Kuna tangazo linalohusika na kilimo linalorushwa hewani
na Runinga ya Citizen linaloupotosha Umma kwamba Nyuki ni mnyama.Ni vema tangazo hilo likaondolewa au kubadilishwa. Tangazo hilo linahusika na kipindi Cha ukulima cha 'Kenya's Gold' ambacho hupeperushwa na Mtangazaji Violetta Ngina siku za wiki kuanza Jumatatu hadi Ijumaa.
Tunadhani kwa kuwa Vyombo vya habari licha ya kuhabarisha pia huelimisha, ni vema maana za maneno au majina ya vitu au wanyama vikatumika vema ili jamii ipate kuelewa vema.
Mwanafunzi aliyefundushwa darasani kwamba Nyuki ni mdudu anaweza kupata shida kukielewa kipindi.
