Mwanamke mmoja kwa jina Rachel Wandeto kutoka Kirinyaga na anayeishi Kasarani anapigania uhai wake kwenye hospitali moja mjini Nairobi
baada ya kuvamiwa na kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.Hivi karibuni Wandeto au kwa jina lingine Muthoni alijipatia umaarufu baada ya kuchora tattoo ya picha ya Rais William Ruto na kuandika maneno ya "Two-Term'' mabegani na kifuani pake.
Sababu:
Ripoti zinaonesha huenda ikawa sababu za Kisiasa, kulingana na masimulizi yake, wavamizi hao walimuuliza kwa nini anafurahia na kunufaika na mambo ya serikali peke yake, jambo linaloashiria chuki za kisiasa na kijamii kuhusiana na uungaji mkono wake wa mlengo wa ''Tutam''
Dini, Siasa na Dunia:
Taarifa zaidi zinasema Mwanamke huyu pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili, jambo ambalo limeibua hisia mchanganyiko na mjadala mkubwa mitandaoni na dodoso za habari kuhusu uamuzi wake wa kuchora tattoo mwilini mwake hasa kwenye marneo ya wazi ya mwili.
Ugomvi na Mumewe
Kuna taarifa kwamba hayupo kwenye mahusiano mazuri na Mumewe ambaye anaaminika kuunga mkono mtazamo wa kisiasa unaopinga muhula wa pili kwa Rais Ruto. Inasemekana mwanaume huyo alikasirishwa sana na hatua hiyo ya mkewe kuchora picha ya rais na kuandika neno "Two Terms" hasa eneo la karibu na kifua Juu ya ziwa lake na alimtaka aondoke nyumbani mpaka pale atakapofuta tattoo hizo.
Maadili, Ukristo na Tattoos
Kumekuwepo mjadala Mzito juu ya hulka za mwadada huyo, Wengi wakihoji utata wa mwanamke huyo kuwa muimbaji wa injili huku akiwa na tattoos kwenye maeneo ya wazi ya mwili wake (kama vile mabegani na kifuani / kwenye titi) na Ukereketwa wake kwenye siasa za 'Tutam''
Mafundisho ya Dini:
Katika mafundisho ya Kikristo, mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Walawi 19:28 na Wakorintho 1 6:19), na tattoos huonekana kama ulimwengu au uvunjaji wa amri za Mungu.
Kuweka picha ya mwanasiasa/rais pamoja na neno lenye mlengo wa kisiasa (“Two Term”) mwilini ni jambo linaloleta mgongano mkubwa wa kimaadili kwa mtu anayejitambulisha kama mtumishi wa Mungu.
HITIMISHO:
Tunadhani ni vema haki itendeke kwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya Vyombo vya haki wavamizi waliohusika.
Lakini pia ni vema kwa wasanii au waimbaji kujipambanua kwa matendo Yao kama kweli wanafanya kazi ya Mungu au wamejificha kwenye matamanio ya Dunia na kutafuta pesa.
Mara nyingi tumewaona waimbaji wakijihusisha na siasa chini ya kivuli Cha dini/ injili. Baadhi wanaonekana wakijipamba kwa UREMBO wa kila namna mathalani kujipodoa na kujipaka wanja, mitindo ya nywele,mavazi, uvaaji wa shanga, mikufu, bangili ambavyo hata hivyo vimekatazwa kwenye maandiko.
Toa maoni yako....
