#JE, MAANDAMANO YA AMANI YANAWEZEKANA NCHINI KENYA?

 Imebainika Kwamba ni vigumu kufanyika kwa maandamano nchini Kenya bila visa vya uhalifu. Kuna haja ya kujiuliza

kama maandamano ya amani yanawezekana  au la hasha.

 Licha ya  katiba ya kenya Kifungu cha 37 cha Katiba ya Kenya kumpa kila raia haki ya kukusanyika, kuandamana, na kuwasilisha malalamiko kwa amani, Maandamano yanayofanyika kila Mara yamekumbwa na vurugu, machafuko yanayoishia kwenye visa vya wizi na uharibifu wa Mali.

#1. Sababu za msingi ni pamoja na:

1.) Mwingiliano wa Wahalifu (Gen-Z): Maandamano yanapochukua muda mrefu au kuwa makubwa, wahalifu na vibaka hujichanganya na waandamanaji wa kweli kwa nia ya kutumia mwanya huo kupora mali za wananchi na wafanyabiashara.

2.) Kuwepo kwa Vijana Wasio na Ajira: Umati mkubwa wa watu, hasa kutoka mitaa ya mabanda, hutumiwa na wanasiasa au kujiunga wenyewe kwa sababu ya njaa na ukosefu wa ajira, hivyo huona uporaji kama njia ya kujipatia riziki au kuiba bidhaa wanazozitamani.

3.) Polisi kuzidiwa Nguvu:

 Polisi wanapotumia vitoa machozi au nguvu kuwatawanya waandamanaji, mazingira huwa ya sintofahamu. Hali hii huleta vurugu ambazo hutoa mwanya kwa watu wasio waaminifu kuvunja maduka na kuiba. 

4.) Polisi Kutumia Nguvu Kupitia Kiasi:

Mara nyingi Polisi hutumia Nguvu Kupita kiasi jambo linalosababisha waandamanaji kuzidisha Kasi au nguvu ya uharibifu hasa pale yanapotokea mauaji.

5.) Kutoshiriki kwa Viongozi:

Viongozi wa Kisiasa wanaohamasisha migomo au maandamano hatimaye hukwepa na kuwaacha waandamanaji peke yao ambao hukosa kauli au maamuzi yao kuhusu mwelekeo wa maandamano.

6.) Siasa za Chuki na Migawanyiko:

Baadhi ya Wanasiasa hutumia magenge au makundi ya wahuni ambao hufanya uharibifu kwa lengo la kukomoana Kisiasa au kulipiza visasi.

# Kwanini viongozi wanaohamasisha maandamano hawajitokezi?

Sababu za Usalama na Ulinzi: 

Mara nyingi, viongozi hawa (hasa wanasiasa wakuu) huwa katika hatari ya kushambuliwa, kutekwa, au kukamatwa na vyombo vya usalama kwa madai ya kuchochea vurugu. Hivyo, hujiepusha ili kulinda usalama wao binafsi.

Mkakati wa Kisiasa: 

Viongozi wengi huhamasisha wananchi kama njia ya kushinikiza serikali ili iketi kwenye meza ya mazungumzo (dialogue) na si lazima kwa wao kuwa mstari wa mbele mitaani.

Kuepusha Lawama za Vurugu:

 Wakati maandamano yanapogeuka na kuwa ya fujo, wanasiasa wanaweza kushtakiwa mahakamani au kupoteza uungwaji mkono ikiwa wataonekana wakiongoza uharibifu wa mali. 

#Kwanini wabunge na madiwani hawajitokezi kuungana na wananchi?

Hofu ya Kupoteza Kazi au Kufungwa:

 Wabunge na madiwani wengi wanaunga mkono serikali iliyopo madarakani (hasa chama tawala). Kushiriki maandamano ya kuipinga serikali yao wenyewe huhesabiwa kama utovu wa nidhamu au uhaini, na wanaweza kufunguliwa mashtaka au kupoteza nyadhifa zao.

Kutofautiana Kimaslahi:

 Viongozi wengi huchaguliwa kwa misingi ya kisiasa. Mbunge anaweza kuona kuwa kuungana na waandamanaji kutampa umaarufu wa muda mfupi lakini kuharibu uhusiano wake na viongozi wakuu wa serikali anaowahitaji ili kuleta maendeleo kwenye eneo lake la uwakilishi.

Kuepuka Kuhusishwa na Uharibifu wa Mali:

 Wabunge mara nyingi huona ni hatari kushiriki maandamano ambayo huenda yakaisha kwa uharibifu wa miundombinu au majengo ya umma, kitu kinachoweza kuwaharibia wasifu wao wa kisiasa.

Hitimisho:

Ili maandamano ya amani yaweze kufanikiwa na kuepusha maafa nchini Kenya, mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:

Kuheshimu Sheria: 

Kila mwananchi lazima afuate sheria kwa kuandamana bila silaha na katika maeneo yasiyovuruga biashara au shughuli za wengine.

Ulinzi wa Polisi:

 Idara ya Polisi inapaswa kutoa ulinzi kwa waandamanaji na kuwatambua waporaji mapema badala ya kutumia nguvu nyingi kupambana na wananchi wote.

Mazungumzo ya Kwanza: 

Viongozi wanaoongoza maandamano wanapaswa kutanguliza mazungumzo na mamlaka husika (kama ilivyofanyika kwenye mgomo wa wasafirishaji) ili kupunguza muda wa wananchi kukaa barabarani, jambo ambalo hutoa mwanya wa wizi. 

Wananchi wabadilike:

Wananchi wanatakiwa kuwa wastaraabu wenye kutii sheria na kuepuka Wizi namuporaji.

Serikali kuongeza Ajira na Uwezeshaji:

Serikali ipanue wigo wa nafasi za ajira na uwezeshaji wa mitaji kupunguza utegemezi na vijana wawe na mambo ya kufanya ili waepuke uharifu kama njia ya kujipatia kipato.

Post a Comment

Previous Post Next Post