Jioni hii tunaarifiwa kwamba Seneta wa Vigiga Godfrey Osotsi
amevamiwa leo Tar 8, Aprili 2026, kupigwa na kujeruhiwa vibaya na Genge la majambazi/ wahuni akiwa kwenye Hotel moja mjini kisumu. Kwa Mujibu wa taarifa kwenye vituo vya Television na redio nchini Kenya ikiwemo Citizen Tv na NTV Kenya, Seneta huyo wa Vigiga baadaye alisafirishwa kwa ndege hadi Nairobi kwa Matibabu zaidi.Tukio hili linajili ikiwa ni kipindi Cha wiki mbili (2) tu baada ya kutimuliwa kama Naibu Mwenyekiti wa chama Cha ODM kilichogawanyika mapande mawili, Ukiwepo mlengo wa 'Linda Ground' na Linda 'Mwananchi' Licha ya yeye kung'olewa kwenye nafasi hiyo hata hivyo Osotsi alikuwa ametoa taarifa kwamba hatakwenda mahakamani kupinga uamuzi.
Tukio hili la leo linazua maswali na taharuki endapo wimbi hili la majambazi litakuwa linawelenga wanachama wa ODM wa mlengo wa 'Linda Mwananchi' nini kitakachofuata baadaye. Endapo ndivyo waswahili wanasema ukiona mwenzako ananyolewa basi tia maji, hii itamaanisha kuwepo hatarini kwa Wanasiasa wa safu ya mbele wa mlengo huu akiwemo Edwin Sifuna, Babu Owino na James Orengo.
Hata hivo taarifa zaidi zimesema Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi ya DCI imetoa taarifa za kuanza uchunguzi wa tukio hilo. Huku hayo yakijiri, taarifa zinasema kuwa karibu Mkuu wa ODM aliyejitenga na chama hicho na kuanzisha vugu la 'Linda Mwananchi' leo alifikia mbele ya mahakama inayoshughulikia utatuzi wa migogoro ya vya siasa kujitetea ili asibanduliwe kutoka kwenye nafasi hiyo licha ya awali kunukuliwa alisema yeye hawezi kuwa karibu Mkuu wa kiwango Cha chini kiasi Cha kuhudumu chini ya Oburu Odinga.
Mwezi uliopita Machi Tar 11, 2026, Tukio sawa na hilo lilitokea tena mjini kisumu kwenye Hotel ya Fairways inayomilikiwa na Irungu Nyakera ambapo Genge la majambazi/ wahuni wapatao 100 walivamia hoteli hiyo na kufanya uharibifu na majeruhi. Hata hivyo hakuna taarifa yoyote kutoka Ofisi ya DCI au Polisi kuhusiana na kukamatwa kwa washukiwa
