#MWENENDO WA MATUKIO NAIROBI, JUNI 25, 2026

Siku ya tarehe 25 Juni,2026 imekuwa siku ya

mapumziko katika maeneo ya nchi hasa Nairobi kinyume Cha taarifa za awali za serikali kwamba itakuwa.siku ya kawaida na kwamba Kila mwananchi ataendelea na shughuli zake za kijamiinau kiuchumi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba serikali hiyohiyo iliyotoa arifa hiyo ndiyo hiyohiyo iliyofunha njia kuu za kuingia mjini Nairobi.

Maanya nyingine mtu yeyote aliyekuwa na mpango wa kwenda mjini au wanafunzi wa kwenda shuleni wasingeweza kufanya hivo.

 # 1. FAMILIA ZA WAATHIRIKA WAZUIWA BUNGENI

Familia za Wakenya waliouawa wakati wa maandamano ya Gen Z ya Juni 2024 hazikuweza kufika Bungeni baada ya vikosi vya polisi kuzuia barabara zinazoelekea eneo la Majengo ya Bunge na kuziamrisha ziondoke.

Familia hizo, zikiwa pamoja na wanaharakati na viongozi wa United Alternative Government, zilikuwa zimetembea kutoka Hoteli ya Serena wakikusudia kuweka maua Bungeni na maeneo mengine ambapo waandamanaji waliuawa mwaka 2024.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Nairobi Issa Mohamud alitetea hatua za usalama na kuiomba kikundi hicho kutawanyika baada ya kuweka maua kwenye vizuizi vya polisi, akisema: "Wakiwa Wakenya wa kweli na waacha sasa, ili Wakenya wengine waendelee na shughuli zao

Hata hivyo baadaye familia za wahanga, wanaharakati na viongozi wa kisiasa walioshiriki Maandamano hayo waliruhusiwa kuweka maua kwenye uzio wa nyaya za usalama uliowekwa kuzunguka majengo ya Bunge badala.ya ndani ya majengo hayo.

Kuna taarifa za kukamatwa kwa baadhi ya wanafamilia wa waathiriwa wa ukatili wa polisi wa mwaka 2024, kwenye maandamano hayo anleo waliokataa kutii amri ya polisi ya kuondoka eneo ya tukio baada ya kuweka maua. Inasikitisha kuona haraka iliyokuwepo kwa maafisa wa polisi kuwataka wafiwa kuondoka kwa vile hakukuwa na muda maalumu uliyokuwa umeratibiwa kwa wahusika kufika, kuweka maua na kufanya maombi katika eneo like.

#2.VIZUIZI NA KAMATAKATA ENEO LA CBD

Kufikia saa 11 asubuhi tarehe 25 Juni 2026, polisi walikuwa wamesimika vizuizi kwenye barabara kuu kadhaa zinazoingia mjini Nairobi ikiwemo Thika Road, Kiambu Road, Jogoo Road, Outering Road, na njia kadhaa zinazoelekea CBD  na matatu yalizuiwa kuingia mjini.

Licha ya mipango ya maandamano ya amani, waandamanaji kadhaa walikamatwa na kupakiwa kwenye malori ya polisi. Video moja ilionyesha mtu mwenye suti akivutwa barabarani na maafisa wa polisi. Alihoji mara kwa mara kwa nini anakamatwa, lakini maafisa hawakumsikiliza na wakamlazimisha kuingia kwenye lori  huku akiwa amebeba bendera ya Kenya tu

Awali Kamanda Mohamud alishatangaza siku moja kabla kwamba maandamano yoyote makubwa ndani ya CBD ni haramu, akisema hakupokea taarifa rasmi kama inavyohitajika kisheria.

#3. GHASIA ENEO LA GITHURAI

Githurai ilikuwa moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi kwa kuzuka kwa vurugu za hapa na pale, mapema asubuhi hadi baadaye mchana, watu walizuiwa kusafiri tangu saa 12 usiku baada ya polisi kusimamisha magari ya umma na ya binafsi. Vizuizi vya polisi viliwekwa katika Ruiru Footbridge, Ruiru Bypass, Githurai Underpass na Allsops kando ya Thika Road, na baadhi ya matatu yalirudishwa nyuma.

Hali ya wasiwasi iliendelea katika eneo hilo siku nzima, huku taarifa za ujasusi zikiwa zimeorodhesha Githurai miongoni mwa maeneo yanayoweza kuwa hotspot za maandamano, pamoja na Thika Town, Kitengela na maeneo mengine yanayozunguka Nairobi.

# 4. HALI YA UTULIVU SEHEMU NYINGI ZA MJI

Katikati ya mji wa Nairobi ilikuwa tulivu asubuhi, huku biashara nyingi zikibaki zimefungwa na maafisa wa usalama wakiongeza doria na kujenga vizuizi. Biashara nyingi katika CBD zilifungwa, huku wasafiri wengi wakitatizika kuingia mjini.

Martha Karua wa People's Liberation Party aliuliza maswali kuhusu madai kwamba wahalifu walipangwa mjini kupitia maandamano, akisema: "Haiwezekani kuwepo kwa wahuni aunwahalifu au kufanyika kwa unyang'anyi wowote kwa kuzingatia uwepo wa mamia ya polisi.

# 5. MUKTADHA MPANA

Siku hii ina uzito mkubwa:

 Miaka miwili baada ya maandamano ya 2024, familia nyingi bado zinatafuta haki. Ripoti ya Human Rights Watch ya 2026 inasema angalau watu 41 wanaohusiana na maandamano bado hawajulikani mahali walipo, 26 kutoka 2024 na 15 kutoka 2025. 

Serikali imeanza mpango wa fidia kwa waathirika wa ukiukwaji wa haki za binadamu unaohusiana na maandamano kuamzia mwaka 2013 na 2025, chini ya Jopo la Wataalamu linaloongozwa na Prof. Makau Mutua.

Kwa ujumla, ingawa mji ulikuwa na utulivu kiasi, usalama ulikuwa mkali sana, na hisia za maumivu na kudai haki zilidhihirika wazi katika vitendo vya familia za waathirika.

Post a Comment

Previous Post Next Post