#PIGO KWA WILLIAM RUTO ---SIASA ZA MLIMA KENYA

Taarifa za hivi punde leo Tar 08 may 206 zinasema Gavana

wa Murang'a, Irungu Kang'ata, ametangaza rasmi kuwa hatatetea kiti chake cha ugavana kupitia chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Lakini Je kwanini ameamua kuchukua hatua hiyo muhimu:

#1. Irungu Kang'ata Ametangaza Kujiondoa UDA?Kang'ata ametoa sababu kadhaa za kutoendelea na UDA, akielezea kutofautiana kimaoni na uongozi wa chama hicho:Kutofautiana kimkakati na Kisera: 

Kang'ata amesema amekuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na Rais Ruto lakini hawakufikia mwafaka ("full convergence") kuhusu mwelekeo wa kisiasa na maendeleo.

"Kusikiliza Wananchi 'Ground"

Amelalamikia mbinu za kisiasa zinazotumiwa na chama Cha UDA akisema baadhi ya viongozi wanatumia presha na vitisho badala ya ushawishi, jambo ambalo anasema linaweza kukigharimu chama eneo la Mlima Kenya.

Anadai amewasikiliza Wananchi wa eneo lake na kupimanhali ya upepo wa Kisiasa.

Maandalizi Uchaguzi wa 2027: 

Kang'ata amesema anataka kutumia jukwaa lingine ambalo litaakisi matakwa ya wapiga kura wake wa Murang'a, ingawa amedai atabaki kuwa mwanachama mwaminifu wa UDA hadi kipindi chake kiishe.

#2. Je, amehamia Mlengo wa DCP?  

Ripoti zinaonyesha kuwa Kang'ata anaelekea au anashinikizwa kujiunga na chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), kinachohusishwa na aliyekuwa Naibu Rais RigathiGachagua.

Shinikizo la Gachagua: 

Ripoti zinasema Gachagua ameweka shinikizo kwa magavana wa Mlima Kenya, akiwemo Kang'ata, kujiunga na DCP ili kuunganisha eneo hilo.Kujiweka Nje ya UDA:

 Ingawa Kang'ata hajatangaza rasmi kujiunga na chama fulani, amesema anatazama chaguzi zake, ikiwa ni pamoja na kuwa mgombea huru au kujiunga na chama kingine, hata hivo Duru za kuaminika zinasema atahamia chama cha DCP.

#3.Pigo kwa Rais Ruto na Chama Cha UDA:

 Hatua ya Kang'ata inatazamwa kama pigo kubwa (Big Blow) kwa Rais Ruto na chama cha UDA kwa sababu zifuatazo:Kuvunjika kwa Umoja Mlima Kenya: Kang'ata alikuwa mmoja wa viongozi muhimu wa UDA eneo la Mlima Kenya. Kujiondoa kwake kunaonyesha ufa unaokua kati ya Ruto na viongozi wa eneo hilo.

Ushawishi wa Gachagua: 

Hatua hii inaimarisha msimamo wa Gachagua kama kiongozi wa Mlima Kenya, na uwezekano wa kugawanya kura za UDA na za eneo hilo ifikapo 2027.

Athari kwa Siasa za Mlima Kenya: 

Kitendo cha gavana maarufu kujiondoa kinaweza kuhamasisha viongozi wengine na wapiga kura wa kawaida kuacha UDA, wakifuata hisia za "kujikomboa" zinazoenezwa na kikundi cha Gachagua.

Kwa ufupi, Kang'ata ameamua kutojifunga na chama Cha UDA 2027 akisema anasikiliza wananchi, jambo ambalo linadhoofisha azma ya Rais Ruto ya kuweka ngome imara Mlima Kenya kupitia chama kimoja.

Post a Comment

Previous Post Next Post