#RIPOTI YA JAJI CHANDE YAPENDEKEZA MLOLONGO WA TUME

Ripoti iliyokuwa ilikingojewa kwa hamu hatimaye imetolewa. Kulingana na ripoti Hiyo iliyowasilishwa na Jaji Othman Chande tarehe 23 Aprili, 2026, kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025 nchini Tanzania, mambo yafuatayo hayakupata majibu:

1. Mahali Miili Ilipozikwa:

 Ripoti ilikiri vifo vya angalau watu 518 na kubainisha kuwa idadi inaweza kuwa kubwa zaidi kutokana na mazishi kufanyika bila taarifa kwa mamlaka, lakini haikuweka wazi yalipo maeneo kamili ya makaburi ya pamoja.

2. Kambi za Mafunzo:

Ripoti ya Jaji Chande imekiri kuliwepo kambi za mafunzo maalumu kwa watu waliohusika na Vurugu na machafuko hayo lakini haikusema wapi zilipo kambi hizo.

3.Kushindwa kwa Usalama wa Taifa

Ripoti ilijikita zaidi kwenye ghasia na ushahidi wa kidijitali na kushindwa kueleza kwanini idara ya usalama wa taifa ilishindwa kugundua kuwepo wa kambi hizo za kiuhalifu.

4. Wafadhili na Ghasia:

 Uchunguzi ulitumia ushahidi wa kidijitali na mashuhuda, ikionyesha kuwepo kwa ghasia zilizoratibiwa, lakini haikutaja majina maalum ya wafadhili au viongozi waliopanga ghasia hizo.

5.Mwenendo wa Uchaguzi, Kususia, na Kuzima Internet: Ingawa ripoti iliangazia ghasia wakati wa upigaji kura, haikusema kama kususia uchaguzi ndio chanzo cha machafuko, wala haikueleza wazi sababu za kuzimwa kwa mtandao na umeme, ikijikita zaidi kwenye matokeo ya ghasia hizo.

6. Kuundwa kwa msululu Tume Nyinginzo:

 Ripoti inapendekeza haja ya kuundwa kwa tume zingine kukamilisja mambo ambayo kimsingi yalipaswa kubainishwa kwenye tume hiyo ya Jaji Chande, jambo linaloleta hofu ya kuendelea kwa msururu wa tume. Bila lengo ni kuwatafuta wanaopaswa kuwajibishwa.


Post a Comment

Previous Post Next Post