
Kuhusu nini hasa sababu na matunda au faida ya Kenya kutokana na hatua yake ya kuwapeleka polisi wake Nchini Haiti. Aidha pamekuwepo maswali kuhusu nini lilikuwa lengo la kupelekwa kwa vikosi vya polisi nchini humo endapo magenge ya Wahuni na Majambazi ndani ya Kenya yameshindikana kudhibitiwa.
Kwa yeyote anayejiuliza swali hili, jibu ni jepesi sana. tatizo si utendaji wa polisi ila ni mfumo wa uendeshaji wa Serikali unaowataka Polisi kufanya kazi kwa matakwa ya watawala na si Sheria.
Ongezeko la visa vya wahuni na majambazi vinavyoshudiwa kenya si kwa kushindwa kudhibitiwa serikali , ila ni njia ya Serikali iliyopo madarakani kutumia dhana ya unafiki kutimiza azma yake ya kisiasa.
Kikosi cha mwisho cha polisi wa Kenya kilihitimisha rasmi misheni yake na kurejea nchini mnamo mwezi Aprili 2026, na hivyo hakuna tena maafisa wa Kenya nchini Haiti.
Kenya iliongoza Misheni ya Kimataifa ya Msaada wa Usalama (MSS) chini ya uidhinishaji wa Umoja wa Mataifa ili kukabili magenge ya wahalifu Nchini Haiti.
1. Kenya ilipeleka lini vikosi, idadi ya vikosi na askari wangapi kwa kila kimoja?Kenya ilipeleka jumla ya vikosi vitano (5) vya maafisa wa polisi katika awamu tofauti. Hata hivyo, hakuna idadi kamili ya askari waliotumwa kwa pamoja inayozidi 1,000 kwa wakati mmoja, kwani askari walikuwa wakienda na kurejea baada ya muda wao wa kazi kuisha.
Baadhi ya makundi yalitangazwa na vyombo vya habari na mamlaka kama ifuatavyo:
Kikosi cha Kwanza:
Takriban maafisa 400 waliondoka nchini na kuwasili Haiti mnamo Juni 2024.
Kikosi cha Pili: Takriban maafisa 200 walisafiri mwishoni mwa 2024.
Kikosi cha Tatu:
Takriban maafisa 217 waliondoka Kenya mnamo Januari 18, 2025 na kuwasili Port-au-Prince.
Kikosi cha Nne:
Maafisa 144 waliondoka Kenya baadae katika awamu mbalimbali.
Kikosi cha Tano:
Maafisa 230 waliwasili Haiti mnamo Desemba 8, 2025.2.
Je, bado kuna polisi wa Kenya nchini Haiti? Hapana, misheni ya awali ya kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa ilifikia tamati rasmi Aprili 2026.
Kikosi cha mwisho kabisa cha maafisa wa Kenya kiliondoka Haiti na kurejea nchini Kenya mnamo mwezi Aprili 2026.
3. Je, lengo la misheni hii nchini Haiti lilifikiwa?
Maoni yamegawanyika:
Kwa upande wa Serikali ya Kenya na mamlaka za Haiti, misheni hiyo inatajwa kuwa ilipata mafanikio makubwa kutokana na kufanikiwa kufungua njia kuu, kurejesha usalama katika maeneo muhimu kama uwanja wa ndege wa kimataifa na bandari, na kupunguza nguvu ya magenge.
Hata hivyo, ripoti nyingine za kimataifa zinabainisha kuwa magenge hayo yaliendelea kudhibiti maeneo mengi na yalikuwa na nguvu kubwa.
4. Nchi gani nyingine zilizopeleka askari na ni ipi iliyopeleka wengi zaidi?
Nchi zilizochangia askari wa polisi na kijeshi ni pamoja na Jamaica, Bahamas, El Salvador, Guatemala, Belize, Chad, na Canada. Kati ya nchi zote, Kenya ndiyo iliyopeleka askari wengi zaidi.
Kenya ndiyo iliongoza misheni hii tangu mwanzo na ilitoa kiasi kikubwa cha nguvu kazi ikilinganishwa na nchi zingine zote kwa pamoja.
5. Nani aliyekuwa mfadhili wa mpango huu mzima? Marekani ndiyo iliyokuwa mfadhili mkuu wa mpango huu, ikitoa ufadhili mkubwa wa kifedha na vifaa ili kufanikisha utumaji wa askari hao.
6. Kwanini Serikali ya Kenya ilipeleka Polisi na sio Jeshi (KDF)? Hatua hii ilitokana na misingi ya kisheria na kidiplomasia. Kikatiba nchini Kenya, Jeshi (KDF) hutumika ndani ya nchi na nje ya nchi katika hali ya vita kamili au dharura kubwa. Kwa upande mwingine, utumaji wa askari katika nchi za nje kwa ajili ya kulinda amani na kusaidia polisi wa ndani (Haitian National Police) ni kazi inayohusu usalama wa raia, jambo ambalo kisheria liliangukia vyema zaidi kwa maafisa wa Polisi.
7. Kwanini Marekani haikupeleka jeshi lake badala yake ikafadhili nchi zingine?Sababu kuu ilikuwa ni ya kihistoria na kisiasa. Historia ya nyuma ya uingiliaji wa kijeshi wa Marekani nchini Haiti haikupokelewa vyema na wananchi wa huko, na uwepo wa wanajeshi wa Marekani mara nyingi huzua maandamano na hisia kali za ukoloni.
Ili kuepusha mivutano ya kisiasa na kulinda mamlaka ya Haiti, Marekani iliamua kufadhili kikosi cha kimataifa kilichoongozwa na nchi zisizo na historia ya kuikalia Haiti (kama Kenya) ili kuleta uhalali mbele ya jamii ya kimataifa.
8. Kwanini Polisi a Kenya walionekana kufanya Nchini vizuri Haiti wameshindwa kudhibiti magenge ya wahuni nchini Kenya?
Sababu kuu:
Kwanza, polisi wa Kenya nchini Haiti walikuwa wakifanya kazi chini ya misingi tofauti kabisa, wakiwa na vifaa maalumu vya kijeshi na silaha nzito, na walikuwa na kinga na mamlaka ya kimataifa ya kutumia nguvu kubwa, tofauti na utendaji wao wa kawaida nchini Kenya unaofungwa na mifumo ya ndani ya kiutendaji, sheria za ndani na haki za binadamu. Pili, vikosi vilivyotumwa Haiti vilijumuisha vitengo maalum na vya kipekee (kama Recce Squad na GSU) vyenye mafunzo ya nguvu ya kukabiliana na waasi au majambazi, huku kukiwa na ushirikiano mkubwa wa vifaa na ndege kutoka kwa washirika kama Marekani na El Salvador.
Nchini Kenya, udhibiti wa uhalifu unahusisha changamoto ngumu za kijamii, kiuchumi, na kisiasa zinazohitaji mikakati ya kitaasisi badala ya nguvu za kijeshi pekee.
Aidha Polisi wa kenya wanafanya kazi kwa mfumo wa Command wa kutii matakwa ya watawala zaidi kuliko Sheria inavyotaka. Kwa maana nyingine uhuru wa kiutendaji kazi walioupata nchini Haiti ni tofauti na hali halisi Nchini Kenya ambapo utendaji wao kazi unaathiriwa na ushawishi au mfumo wa Serikali na Siasa.