Ndindi Nyoro anapendekeza kupunguzwa kwa kodi na tozo mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja kupunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima ili
kushusha bei ya mafuta, Nyoro anaongezea kwa kujenga hoja kwamba mafuta yanayoagizwa kuja kenya hayapitii kwenye mfereji wa Hormuz kama serikali inavyodai mara kwa mara.Mbunge huyo wa kiharu anadai kwamba mgogoro kwenye mfereji wa Hormuz na mfumo wa Serikali kwa Serikali (G-to-G) hautoi picha kamili ya ugumu wa gharama hizo.
Hiyo ndivyo sababu ya wakenya kuuliza swali moja muhimu linalojirudia kila uchao:
Kwa Nini Bei ya Mafuta Iko Juu nchini Kenya?
Hakuna jibu la msingi la swali hili lililokwishatolewa.
Upekuzi wetu hata hivo umebaini kwamba ingawa mafuta yanayoagizwa nchini kenya hayapiti moja kwa moja kwenye Mlango wa Hormuz kuja Kenya, bei zinaweza kuwa juu kutokana na mambo haya makuu:
Kodi na Tozo Kubwa:
Sehemu kubwa ya bei ya mafuta inatokana na kodi. Zaidi ya nusu ya gharama ya lita moja inachangiwa na ushuru, kodi ya barabara, na VAT hizi ndizo Kodi anazodai Mbunge wa kiharu kwamba zipunguzwe japo kwa muda.
Gharama za Kimataifa:
Hata kama mafuta hayapitishwi Hormuz moja kwa moja, yanategemea soko la Mashariki ya Kati. Mivutano ya kijiografia katika ukanda huo huongeza gharama za bima ya baharini na usafirishaji.
Mikopo ya Ndani na Dharura:
Kulingana na Mbunge Ndindi Nyoro, baadhi ya tozo za mafuta zimetumika kama dhamana ya mikopo ya serikali, na hivyo kuongeza mzigo kwa mwananchi wa kawaida.
Mapendekezo ya Ndindi Nyoro ya Kushusha Bei ya Mafuta
Ili kupunguza makali ya maisha kwa wananchi, Mbunge huyo amependekeza mikakati ifuatayo ni
Kuondoa Ushuru wa Thamani (VAT): Pendekezo la kufanya bidhaa za mafuta kutosimamiwa kwa VAT ya sasa ya 8% na badala yake kuisawazisha hadi
kwa kipindi kifupi
Kufuta Tozo ya Barabara:
Kuondoa nyongeza ya shilingi 7 kwenye Road Maintenance Levy Fund iliyoanzishwa mwaka 2024 ili kuondoa mzigo.
Kupunguza Matumizi ya Serikali:
Kukata bajeti za serikali (hasa safari za kigeni na matumizi ya kifahari) kwa kiasi cha Ksh. Bilioni 100 na pesa hizo zitumike kufadhili mfuko wa kurejesha utulivu wa bei za mafuta.
Kufuta Mpango wa G-to-G:
Kukomesha kabisa mpango wa kununua mafuta Serikali kwa Serikali (G-to-G), akidai kuwa umekuwa ghali na haufanyi kazi inavyotakiwa katika kupunguza gharama.
Kupunguza Faida za Waagizaji:
Kushusha kiasi cha faida (margin) wanachopata wauzaji wa jumla na rejareja kwa takriban Ksh. 4 kwa lita.
Ruzuku ya Dizeli: Kutoa ruzuku ya ziada ya Ksh. Bilioni 5 kupitia Mfuko wa Kurekebisha Nishati (Fuel Stabilization Fund) ili kupunguza bei ya dizeli.
Je, Serikali ya Kenya Itakubali Mapendekezo Haya?
Serikali ya Kenya, inayoongozwa na Rais William Ruto na viongozi wa Hazina, imekuwa na msimamo tofauti.
Msimamo wa Rais:
Rais ameyataja mapendekezo haya kama siasa zinazopuuza hali halisi ya uchumi na ukweli kwamba kuondoa kodi hizo kunaweza kuathiri uendeshaji wa serikali, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara.
Changamoto ya Utekelezaji:
Ingawa Bunge la Kitaifa lilikubali kupokea na kujadili mapendekezo haya kwenye Kamati ya Bajeti na Kamati ya Fedha, mapendekezo ya aina hii ya kupunguza mapato ya serikali yana upinzani mkali.
Matokeo Yanayotarajiwa:
Ni dhahiri kuwa utekelezaji wa mapendekezo ya Nyoro utahitaji makubaliano ya kina na Waziri wa Hazina ili kuzuia mgogoro wa mapato na upungufu wa fedha katika miradi ya maendeleo.
