#SAFARICOM ISIRUHISIWE KUPIGA CHAPA YA '666' KWA WAKENYA

Katika makala hii, ni maoni yetu Kwamba SERIKALI IJIONDOE KWA SAFARICOM Serikali ya Kenya ijiondoe kabisa kwenye umiliki wa hisa kwenye kampuni ya simu ya safaricom na isiwe mdau. 

Katika kipindi Cha hivi karibuni kumekuwepo mijadala kuhusiana na kuuzwa kwa hisa za serikali zilizowekezwa safaricom. Lakini hii inatakiwa kuangaliwa zaidi ya kujadili kuuza au kitokuuzea kwa hisa hizo.

Kuna haja ya kujadili pia ndoa ya udau iliyopita kati ya Serikali na Kampuni ya simu ya safaricom hasa pale ambapo Serikali inapoweka dira yake kwenye Kampuni moja kwa swala ambalo ni huduma kwa Umma. Mazingira haya ya ushirikiano uliojikita katika uwekezaji yanakwenda mbali na kufanya Safaricom kuonekana kama Idara au Kitengo Cha Serikali. 

Labda tutoe mfano, Mnamo mmoja Tar 6 Okotoba 2022, Rais William Ruto alifanya Ziara nchini Ethiopia kwa lengo la kuzindua huduma za za Kampuni ya Safaricom nchini humo. Ni wazi kwamba hali ingelikuwa tofauti endapo Serikali isingekuwa mdau/ mwenye hisa kwenye kampuni hiyo. Rais anawezaje kuhamasisha uwekezaji wa Kampuni za nje kama serikali yake imehodhi hisa kwenye kampuni ya ndani?

Swali ni je, Serikali itawezaje kutoa fursa sawa kwa Kampuni zingine kwenye sekta ya Mawasiliano endapo dira, dhima na malengo yake yameelekezwa kwa Kampuni moja tu ya Safaricom? Hii maana yake ni kwamba lazima Kuna upendeleo fulani ambao Safaricom itakuwa inaufaidi kutoka kutoka kwa Serikali. Ndo maana Serikali haiwezi kuhoji Wala kudhibiti gharama za juu za Mawasiliano za Safaricom au viwango vya ushindani kwa sababu yenyewe ni mshirika wake.

Kinachoshangaza ni kwamba hata Wanasiasa kama Ndindi Nyoro wanaooneka kana kwamba wamao upeo mkubwa kuhusu uwekezaji kwenye masoko ya hisa, hawaoni Wala kujadili uwezakano wa Kampuni hii ya simu yenye ukwasi mkubwa wa uwekezaji nchini Kenya kuwa na ukiritimba hapo mbeleni.

Tunadhani uwekezaji wowote wenye tija ni ule unaoruhu ushindani unaolenga kuboresha huduma na pia kupunguza gharama kwa watumiaji. .Hii ni muhimu pale ambapo Kampuni au Shirika husika linakuwa na uwekezaji wa kibiashara lakini wakati huo huo linakuwa mtoa huduma.

Kulingana na taarifa za hivi majuzi kufikia tarehe 16 Aprili 2026, Mahakama nchini Kenya ilirefusha amri ya kusitisha mchakato wa serikali kuuza hisa zake kwa asilimia 15% katika kampuni ya Safaricom kwenda Vodacom/Vodafone. 

1. Hatua ya Uamuzi wa Mahakama

Uamuzi wa Mahakama (16 Aprili 2026)

Jopo la majaji watatu (Francis Gikonyo, Ouya Tabitha Wanyama, na Roselyne Aburili) waliafikia kudumisha hali ya sasa (status quo) na kuzuia mauzo hayo ya hisa yenye thamani ya takriban Sh204 bilioni 204 fedha ya Kenya.

Muda

Kusitishwa huko kutaendelea hadi tarehe 27 Aprili 2026, wakati kesi hiyo itakaposikilizwa tena.

Sababu za Mahakama

Walalamishi (ikiwa ni pamoja na mwanasiasa Tony Gachoka na wengineo) walipinga mauzo hayo kwa madai kwamba yanaweza kuhatarisha data za mamilioni ya Wakenya na kuathiri usalama wa taifa. Pia, kulikuwa na wasiwasi kuhusu uwazi wa mchakato huo wa serikali kuuza asilimia 15 ya hisa zake kwa Vodafone, na kupunguza umiliki wa serikali kutoka asilimia 35 hadi 20. Sasa data za wakenya zinaaminika kwa kiasi gani kulindwa na Safaricom kwa sababu si Idara Wala kitengo Cha Serikali!? Kuna imani gani hasa kwa safaricom kuliko Vodaphone!? Haya yote ni mashirika binafsi.

Hii ndivyo mantiki ya hoja yetu kwamba Serikali ya Kenya inapaswa kujiondoa kabisa kwa Safaricom hata kama itachukua mchakato wa kipindi kirefu lakini Hatimaye kuwepo uhuru wa uwekezaji kwenye sekta ya Data na Mawasiliano.

 2. Mawazo Tofauti kuhusu Serikali Kuuza Hisa (Ubinafsishaji)

Kuna maoni yaliyogawanyika kuhusu hatua ya serikali kujiondoa kikamilifu au kupunguza hisa Safaricom:

Wanaounga mkono kujiondoa (Kuuza Hisa zote): Wanahoji kuwa serikali ikiwa mdau mkubwa (35% awali), kunakuwa na upendeleo unaozuia ushindani wa haki.

 Hii inazuia kampuni zingine za simu (kama Airtel au Telkom au Kampuni mpya) kuwekeza kikamilifu, na hivyo kudumisha gharama kubwa za mawasiliano. Wanaamini ushindani huru utashusha bei.

Wanaopinga (Kubaki na Hisa): Wanahoji kuwa Safaricom ni "Mali ya Kitaifa" inayozalisha faida kubwa (dividends) kwa Hazina ya Kitaifa. Kujiondoa kabisa kunaweza kuifanya serikali kupoteza udhibiti wa kimkakati wa data na miundombinu muhimu ya mawasiliano.

Hali halisi ya Safaricom: 

Ingawa ni kweli Safaricom ina nguvu kubwa ya soko, imekuwa na viwango na gharama za simu na data zisizotabirika zenye upendeleo kutoka mteja mmoja hadi mwingine. Japo kwa upendeleo huo ni ngumu kwa mtu kufahamu kwa haraka vigezo wanavyotumia, tunadhani ni vema Kampuni ambayo ni mtoa huduma kuwa na viwango visivyobadilika.

Ili kusawazisha ushindani na mapato ya serikali, hatua zifuatazo zinapendekezwa na wadau:

Kurekebisha Mchakato wa Uuzaji: Kuhakikisha uwazi kamili na tathmini huru ya bei ya hisa badala ya mazungumzo ya siri ( private negotiated deal).

Kuimarisha Mamlaka ya Mawasiliano (CA): Kuhakikisha mamlaka hiyo inasimamia ushindani wa haki (fair competition) bila kuogopa ushawishi wa serikali au wa Safaricom yenyewe.

Kutenganisha M-Pesa na Safaricom: Wadau wengine wamependekeza kutenganisha huduma ya M-Pesa na Safaricom ili kutoa fursa sawa kwa watoa huduma wengine wa kifedha. 

Muhtasari

Hadi sasa (Aprili 16-17, 2026), mauzo ya hisa hizo yamesimamishwa na mahakama huku kukiwa na mzozo wa kisheria kuhusu athari zake kwa usalama wa data na uchumi wa Kenya.

Lakini itoshe kusema kwamba kwa jinsi hali ilivyo sasa nchini Kenya huduma za Kampuni ya simu ya safaricom ni sawa na ukiritimba. Kama hali itaendelea hivi, huduma za Kampuni ya safaricom nchini Kenya zinaweza kufananishwa na chatta ya alama 666 inayoelezewa kwenye kitabu Cha Biblia, Ufunuo 13:16-18. Maana yake ni kwamba bila kuwa na Laini ya safaricom kina huduma utazikosa.

 Kuna maeneo mengi nchini Kenya ambapo mwananchi hawezi kupata huduma ya simu au huduma za miamala ya kifedha bila kuwa na lakini/ kutumia huduma za safaricom.

Serikali imekita lengo lake kwa safaricom kiasi kwamba husaidia kumwezesha matangazo yake, si rahisi mtu kujua kwamba safaricom si Shirika la Serikali ila ni Kampuni binafsi. Kwa maoni yetu, kujiondoa kabisa kwa Serikali kwenye Kampuni hiyo kunaweza kutoa fursa kwa wawekezaji wapya hatua ambayo japo itachukua muda huenda kukawa punguzo la gharama za Mawasiliano na data.

Post a Comment

Previous Post Next Post