# KINDIKI UNDER HEART ATTACK ---NI Kuhusu Kesi ya Gachagua

Makamu wa Rais wa Kenya Prof. Kithure Kindiki yuko mashakani,

presha juu na tumbo joto kufuatia Mwenendo wa kesi ya mtangulizi wake Rigathi Gachagua ya Kupinga kuondolewa kwake ofisini. 

Kindiki ana hofu kubwa kwamba huenda Gachagua akashina kesi hiyo na kuibua mgogoro wa kimadaraka hasa kwenye nafasi ya Unaibu Rais ambao unaweza kusababisha kuondolewa kwake ofisini.

Kindiki ameiomba mahakama kuu ya Milimani iruhusu kuchunguzwa kwa nyaraka za hospitali za aliyekuwa Naibu wa Rais, Rigathi Gachagua zilizotolewa na Hospitali ya Karen ya Mjini Nairobi zilizowasilishwa Mahakamani kuthibitisha kwamba alikuwa mgonjwa kipindi mchakato wa kumwondoa Ofisini ulipofanyika.

#MUHIMU 

#I) Upekuzi wa Nyaraka za Hospitali:

Kuna Mvutano wa Kisheria kati ya fahari Hawa wawili, Kindiki, akiwa Naibu wa Rais (aliyeapishwa baada ya Gachagua kuondolewa), anataka kusikilizwa kwa hoja aliyowasilisha mahakamani kupata kibali cha mahakama ili kuhoji madaktari waliomhudumia Gachagua wakati wa mchakato wa kumwondoa (impeachment) Oktoba 2024. Hii inalenga kubatilisha ushahidi wa matibabu uliotumiwa na Gachagua kuthibitisha kuwa alikuwa mgonjwa na hakuweza kujitetea bungeni.

#II) Kuingilia Kati Uchunguzi wa Afya

Hatua hiyo imemweka Kindiki katika mgogoro wa moja kwa moja na Gachagua, ambaye anadai kuwa kuondolewa kwake kulikuwa na ushawishi wa kisiasa na nyaraka hizo ni muhimu kuthibitisha ukiukwaji wa haki.

#iii) Tuhuma za Usalama: 

Kindiki pia amejikuta akijitetea dhidi ya madai ya Gachagua yanayomhusisha na vurugu na udukuzi wa kisiasa, hatua inayozidisha uhasama kati yao.

#MATARAJIO KWA WAKENYA 

  Matarajio ya Mvutano huu kwa Wakenya:

Hali ya Kutokuwa na Uhakika (Uncertainty):

i) Nani anastahili kuwa Naibu Rais?

Mvutano huu unaendelea kuzua maswali kuhusu uhalali wa kisheria wa nani hasa ni Naibu wa Rais halali, huku kesi ikiendelea mahakamani.

ii) Kuyumba kwa Siasa za Mlima Kenya: Mvutano huu ni sehemu ya mapambano ya ubabe wa kisiasa wa eneo la Mlima Kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.

iii)  Mtihani kwa Mahakama:

 Wakenya wanatarajia kuona kama mahakama itadumisha uhuru wake na kutoa haki, au ikiwa maamuzi yatashawishiwa na siasa, kwani kesi hii inaamua hatima ya uongozi wa nchi.

iv) Hofu ya Vurugu: 

Hatua ya viongozi hawa kuvutana inahofiwa kuongeza mgawanyiko wa kisiasa na kikabila nchini.Hali ya Kesi (Mei 2026):

Mahakama kuu iliridhia ushahidi wa matibabu wa Gachagua (supplementary affidavit), ikiruhusu kesi iendelee huku majaji wakitafuta kubaini ukweli. Gachagua ameondoa ombi la kutaka kurejeshwa ofisini na sasa analenga fidia, akidai kuondolewa kwake kulikuwa kinyume cha sheria.

Post a Comment

Previous Post Next Post