#THE KENYAN FOOTBALL FAN SLAVERY

 #Maelfu na mashabiki wa Timu ya Soka ya Arsenali ya nchini Uingereza wamejitokeza katika miji mikuu ya Kenya kushangilia ushindi

wa Ligi Kuu ya Uingereza uliotwaliwa na klabu ya Arsenal.

Hata hivyo, hali hii imezua mjadala mzito baada ya kubainika kuwa jijini London (Uingereza) hakuna utambuzi wowote unaofanywa na wazungu au japo kuutambua Mchango wao, au hata  kuonyesha wanajua uwepo wa mashabiki hawa wa Kenya kwa nguvu na Ari kubwa waliyonayo wakenya kwa Timu ya Arsenal.

Makao makuu ya timu ya Arsenal yapo kwenye eneo la Islington, Kaskazini mwa mji wa London nchini Uingereza, na uwanja wao wa nyumbani unajulikana kama Emirates Stadium. 

Uamuzi wa kuacha shughuli za kujenga uchumi au kazi zingine za kijamii na kupoteza muda mwingi kwa ajili ya kushabikia timu kutoka nchi nyingine ni suala linaloleta utata mkubwa. 

Jambo linaloumiza zaidi ni kwamba hakuna juhudi au nguvu zinazowekezwa katika klabu za ndani za Kenya kulinganisha na zile zinazotumika kushangilia ligi za mbali 

Tumejaribu kupekua sababu za ushabiki wa aina hii usiokuwa na tija wa nguvu za vijana zinazotumika na kubaini changamoto kadhaa za kijamii na kiuchumi zinazowakabili vijana:

#Uchambuzi wa Sababu za Hali Hii

Ukosefu wa Ajira na Kuzubaa:

Ukosefu wa ajira/kazi umesababisha kundi kubwa la vijana kubaki bila shughuli maalumu. Kushangilia timu za kigeni kunakuwa njia ya kupitisha muda (idleness) na kujaza utupu unaosababishwa na ukosefu wa ajira 

Kukosekana Mitaji ya Kibiashara:

Serikali kukosa/ kushindwa kuwawezesha vijana kwa mitaji au kufadhili wa shughuli za biashara na uzalishaji ili kujiinua kiuchumi na kushiriki kikamilifu ujenzi wa taifa.

Uwekezaji Unaowafaidisha Wageni:

Ligi ya Uingereza imewekeza mabilioni ya fedha katika utangazaji na ubora wa mchezo. Kinyume chake, klabu za humu nchini zinakosa fedha za kutosha, kukosekana wadhamini, na miundombinu ya kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wetu.

Kukosa Uwezeshaji wa kukuza Vipaji:

Kinyume na mataifa ya nje Kenya haijatenga bajeti Wala sera madhubuti ya kukuza vipaji vya mpira wa miguu kuanzia kwa vijana wenye rika ndogo. Kwa vile huwezi kumnenepesha ng'ombe siku ya soko, mafanikio ya kesho yanapaswa kuanza leo.

Fursa ya Kuondoa Msongo wa Mawazo:

Vijana wengi wasio na kazi/ajira huichukulia hii kama nafasi ya kujumuoka na kutuliza mawazo ya kwa uraibu wa mpira wa Soka la ulaya. Kwa wengi, msisimko wa ligi za kigeni hutoa burudani na njia ya kusahau changamoto ngumu za kiuchumi zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku.

Dharau kwa Soka la Nyumbani:

Dhana ya Kudharau Michezo ya Nyumbani na Kupenda ya nje. Kuna mtazamo hasi miongoni mwa jamii kuwa soka la Kenya ni la "chini" (linalodharaulika), huku wakiamini ligi za nchi za magharibi ndio kilele cha soka lenye mvuto na hadhi.

Kukosa Uwezeshaji kutoka Serikalini:

 Soka la Kenya linakabiliwa na uhaba wa ruzuku kutoka serikalini na ukosefu wa viwanja vizuri vya kukuza vipaji. Hii inazifanya klabu za nyumbani kushindwa kujitangaza na kushindana ili kuvutia mashabiki.

Ushabiki wa Makundi Rika:

 Vijana wengi hujiingiza katika ushabiki huu mkubwa ili tu kwenda sambamba na marafiki zao na kujumuika katika makundi ya rika zao. Kutengwa na kundi hufanya mtu ajihisi amepitwa na wakati.

 Dhana ya Umagharibi (Eurocentrism):

 Kuna fikra zilizojengeka miongoni mwa jamii zetu zinazoamini kuwa kila kinachotoka Ulaya au nchi za magharibi ni bora na cha kisasa zaidi kuliko vilivyomo ndani ya nchi yetu. Hii inapelekea kupenda michezo yao na kuisahau ya nyumbani.

Toa maoni yako....



Post a Comment

Previous Post Next Post