Hatimaye pepo na tufani za Mgomo na madai ya viongozi wa Vyombo vya usafirishaji vya Kenya
ulioingliwa namkuungwa mkono na Wananchi na Wanasiasa umetulizwa Ksh 10 baada ya kufanyika kikao cha dharula kati ya viongozi hao na Rais Ruto.Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu ya Mombasa, makubaliano makuu yalilenga kusitisha mgomo wa kitaifa uliosababisha uharibifu na kuyumba kwa uchumi. Hata hivo Kuna madai ya Kuwepo mgawanyiko kwa viongozi hao ambapo taarifa zinasema baadhi Yao Waliachwa nje ya kikao kwa kusalitiwa wenzao.
Miongoni mwa Viongozi ambao hawakudhuria kikao leo ni pamoja na Kennedy Kaunda, Mkurugenzi mtendaji wa chama cha waongoza watalii na madereva. Awali bila uwepo wa Rais, viongozi hao walikubaliana na Serikali kusimamisha mgomo kwa wiki moja ili kutoa fursa kwa mazungumzo ya kina. Kubwa kati ya makubaliano yaliyoafikiwa leo rarehe 22 Mei 2026 ni kusitishwa kwa Mgomo kwa jumla.
Hata hivo hakuna manufaa wala faida ya mgomo huo baada ya Rais Ruto kutangaza punguzo la Bei ya dizeli kwa Ksh 10 kuanzia Mwezi ujao badala ya mwezi huu. Wakenya wengi hata hivo wameichukulia hatua hiyo kama isiyokuwa na tija.
Aidha Baada ya kikao hicho na Rais William Ruto, mambo mengine yafuatayo yaliafikiwa:
1. Kupunguzwa kwa Bei ya Mafuta
Punguzo la Bei ya Mafuta: Rais alielekeza kuwa bei ya nishati ya dizeli itapunguzwa kwa KSh 10 zaidi tofauti na lile punguzo la mwanzo litakalotekelezwa katika mzunguko wa bei wa mwezi juni/july.
Hatua hii inalenga kuleta nafuu kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na wananchi kwa ujumla.
2. Masuala ya Bima na Sheria za Madalali (Auctioneers)
Malalamiko ya Wamiliki:
Wamiliki wa vyombo vya usafiri walieleza kero zao kuhusu kunyang'anywa magari yao kiholela na madalali au kucheleweshwa kwa malipo ya bima pindi ajali zinapotokea.
Makubaliano:
Serikali ilikubali kufanya uhakiki wa Sheria ya Bima na Sheria ya Madalali ili kuwalinda wamiliki dhidi ya unyonyaji na hasara katika kipindi cha miezi mitatu.
3. Huduma za Usafiri wa Kidijitali (Ride-hailing Platforms)
Tathmini:
Changamoto zinazowakabili madereva wa teksi mtandaoni zilijadiliwa. Iliazimiwa kuwa Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani (NTSA) ishirikiane na kampuni za kidijitali kuweka nauli ya chini (minimum taxi fare) ili kuhakikisha madereva wanapata faida inayostahili.
4. Utamaduni wa Matatu (Sanaa na Michoro)
Mwelekeo Mpya:
Rais alielekeza NTSA kutoa mwongozo na mazingira wezeshi kwa wamiliki kuendelea kuweka picha za kisanii na michoro (graffiti) kwenye magari yao kama sehemu ya utamaduni unaokubalika kisheria.
5. Usafiri Endelevu na E-Mobility
Dira ya Baadaye: Serikali ilieleza mpango wake wa kuagiza magari ya umeme (e-vehicles) na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza utegemezi wa mafuta kutoka nje ya nchi.
6. Misimamo ya Kiasa na Kiuchumi
Uchumi Kwanza:
Rais alisisitiza kuwa upandaji wa bei ya mafuta ni tatizo la kimataifa na akawataka viongozi na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuepuka kutumia mgogoro huo kujipatia faida za kisiasa.
MATARAJIO:
Kutokana na makubaliano haya, wamiliki wa vyombo vya usafiri watapata faida zifuatazo:
1.) Gharama nafuu za uendeshaji: Kushuka kwa bei ya dizeli kutapunguza gharama za matumizi ya mafuta kwa kila kilomita, jambo linalotoa ahueni ya kifedha kwa waendeshaji wa vyombo vya usafiri.
2.) Ulinzi wa rasilimali zao: Marekebisho ya Sheria ya Bima na Madalali yanatarajiwa kukomesha utaratibu wa magari yao kupigwa mnada kiholela au kukamatwa isivyo halali pale yanapohusika na kesi za madai.
3.) Mazingira thabiti ya biashara: Kusitishwa kwa mgomo kunarejesha utulivu na kuwaruhusu kurejea barabarani kuchuma mapato, badala ya kupata hasara ya mamilioni ya pesa kwa siku kutokana na magari kuegeshwa.
Toa maoni yako...
