Luo-Nyanza Region Decline to Demonstrate on Petrol Price Hike:

Eneo la Luo Nyanza lasalia tulivu licha ya Mgomo wa makali ya ongezeko la bei ya Mafuta kutanda maeneo

mengi nchini nchini Kenya. Kumeshuhudiwa mgawanyiko mkubwa kutokana na viwango vya ushiriki wa Mgomo uliolenga kushinikiza punguzo la bei ya mafuta. katika maeneo mengi nchini, Luo Nyanza , Migori, Homa bay, Kisumu, wasusia Mgomo. 

Chanzo:

Mgomo huo ulifuatia tangazo la Mamlaka ya Udhibiti wa Kawi na Petroli (EPRA) lililoongeza bei za mafuta kwa kiasi kikubwa. 

Sababu:

Kwa nini hakukuwa na maandamano katika marneo ya Luo Nyanza (Kisumu, Migori, na Homabay)?

Maeneo ya Luo Nyanza hayakushuhudia maandamano kama ilivyokuwa maeneo mengine kutokana na mambo makuu yafuatayo:

Ushirikiano wa Serikali ya Umoja (Broad-Based Government):

 Utulivu mkubwa katika eneo hili unahusishwa moja kwa moja na kuingia kwa viongozi wakuu wa upinzani (hasa kutoka chama cha ODM) katika serikali ya Rais William Ruto. Ushirikiano huu umepunguza sana hamasa ya kisiasa ya kuandaa maandamano ya mitaani dhidi ya serikali.

Mabadiliko ya Vipaumbele vya Kiongozi

Kiongozi wa ODM, ''Linda Ground ''Oburu Oginga, kupitia Misingi iliyoachwa na Raila Odinga, na viongozi wengine wa ngazi za juu walioshiriki katika misingi ya serikali ya 'broad-based government' kwa kiasi kikubwa wamechagua njia ya mazungumzo na serikali.

 Hali hii imeondoa utamaduni wa maandamano uliokuwa ukiongozwa na upinzani kila wakati gharama ya maisha inapopanda.

Uwepo wa Viongozi Serikalini: 

Baadhi ya wananchi wanaoegemea mrengo huo wanaamini kuwa uwepo wa viongozi wao katika baraza la mawaziri, kama vile John Mbadi (Waziri wa Fedha) na Opiyo Wandayi, unawapa fursa nzuri ya kusikilizwa na kushawishi mabadiliko ya sera kutoka ndani ya serikali badala ya kutumia maandamano. 

Hali ya Uchumi na Siasa kwa Ujumla

Ongezeko hili la hivi karibuni la bei za mafuta limechangiwa na mizozo ya kimataifa, hasa Mashariki ya Kati. Hata hivyo, wakenya walio wengi wanaendelea kulalamikia mzigo huu wa gharama ya maisha. 

Serikali imekuwa ikifanya mikutano na wadau wa uchukuzi kujaribu kutafuta suluhu ya haraka na kupunguza maumivu haya ya kiuchumi. 

Post a Comment

Previous Post Next Post