#NI DHAHIRI SHAHIRI WAHUNI NI MTAJI WA UDA

 Mzozo wa hivi majuzi tarehe 19 Juni,

2026, kati ya Mbunge wa Kuresoi Kaskazini Alfred Mutai na Gavana wa Nakuru Susan Kihika uliotokea wakati wa hafla ya maendeleo huko Sirikwa, ulisababisha vurugu zilizopelekea watu watatu kujeruhiwa kwa risasi. Mgogoro huo umeonyesha mpasuko mkubwa ndani ya chama cha UDA lakini kubwa zaidi lililojitokeza ni Ukweli kwamba matuzi ya magenge ya Wahuni ni mtaji wa Kisiasa wa chama cha UDA. Kwa sasa hakuna yeyote anayeweza kupingana na kauli hiyo.

Baada ya kuwatuma wahuni hao kuvuruga mikutano ya wapinzani na makongamano mengine ya Asasi za Kiraia na Wanaharakati sasa wamedhihirisha kugeukana wao kwao.

Misingi ya vyama:

 Mbunge Alfred Mutai anawakilisha Eneo Bunge la Kuresoi Kaskazini kupitia tiketi ya chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA), ambacho ndicho chama cha Susan Kihika, hivyo basi, wote wawili yeye na Gavana Susan Kihika wanatoka katika chama kimoja.

Chanzo cha Mgogoro: 

Mvutano wao unatokana na ushindani mkubwa wa kisiasa na utawala wa maeneo (supremacy battles) ndani ya Kaunti ya Nakuru. Inadaiwa mgogoro huo uliibuka baada ya pande hizo mbili kutofautiana kuhusu nani anayepaswa kudhibiti na kuandaa hafla hizo za uwezeshaji.

Hali ya Kisheria (Kurekodi Maelezo): Kufikia sasa viongozi hao hawajaandikisha maelezo pamoja. Badala yake, Huduma ya Kitaifa ya Polisi National Police Service (NPS) ilianzisha msako mkali dhidi ya Mbunge Alfred Mutai, wakimtaja kama mshukiwa mkuu kufuatia ufyatuaji wa risasi uliojeruhi wananchi.

Uhusiano wa Mgogoro na UDA: 

Vurugu hizi zinaonekana wazi kuwa ni mpasuko au vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama cha UDA (UDA vs UDA). Viongozi wengi wanaonyesha kutoelewana hadharani huku wanasiasa wakigawanyika katika kambi tofauti kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.

Picha ya Siasa kuelekea 2027: 

Tukio hili linaashiria hatari ya kuongezeka kwa vurugu, na kutovumiliana kisiasa, na matumizi ya vijana kama vibaraka kufanya fujo dhidi ya wanasiasa wanaopingana.

 Hali hii inatoa picha ya uwezekano wa vurugu na machafuko uanayosababishwa na wanasiasa yanayoweza kujitokeza katika kipindi hiki Cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Lakini kubwa zaidi ni pale ambapo Wahusika ni wanachama wa chama kinachoongoza Serikali ambacho kinatakiwa kuwa mfano ili kiweze kuwadhibiti wengine.

Post a Comment

Previous Post Next Post