
Upekuzi wetu umebaini kwamba Samia Suluhu ambaye aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania Tarehe 19 Machi, 2021 baada ya kifo Cha mtangulizi wake, Hayati John Magufuli ametunukiwa shahada za tuzo za heshima zaidi ya Saba(7) kwa hadi kufikia mapema mwaka 2026.
Hii ni Kasi kubwa ambayo hakuna Rais yeyote wa afrika wakiwemo marais wapigania uhuru katika nchi za afrika kama vile Nelson Mandela, Julius Nyerere, Joackim Chissano, Cyril Ramaphosa, Akinwumi Adesina n.k waliowahi kupewa shahada za heshima kwa kipindi kifupi na kwa idadi sawa na ilivyo wa Samia Suluhu wa Tanzania, na hasa ukilinganisha juhudi na kazi walizozifanya kwenye nchi zao na kile anachikifanya Tanzania.
#Orodha ya Shahada za Heshima za Rais Samia:
I) UDSM, Tanzania (2022): Doctor of Letters (Haki za Binadamu/Elimu).
ii) Jawaharlal Nehru University, India (2023): Doctor of Philosophy (Uhusiano wa India-Tanzania).
iii) SUZA, Zanzibar (2023): Doctor of Philosophy (Utalii).
iv) Ankara University, Uturuki (2024): Doctorate in Economics.
v) Korea Aerospace University (2024): Doctorate in Aviation Management.
vi) Mzumbe University (2024): Honoris Causa.
vii) Nasarawa University, Nigeria (2026): Doctor of Philosophy (Uongozi).
*Tuzo ya Chama cha Madaktari:
*Rais Samia alitunukiwa tuzo ya Global Goalkeeper Award (Feb 2025) na Gates Foundation kwa kupunguza vifo vya mama na mtoto.
MUHIMU
Ni vema itambulike hapa kwamba Samia Suluhu Hassan hana Shahada ya Taaluma ya Udaktari(PhD) ila Udaktari alionao unatokana na tuzo za Shahada za heshima.
Ukilinganisha na Marais walimtangulia kwa mfano:
Hayati Benjamin William Mkapa, ayekuwa na kiwango Cha Elimu ya Shahada ya Uzamili, alitunukiwa jumla ya shahada za heshima nne (4) kwa Kipindi Cha miaka kumi (10)
Rais msitaafu Jakaya Kikwete mwenye Taaluma ya Shahada ya kwanza (Bachelor 'degree), alitunukiwa takriban Shahada za heshima Saba (7) akiwa madarakani miaka kumi 10) lakini jumla ni 11 ukiongeza na alizopata baada ya kuondoka uongozini.
Hayati John Magufuli ambaye anatajwa kuwa mchapa kazi kuliko Samia Suluhu, alikuwa na kiwango Cha juu Cha Elimu Cha Shahada ya Uzamivu (PhD) alitunukiwa shahada moja (1) ya heshima ya Udaktari inayotambulika kutoka chuo kikuu Cha Dodoma kwa kipindi Cha miaka Sita (6) ukijumlisha ule mwaka mmoja wa awamu ya pili ya uongozi wake kabla ya kufikwa umauti.
Sasa unaweza kulinganisha mifano hii mathalani muda aliokaa madarakani Hayati Magufuli, kiwango Cha utendaji wake wa kazi na idadi ya tuzo za heshima alizotunukiwa kwa tathimini linganifu na muda aliokaa madarakani Samia Suluhu, kiwango Cha utendaji wa kazi na idadi ya tuzo za heshima alizopewa unaweza kudhani ni biashara ya aina fulani.
Kimsingi idadi ya tuzo hizi za sifa na heshima haiendani na Kasi ya maendeleo ya Tanzania na Sura ya nje ya Tanzania kwa sasa ukilinganisha awamu ya uongozi wa Samia na ule wa Magufuli. Kuna tetesi kwamba wapambe na washauri wake wanahusika katika ushawishi wa kutolewa kwa tuzo hizo ili kumjengea sifa na hadhi ya kimataifa.
Mifano kutoka kwa Marais wengine wa afrika Mashariki:
Rais William Ruto wa Kenya mwenye kiwango Cha Elimu Cha Shahada ya Uzamivu(PhD) ametunukiwa Shahada mbili (2) za heshima kwa kipindi Cha miaka minane(4), Kwa maoni yetu kiwango Cha Utendaji kazi wa Rais Ruto, kwenye nchi yake ni zaidi ya tuzo alizopewa. Bila shaka wanaozitunuku hawajamwona.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda mwenye kiwango Cha Elimu Cha Shahada ya kwanza (Bachelor's degree) kutoka Chuo kikuu Cha UDM ametunukiwa tuzo za shahada za heshima Tano (5) kwa kipindi Cha zaidi ya miaka ishirini (20)
Sasa hapa tunaye Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania ambaye anaibuka kidedea kutoka kwenye Ombwe la kifo Cha mtangulizi wake ambaye matendo na kauli zake haziakisi chembe zozote za kuhodhi tuzo lukuki za shahada za heshima zilizoorodheshwa hapo juu.
Rais ambaye anashinda uchaguzi katikati ya Vurugu na machafuko kwa asilimia kubwa kuliko Rais mwingine yeyote wa Tanzania, huku wapinzani wake wakiwa kizuizini na wengine wakiwekewa mikingamo ya Aina mbalimbali.
Tuangalie hasa ni kwanini tuzo za heshima za aina hii hutolewa:
#Sababu za kutunukiwa:
Japo kwa mukhutadha Samia Suluhu amelitunukiwa tuzo hizi kwa lengo kuimarisha diplomasia ya uchumi wa nchi kuongeza uwekezaji, mageuzi ya kisekta utalii, elimu, nishati, na kuimarisha haki za binadamu, hali ni Tofauti ndani ya Tanzania.
Umuhimu:
Tuzo hizi zinalenga kuongeza heshima ya Tanzania kimataifa na kuvutia wawekezaji, ikionyesha mwelekeo mpya wa utawala wake wa 4R (Reconciliation, Resilience, Reform, Rebuilding). Lakini kwa upande mwingine jiulize ni mwekezaji gani anayeweza kuwekeza kwenye nchi ambayo Rais anakiri kwamba watu,makundi au magenge ya vijana wasio watanzania waliohusika kufanya vurugu, ghasia na hata mauaji wakati wa uchaguzi kwenye nchi ambayo Ina Vyombo vya ulinzi.
Na licha ya hayo hakuna kiongozi yeyote wa idara za usalama aliyefukuzwa kazi au kuwajibishwa, Kisha baadaye Rais huyo anajiundiantume ambayo inakiri kwenye taarifa yake kuwepo makundi magenge ya watu waliopewa mafusho ya uharamia kwenye misitu ya nchi hiyo, majengo mbalimbali na hawakunduliwa.
Na licha ya tume hiyo kuyabainisha hayo, ikiwemo vifo vya raia, na uharibifu wa Mali, bado hakuna uwajibishwaji na wakuu wa idara zote za usalama wanasalia kwenye nafasi zao. Huu ni usanii wa viwango vya kimataifa unaolenga kuihadaa Dunia kwa kinachoendelea ndani ya Tanzania.
#MAGUFULI HAWEZI KUSAHAULIKA
Kuna sababu nyingi zinazowafanya watanzania kutokumsahau Magufuli. Kutokana na hali ilivyo sasa nchini humo Watanzania walio wengi wanaiona tofauti kubwa ya kiutendaji kati ya Samia Suluhu na Hayati John Magufuli.
Ingawa Rais Samia alisifiwa mwanzoni kwa kufungua nchi kidiplomasia, kurejesha uhuru wa kisiasa, na kuruhusu mikutano ya hadhara, hata hivo baadaye hali ilibadilika aliposhika Kasi ya uongozi, na mbaya zaidi kwenye Matukio ya uchaguzi uliopita wa Okotoba 29, mwaka Jana 2025.
kuna maeneo muhimu ambayo wananchi wengi wanahisi hayajatekelezwa vema kama ilivyokuwa chini ya Magufuli.
Hapa Kuna mifano michache:
#1. Hali ya Kupanda kwa Gharama ya Maisha
Wananchi wengi wanalalamikia kupanda kwa kasi kwa gharama za maisha, bei za mafuta, tozo za Kodi lukuki kwenye biashara hata ndogo na kwenye miamala ya Benki na simu, tozo kwenye bidhaa muhimu, ni miongoni mwa mambo kuwakera wananchi wa kawaida ikilinganishwa na enzi ya Magufuli ambaye alijulikana kwa kubana matumizi ya serikali na kudhibiti bei.
Hali Halisi (2026):
Ingawa serikali imechukua hatua kama kuongeza mshahara wa kima cha chini kwa 35.1% hadi TZS 500,000, athari za kiuchumi duniani, ikiwemo kupanda kwa bei za mafuta, zimeendelea kuathiri maisha ya kila siku ya Watanzania.
Utawala wa Samia unakabiliwa na shinikizo kubwa la kiuchumi, huku wananchi wakihisi utulivu wa bei uliokuwepo zamani umepotea.
Kuwarudisha Serikalini Watu Walioachwa na Magufuli
Tangu kifo cha Hayati Magufuli pamekuwepo na hoja za misingi ya uwajibikaji wa Serikali ya Samia Suluhu kwa kudhibiti mtandao wa ufisadi ambao kwa kiasi kikubwa uliaminika kudhibitiwa na Magufuli. Watanzania walio wengi wanamwona Samia Suluhu kama mtu aliyeshindwa kufuata nyayo za mtangulizi wake za kutumbua Majipu' na badala yake kuwarudisha Serikalini Watu ambao kimsingi Waliachwa '' kutumbuliwa'' na Magufuli kwa kushindwa kazi au kwa tuhuma za ubadhilifu.
Baada ya kushika hatamu za uongozi, Samia aliwarudisha serikalini baadhi ya watu wanaosadikiwa kuwa wanamtandao wa Rais msitaafu Jakaya Kikwete ambao waliondolea na Magufuli kwa kuukumnatia ufisadi.
Ni vema ieleweke vema kwamba Sera za Magufuli zilitofautiana na za Kikwete. Magufuli alipoingia madarakani alitumia fagio la chuma kuuvunja mtandao wa Kikwete. Ila alipofariki, Samia aliurudisha tena baada kuukwaa Urais . Hii ndo sababu ya msingi ya yeye Samia kuonekana hajafanya vya kutosha kupambana na Ufisadi.
#2. Kuuzwa kwa Vitega Uchumi/Rasilimali za Nchi
Kuna hofu miongoni mwa wananchi kuhusu mikataba ya uwekezaji na wawekezaji wa kigeni, hasa katika sekta za bandari na rasilimali za Madini na Utalii
Mitazamo:
Wakosoaji wanahisi utawala wa Samia unatoa kipaumbele kikubwa kwa wawekezaji wa kigeni (k.m. uwekezaji wa bandari), madini, jambo linaloonekana kama kuuza rasilimali za taifa, tofauti na mtindo wa Magufuli wa kizalendo (nationalism) na kuweka mkazo katika umiliki wa Mali za ndani.
Msimamo wa Serikali:
Serikali inatetea hatua hizi kama sehemu ya "Diplomasia ya Uchumi" ya kuvutia uwekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi, na inasisitiza kuwa hawauzi nchi bali wanashirikiana.
#3. Uchumi na Uwekezaji
Uchumi umepata mabadiliko ya kimuundo, huku ukionyesha ukuaji wa kiwango cha juu kwenye makaratasi (kwa mfano, ukuaji wa GDP kutoka asilimia 3.9 mwaka 2021 hadi 5.5 mwaka 2024), lakini wananchi wanahisi ukuaji huo hauakisi hali zao za maisha.
Marekebisho ya Kodi:
Rais Samia amekemea matumizi ya nguvu katika ukusanyaji mapato yaliyokuwepo awali na kutafuta mfumo wa haki. Hata hivyo, wengi wanahisi makali ya kikodi yamezidi huku wakilalamikia mifumo mipya ya ukusanyaji kodi kuwa ya unyonyaji na ukandamizaji wa mitaji yao kupitia TRA
Deni la Taifa:
Deni la taifa limeendelea kupanda, ikilinganishwa na enzi ya Magufuli ambaye alikopesha kiasi kidogo.
Fedha inayokopwa haibainishwi matumizi ya wazi kwa Wananchi ambapo katika baadhi ya mikopo hiyo Serikali ya Samia inadaiwa kutoomba ridhaa ya Bunge kwa kushirikina na Benki kuu.
Inasemekana hii ndo ilikuwa chanzo Cha aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Hayati Job Ndugai, kushindana na Rais Samia kwa kuhoji ukopaji isipokuwa na tija, kisha Kujiuzuru na kufanyiwa mizengwe na Hatimaye alifariki kifo chenye utata.
Inadaiwa pia kwamba Ndugai alikuwa mwiba ndani ya CCM na Serikali ya Samia na alihofiwa angekuwa changamoto au kizuizi kwa Rais Samia kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopita 2025, kama angekuwa hai.
#4. Ukandamizaji wa Haki na Uhuru wa Maoni, Kuminywa kwa Demokrasia
Ingawa kulikuwa na utulivu wa awali kwenye Sera ya Samia ya (4R) Reconciliation, Resilience, Reforms, Rebuilding), kumekuwa na malalamiko ya kuendelea kwa baadhi ya sheria kandamizi na ukandamizaji wa uhuru wa kutoa maoni, hasa kwa vyombo vya habari, wanaharakati na wapinzani.
Hivi karibuni Mwezi May 2026, Samia Suluhu aliwashangaza Watanzania na Dunia kwa jumla aliposema hadharani kwamba walijadili na Rais Ruto wa Kenya aliyekuwa ziarani Tanzania jinsi ya kushirikiana kudhibiti maandamano ya Vijana wa Gen Z ambao alisema nao wanajifanya kuwa mshikamano wa Afrika Mashariki. Alimtaka Rais Ruto kuwadhibiti kwa kuwapiga mikwaju huko Kenya na wakienda Tanzania pia yeye awapige mikwaju ili kuleta utulivu na amani kwenye nchi hizo.
Picha inayojitokeza hapa ni kwamba Bado Samia Suluhu hajajifunza chochote kwa Vurugu na machafuko makubwa yalitokea nchini mwake Oktoba 29 mwaka 2025.
Hali ya sasa:
Ingawa Rais Samia amelegeza kidogo kuruhusu mikutano ya kisiasa, bado kuna matukio ya ukamataji na vizuizi, jambo linalofanya uhuru wa kweli wa maoni kuonekana kuwa na mipaka.
#5. Miradi ya Maendeleo
Miradi mikubwa ya kimkakati ni Ile iliyoanzishwa na Magufuli mifano kama Bwawa la Nyerere, Reli ya SGR, na Daraja la Kigongo-Busisi, licha ya baadhi yake kuwa imekamilishwa hapajaonekana jitihada zaidi za kuibua na kutekeleza miradi mingine zaidi kwa kasi ileile.
Tofauti:
Utekelezaji wa miradi chini ya Samia haujazingatia zaidi uwazi wa ufatiliaji wa karibu ambapo inasemekana anatumia diplomasia zaidi na wawekezaji huru akiwaachia mianya ya Wizi, jambo ambalo Wananchi wanahisi pesa nyingi zinaporwa aidha Kuna hisia kwamba kasi ya kuanzisha miradi mipya mikubwa ya "kushtua" ni ndogo ikilinganishwa na kasi ya "bulldozer" ya Magufuli.
#6. Upendeleo katika Uteuzi (Nepotism)
Rais Samia amekabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusu uteuzi wa viongozi, na hasa nafaoza uwaziri ambapo alimteua Binti yake Wanu Hafidh Ameir kuwa Malibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Mkwe wake Mohamed Mchengerwa kuwa Waziri wa Afya.
Madai hayo yanakuja pindi akituhumiwa kuteua ndugu au marafiki wa karibu, na hasa wa kutoka Zanzibar kuhodhi madaraka upande wa bara. Inasemekana kwa sasa Ofisi nyingi za Idara na Vitengo vya Serikali kwa sasa zinashikiriwa na wazanzibari.
Licha ya Kuwepo haja ya usawa wa Kijinsia lakini inadaiwa nafasi nyingi za uteuzi wamepewa wanawake kwa asilimia kubwa, tena wenye asili ya dini yake. Hali hii imekuja kinyume na msimamo wa Magufuli wa kutozingatia uhusiano wa kifamilia au kisiasa.
Kumekuwepo na ripoti zilizonyesha uteuzi wa baadhi ya ndugu wa karibu katika nafasi za juu za kiserikali, jambo linalozua mjadala kuhusu "nepotism" na kuondoa misingi ya utendaji uliotukuka (meritocracy).
#Tuhuma Dhidi ya Abdul Halim Hafidh
Abdul ambaye ni mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu, hasa kwa kuratibu kutekeleza au kufadhili utekaji nyara wa watu. Aidha imedaiwa amekuwa kivuli Cha inteligensia ya kuzima sauti za wapinzani nchini Tanzania.
Sasa bila kujali kama taarifa hizo ni kweli au lah Kuna haja ya kujiuliza kwa nini atajwe Abdul na si mwingine!? Tanzania imekuwa na Marais wengi waliopita, kwanini leo hii atajwe mtoto wa Samia kwenye tuhuma mzito za aina hii? Mbona hakutajwa mtoto wa Magufuli? Au wa Kikwete au Mkapa? Tuseme Hawa hakuwa na watoto? Huyu ni mtu ambaye ana hodhi picha na taswira ya Rais aliyepo madarakani, ni familia ya Rais, Ni kioo Cha jamii na matendo yake kama ilivyo kwa Rais yanafuatiliwa. Anapotajwa kwenye mitandao ya kijamii au Vyombo vingine vya habari inatoa picha gani?
Abdul Halim Hafidh amewahi kutajwa mwishoni mwa mwaka jana 2025, kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 , kwenye Machapisho kama vile 'Africa Confidential' na ''The Africa Repor't' ikiwa ni pamoja na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kwa kuhusika au kushirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania (TISS) iliyoshindwa kubaini wageni walioingia Tanzania kufanya vurugu na ghasia za uchaguzi wa Okotoba 29, 2025, au hata makambi ya vijana waliopewa mafunzo kwenye majengo na misituni, lakini inadaiwa kushirikiana na Abdul kwenye visa vya Utekaji wa wanaharakati, Waandishi wa Habari na Wapinzani wa Serikali. Haya si mambo ambayo yangefanyika chini ya utawala wa Hayati John Magufuli.
#7. Vurugu na Ghasia za Uchaguzi:
Ni kwa mara kwanza chini ya Rais Samia ambapo nchi ya Tanzania ilishuhudia Machafuko, Vurugu na Ghasia kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tar 29 Oktoba 2025 na baadaye. Kwa mara kwanza katika historia ya nchi hiyo walijionea kwa macho matukio ambayo waliyaona kwenye runinga na kusikia redioni yakiwa 'live'
Licha ya kwamba hadi sasa haijajulikana Wafadhili au Wahusika wa ghasia hizo, si kwamba Serikali ya Tanzania haijui kinachoendelea ila kwa lengo la kulinda taswira yake ya nje inashindwa kujivua nguo. Mwisho wa siku mtaambiwa ni wapinzani wa Serikali maana ndiko wanakoelekea.
Lakini kwa vyovyote itavyokuwa ukweli unabakia kwamba yote hayo yametokea chini ya utawala wa Samia Suluhu hilo halikwepeki. Kwa maana nyingine huenda anahusika kwa namna moja au nyingine. Vinginevyo Mbona isitokee kwa Marais waliomtangulia?
Huyu ndiye Rais wa Tanzania anayemwagiwa sifa kabao huku wapambe wake wanakula nyuma ya mgongo wake, mwenye tuzo za shahada zaidi ya 7 kwa kipindi isiyozidi miaka mitano, ambaye kwake kuwapiga bakora wakuu zake wanadai uwajibikaji na Utawala Bora ni kufikia tu hana simile!