala mpana kunaongeza mfumuko wa bei na madeni kwa wananchi wa kawaida.
6. Maoni ya Wananchi kwa Ujumla
Hasira na Kukata Tamaa:
Wakenya wengi wana mtazamo kwamba wabunge wao ni waoga na wanafiki. Wanahisi hawajali maisha magumu ya wananchi.
Wito wa Uwajibikaji:
Wananchi wanazidi kulalamika mtandaoni na kwenye vyombo vya habari wakitaka uwazi na uwajibikaji kutoka kwa wawakilishi wao. Kulingana na asasi za kiraia na maoni ya mitaani, wengi walitaka mswada wa fedha wa 2026 ukataliwe kabisa.
Maoni Yako ni muhimu kwetu....