
#1. MUKTADHA WA TUKIO
Mkutano uliokuwa ukiendelea katika Kanisa la All Saints Cathedral, Nairobi, ukihusisha makundi ya mashirika na Asasi za kiraia kujadili athari za bajeti ya kitaifa ya 2026/27 kwa wananchi wa kawaida ulisimama ghafla na kuwa hekaheka za mguu niponye baadha ya Genge la wahuni kuvamia shughuli hiyo.
Tukio hilo lilifuatia siku moja tu baada ya Waziri wa fedha wa Kenya John Mbadi kusoma bajeti hiyo Bungeni.
# 2. JINSI UVAMIZI ULIVYOFANYIKA MAWIMBI MAWILI
Kulingana na picha za CCTV zilizowekwa hadharani na kituo maarufu Cha Runinga ya Citizen Nchini Kenya, tukio hilo lilifanyika kwa awamu mbili, kundi la kwanza la washambuliaji walifika saa tatu unusu asubuhi (9:39 AM) wakitumia pikipiki, wakivamia kwa nguvu eneo la kanisa. Dakika tano baadaye, saa tatu na (9:44 AM), polisi waliwafukuza nje kuelekea Valley Road na kanisa likawa tulivu.
Hata hivyo, kwa mshangao mkubwa, saa nne na dakika kumi na moja (10:11 AM), kikundi hicho kilichofukuzwa na polisi kilirudi tena wakati huu wakiacha pikipiki zao nje na kuingia kwa miguu. Kamera ziliwapiga picha wakiingia eneo la kanisa na kwenda kwenye ukumbi wa mikutano, ambapo walivunja mkutano kwa kupiga kelele na kutawanyisha waliokuwapo.
Kamera za CCTV za ghorofa ya pili zilipiga picha wahuni angalau watano wakikabiliana na kuwadhulumu watu waliokuwa wakikimbia kwenye ghorofa ya tatu. Polisi mmoja alionekana akijaribu kuingilia kati lakini alionekana kushindwa na machafuko yaliyoendelea. Nje ya kanisa, risasi zilisikika polisi wakijaribu kutawanya washambuliaji.
Miongoni mwa taarifa ambazo Runinga ya Citizen inaweza kujipigia kifua ni hii ya UFICHUZI wa kijana aliyerekodiwa akitoa maelezo ya mlolongo mzima j itinsi tukio hilo lilivyopangwa na kuratibiwa.
kijana huyo alidai kwamba yeye na wenzake walitumwa na wanasiasa wasiowajua ila kwa kuambiwa Kwamba Mbunge mmoja wa Nairobi alihusika kufadhili tukio hilo. Akizungumza katika mahojiano baada ya kukamatwa kwake, alisema kundi la vijana hao walilipwa shilingi Ksh1,000 kila mmoja kushiriki katika operesheni hiyo. Alidai walikuwa wakifuata maelekezo ya watu aliowataja tu kama "wanasiasa wenye ushawishi." Akiwemo Mbunge wa Nairobi aliyeratibu tukio hilo.
Kulingana naye, yeye alikuwa ni sehemu ya kundi la vijana wa mitaani ambao mara kwa mara huajiriwa kwa kazi mbalimbali, ambazo wakati mwingine huhusisha shughuli haramu. Aliongeza kwamba mipangilio kama hiyo si mpya kwao, akidai mara nyingi wanasogezwa na watu wanaotaka kuwatumia kwa kazi za kisiasa.
# 4. GENGE LA "CHINI YA MNAZI"
Hatimaye lilifajamika jina la Genge hilo la wahuni kuwa lilijiita "Chini ya Mnazi " baada ya kufikishwa mahakamani tarehe 16 Juni 2026, baadhi ya Washukiwa waliokamatwa. Mahakama ya Kibera iliamuru kuwekwa kizuizini washukiwa watatu waliohusishwa na uvamizi huo wa kusikitisha ndani ya Kanisa All Saints Cathedral. Watuhumiwa George Omondi Otieno, Effenburg Wanyama Khisa, na Melvin Alumasa Bwani walitokea mbele ya Hakimu Mkuu Stella Atambo baada ya kukamatwa kuhusiana na tukio la Juni 12.
Kulingana na hati za mahakama, washukiwa wanachunguzwa kwa madai ya kushiriki katika kikundi cha uhalifu kilichopangwa, kinyume na Sheria ya Kuzuia Uhalifu Uliopangwa, pamoja na njama ya kutenda kosa kubwa chini ya Kanuni ya Adhabu. Mamlaka zilisema uchunguzi wa ziada unaweza kusababisha mashtaka zaidi.
Afisa mchunguzi Constable Carrey Odhiambo aliiambia mahakama kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha washukiwa ni wanachama au washirika wa genge la uhalifu linaloitwa "Chini ya Mnazi," ambalo lilidhaniwa, kupangwa kuratibiwa na kutekeleza uvurugaji wa amani katika kanisa. Pia alidai washukiwa wengine kadhaa wanaohusiana na tukio hilo bado wako huru.
Taarifa zinasema mtuhumiwa mwingine wa nne (4) amefikishwa Mahakamani tarehe 17, 2026.
#5. JE, WAZIRI WA FEDHA JOHN MBADI ANAJUA CHOCHOTE?
Itakuwa ni ufinyu wa mawazo endapo hakutokuwepo mtu yoyote wa kudadisi kama Waziri Mbadi alihusika au lah. Haingii akirini kwamba Waziri anaweza kuwasilisha mswada wa Bajeti Bungeni kisha siku moja baadaye magenge ya Wahuni yawavamie wananchi wanaokutana kuujadili mswada ule na waziri huyo awe hajui kitu!? Tuna haki ya kuhoji hapa kwamba licha ya tukio Lile kudaiwa kuratibiwa au kufadhiliwa na Mbunge wa Nairobi, lakini ni kwa maslahi ya nani? Je tutakuwa na makosa kusema huenda waziri huyu anazo taarifa nyeti na anapaswa kuhojiwa? Kwanini kujadili mswada wa bajeti ya Taifa ambao si Mali ya mtu uwe kero kwa mtu fulani? Kwa haraka haraka, ni rahisi kufikiria kwamba Serikali haitaki hoja yoyote inayohusu kuujadili au Kupinga mswada wa bajeti wa 2026/27. Kwa mantiki hiyo Wanasiasa wanaodaiwa kufadhili magenge ya Wahuni wamo kwenye mtandao wa Serikali.
#6. WABUNGE WA KAUNTI YA NAIROBI:
Kwa mujibu wa maelezo ya kijana aliyehojiwa na Runinga ya Citizen, Wabunge wa Nairobi waliohusika katika kupanga, kuratibu na kufadhili tukio hilo na bila shaka na mengine ambayo yamekuwa yakishuhudiwa hapo nyuma.
Upekuzi wetu umebaini Kaunti ya Nairobi kuwa na takriban Majimbo 17 ya Uchaguzi. Miongoni and hayo wako Wabunge wa kujitegemea, wabunge wa chama Cha Wiper, Wabunge wa chama Cha Jubilee, Wabunge wa chama Cha UDA na Wabunge wa chama Cha ODM.
Ni Imani yetu kwamba si rahisi kwa Mbunge yeyote wa upinzani kuhusika na katika tukio hili la juzi hasa kutokana na mazingira ya kuonekana wazi kwamba polisi walishirikiana na Majambazi hao. Hakuna Mbunge wa upinzani mwenye ubavu wa kupanga tukio kama hilo kwa kushirikiana na polisi. Kwa maana nyingine upo uwezekano mkubwa wa ushiriki wa Wabunge wa UDA na ODM waliomo kwenye Broad Based arrangement. Endapo maafisa wa Upelelezi watazingatia taarifa ya wazi ya Runinga ya Citizen, baadhi ya wabunge hawa huenda wakahojiwa.
# Majimbo 17 ya Nairobi, Wabunge, na Mwelekeo wao wa Kisiasa
| Jimbo | Mbunge | Chama | Msimamo wa Kisiasa |
| Westlands | Tim Wanyonyi | ODM | Mwelekeo wa BBA (kambi ya Oburu) |
| Dagoretti North | Beatrice Elachi | ODM | Mwelekeo wa BBA|
| Dagoretti South | John Kiarie (Jaguar) | UDA | Kenya Kwanza/Serikali |
| Langata | Phelix "Jalang'o" Odiwuor | ODM | Mwelekeo wa BBA |
| Kibra | Peter Orero | ODM | Mwelekeo wa BBA |
| Roysambu | Augustine Kamande | UDA | Kenya Kwanza/Serikali |
| Kasarani | Ronald Karauri | Independent | Karibu na Serikali |
| Ruaraka | Tom Kajwang' (TJ) | ODM | Mwelekeo wa BBA|
| Embakasi South | Julius Mawathe | Wiper | Kambi ya Kalonzo (baadhi wanaiunga Linda Mwananchi) |
| Embakasi North | James Gakuya | UDA | Kenya Kwanza/Serikali |
| Embakasi Central | Benjamin Gathiru | UDA | Kenya Kwanza/Serikali |
| *Embakasi East* | *Babu Owino*| *ODM* | *Kiongozi mkuu wa Linda Mwananchi — Upinzani wa kweli* |
| Embakasi West | Mark Mwenje | Jubilee | Karibu na Serikali |
| Makadara | George Aladwa | ODM | Mwelekeo wa BBA|
| Kamukunji | Yusuf Hassan Abdi | Jubilee | Karibu na Serikali |
| Starehe | Amos Mwago | Jubilee | Karibu na Serikali |
| Mathare | Anthony Oluoch | ODM | Haijathibitishwa moja kwa moja, eneo lina mwelekeo wa Linda Mwananchi |
*Mbunge wa Viti Maalumu (Women Rep) - Nairobi:* Esther Passaris (ODM) alioneka kuwa karibu sana na Waziri John Mbadi kwenye Mijadala ya Bajeti.
#7 MAELEZO YA MCHUNGAJI CANON EVANS OMOLLO:
Akiongea katika kituo Cha Runinga Cha Citizen Tarehe 15 Juni, 2026, Kasisi/ Mchunhaji Canon Omollo alisema kilikuwa na mpango wa kuzimwa kwa Kesi kuhusiana na tukio la kuvamiwa na wahuni kwa kanisa la All Saints Cathedral na watu wanaosadikiwa kuwa vigogo wa Serikali.
Omollo alieleza sababu kubwa kuwa kuzuiwa kuandikisha maelezo kwa watu wawili walioporwa simu zao siku ya tukio na kwamba walipofika kituoni walilipwa fidia ya Ksh 24,000/- kila mmoja ili waachane na swala hilo. Hata hivyo haikuweza kufahamika ni akina nani na ni kwanini? Jambo kama hili haliwezi kufanywa na mtu asiye na ushawishi na Serikali.
# 8. MAJIBU YA SERIKALI NA VIONGOZI
Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen alithibitisha kwamba Idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) inachambua picha za CCTV. Akizungumza kanisani Nairobi Jumapili Juni 14, Murkomen alishutumu tukio hilo, akiliita kuwa lisilo la kufurahishwa kabisa. Alisema: "Hatua yetu inayofuata ya ulinzi ni kutokomeza tishio hili la magenge."
Akiongea kwenye chuo Cha Polisi eneo la Ngong, Tarehe 17, Juni 2026, Inspecta Mkuu wa Jeshi la polisi Nchini Kenya Douglas Kanja amesema Serikali haitavumilia kushamiri kwa magenge ya Wahuni na kuongeza kwamba maafisa wote wakuu wa Polisi kote nchini wamepewa maelekezo ya kuchukua hatua kali dhidi ya vikundi vya wahuni.
Mkuu wa Kanisa la Anglikana Kenya, Askofu Jackson ole Sapit, alitoa changamoto kwa vyombo vya usalama kuwakamata haraka washukiwa, akionya kwamba wakurugenzi wakuu wa vyombo vya usalama wanapaswa kujiuzulu wakishindwa kuleta wahalifu mbele ya haki.
#9.TAMKO LA NCCK NA LSK:
Muunhano wa Makanisa ya Kenya NCCK na chama Cha Wanasheria wa Kenya walitoa taarifa ya kulaani uvamizi huo na kutaka hatua za haraka: "Tunadai kwamba ofisa wa serikali aliyetajwa kama mfadhili wa wahuni akamatwe na shtakiwe mara moja."
#10. TAMKO LA ASKOFU MKUU:
Askofu Mkuu wa kanisa la Kiangikana Jackson Ole Sapit mnamo tarehe 14 Juni 2026, aliwataka Inspecta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja na Mkuu wa Upelelezi Mohammed Amin kujiuzuru kwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
# 11 TAMKO LA BARAZA LA WAISLAM
Baraza Kuu la Waislamu wa Kenya (SUPKEM) lilisema tukio hilo lilikuwa onyesho lisilokubalika la kutovumiliana kisiasa, na likaionya Kenya isije ikarudia mvutano uliotangulia udhalimu wa uchaguzi wa mwaka 2008.
Mratibu wa programu ya KHRC, Annette Nerimah, alisema wahuni walipiga kelele za "Tutam," ikionyesha walikuwa wakifuata maelekezo.
# TATHMINI YA JUMLA
*Mambo yaliyothibitishwa:
* Uvamizi ulitokea Juni 12, 2026, katika mikutano ya kiraia ya kujadili bajeti
* CCTV ilipiga picha wahuni wakiingia kwa nguvu mara mbili
*Jumla ya Washukiwa watano Wamekamatwa na wanazuiliwa kizuizini kwa siku 10 na mahakama
* Genge la "Chini ya Mnazi" linashukiwa kupanga shambulio hilo kwa ufadhili wa Wanasiasa.
*Mtu mmoja alikiri kulipwa Ksh 1,000 na kudai wanasiasa walitoa ufadhili na uratibu.
Mambo yanayohitaji uchunguzi zaidi:
*Jina la Mbunge anayedaiwa kufadhili shambulio halijatajwa wazi kirasmi bado, ingawa Citizen TV iliripoti kumhoji mtu mmoja aliyeshiriki tukio hilo "alimfichua" mbunge huyo
*Ushiriki wa polisi uliodaiwa na mtu huyo haujaungwa mkono na ushahidi wa kutosha hadharani bado
Kesi hii ipo mahakamani na upelelezi unadelea. Ni muhimu kufuatilia maendeleo ya kesi hiyo kwa makini, hasa pale ambapo jina la mbunge anayedaiwa litakapotajwa rasmi na mamlaka.
MWISHO:
Endapo watuhumiwa wote wa unyama huu hawatakamatwa na kufikishwa kwenye Vyombo vya Sheria na Wanasiasa wanaodaiwa kuratibu na kufadhili vitendo hivi kuchunguzwa na kukamatwa, basi ni maoni yetu Kwamba hata hao wachache waliokamatwa miongoni mwa Genge la watu karibu mia moja watakuwa ni Kondoo wa kafara'. Ni
Hii ni kwa kwa Sababu mzozo wa fitina utakuwa haujakatwa.

