#USALAMA WA RAIS WA KENYA HATARINI

 Usalama wa Rais William Ruto wa Kenya uko hatarini baada ya kikosi Cha itifaki ya ulinzi wa Rais kuonekana

kushindwa kazi. Hali hiyo ya Rais kukosa ulinzi madhubuti  imedhihirika leo tarehe 24 Mei 2026 kwenye mkutano wa kisiasa wa Rais eneo la Ganze, kilifi mkoa wa Pwani.

Katika mkutano huo mtu mmoja alifanikiwa kupenyeza kikosi Cha ulinzi wa Rais na kumvamia jukwani na kumkumbatia Rais Ruto huku akiwa amebeba Biblia. 

Cha ajabu ni kwamba hata baada ya kumfikia Rais na Kutaka kupiga naye pambaja, walinzi wa Rais waliokuwa usingizini walikurupuka wote kukimbia kumwondoa mtu huyu kisha wote waliondoka kumfuatilia mtu huyo huku Rais akibaki bila ulinzi.

Visa vya Rais William Ruto kuvamiwa, kuzomewa, au kukatiziwa hotuba jukwaani vimekuwa vikitokea mara kwa mara katika mikutano ya Rais Ruto. Kumekuwepo na sababu mbalimbali zinazohusishwa na visa hivyo zikiwemo, ukosoaji wa sera zake za kiuchumi, mizozo mikali ya kisiasa, na hasira za wananchi kuhusu gharama ya maisha. Hali hizi mara nyingi huchochewa na mambo yafuatayo:

Uzembe wa Kikosi Cha Ulinzi wa Rais:

Kwa vile Matukio haya yamekuwa yakijirudia mara kwa mara, Kuna dalili za uzembe wa wazi wa Kikosi Cha Ulinzi wa Rais.

Maisha Magumu:

Wananchi wengi wamekuwa wakionyesha kutoridhishwa kwao kutokana na tabia ya Kuzomea na alama za kidole komoja kumaanisha Muhula mmoja, "one term''

Rundo la Tozo/Kodi:

Sababu nyingine ni mzigo wa tozo, Makato au kodi, mfumuko wa bei za bidhaa, na ahadi ambazo hawajaziona zikitekelezwa tangu serikali ya Kenya Kwanza iingie madarakani.

Mivutano ya Ndani ya Kiserikali:

 Baada ya mtafaruku wa kisiasa uliomhusisha aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na kuibuka kwa mabadiliko ya serikali, kumezuka mgawanyiko wa kisiasa hata ndani ya ngome kuu za Rais. Hali hii imewafanya wakazi wa maeneo hayo kupinga hadharani viongozi wanaomuunga mkono rais.Kusambaa kwa 

Utamaduni wa Vijembe:

 Katika mikutano yake ya hadhara, Rais na viongozi wengine wamekuwa wakitumia jukwaa kujibizana na kuwarushia vijembe wapinzani na viongozi wenzao, jambo linalobadili mwelekeo wa mikutano ya kimaendeleo na kuchochea hisia za wafuasi tofauti.

 Rushwa/Ufisadi:

 Malalamiko ya wananchi kuhusu ufisadi na uhaba wa huduma muhimu huwasukuma baadhi ya vijana kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu na kuvuruga mikutano kama njia ya kufikisha malalamiko yao.

Dalili za Kuchoshwa na Utawala wa Ruto:

Matukio haya ni dalili/ishara ya wananchi Kuchoshwa na Utawala wa Rais Ruto. Tangu Rais Ruto aingie madarakani, kumekuwa na zaidi ya visa 10 vya vurugu, uzomeaji, na uvunjifu wa kiusalama katika ziara zake. 

Baadhi ya matukio makuu yaliyojitokeza ni pamoja na:

Mwezi Aprili Tar 12, 2026, Rais Ruto alizomewa hadharani na umati ulioanza kupiga kelele alipokuwa ziarani Mombasa.

 Mwezi Februari tar 7, 2025, Vijana wenye hasira walimzomea rais na msafara wake walipokuwa wakizindua miradi Isiolo, huku baadhi ya viongozi wakishindwa kutuliza ghasia.

 Novemba tar 17, 2024, Umati ulimzomea Rais Ruto wakati akihutubia kwenye ibada ya kanisa Katoliki dayosisi ya Embu, tukio lililolaaniwa na viongozi wa chama cha UDA.

Mwezi Mei tar 19, 2024, Mwanamume mwingine alirusha kiatu na kumpiga nacho rais wakati akihutubia wananchi Kehancha, Kaunti ya Migori.

Mwezi Machi 2024, Kundi la wananchi liliripotiwa kumzomea na kuonyesha uhasama katika Kaunti ya Bomet na Kericho, hali iliyosababisha serikali kuwakamata baadhi ya waandamanaji na wachochezi.

Mwezi Januari 2024,  Katika soko la Kangeta, Meru, Ruto alilazimika kuingilia kati na kukemea umati uliokuwa unamzomea Gavana Kawira Mwangaza alipopewa nafasi ya kuongea.

Mwezi Machi 2026, Ziara yake katika eneo la Mlima Kenya (kaunti kama vile Murang'a na Kiambu) ilikumbana na mvurugano na uzomaji uliowalenga pia viongozi wakuu walioandamana naye.

Mwezi Machi 2026, Msafara wa Rais ulipata vurugu na kusimamishwa kwa muda na vijana waliokuwa na hasira katika eneo la Kawangare, Jimbo la Dagoretti Kaskazini.

Hakuna Rais mwingine wa Kenya miongoni mwa Marais waliostaafu aliyewahi kukumbwa na kadhia ya aina hii katika ulingo Siasa.





Post a Comment

Previous Post Next Post