#Kukamatwa Waandamanaji, Je Unadhani Sheria inawalinda kikamilifu?

Takriban watu zaidi ya 50 Walikamatwa jana  (Aprili 21, 2026) kote nchini

kenya wakati wa maandamano dhidi ya kupanda kwa gharama ya bei ya mafuta na maisha kwa ujumla.  Licha ya katiba ya Kenya kuruhusu maandamano Polisi Mara nyingi huwa hawakosi sababu za kuzuia wananchi kuandamana ambapo hutoa sababu kadhaa za kiusalama na kisheria zikiwemo:

Maandamano Kutoarifiwa Polisi: 

Kwa mujibu wa sheria za Kenya, waandaaji wanatakiwa kutoa taarifa kwa polisi kabla ya maandamano. Polisi walieleza kuwa hakuna kikundi kilichopewa ruhusa ya kuandamana katikati ya jiji la Nairobi, hivyo kuyatambua kama maandamano yasiyo halali.

Vizuizi vya Kiusalama: 

Polisi walikamata waandamanaji waliojaribu kukusanyika katika maeneo yaliyopigwa marufuku, hasa maeneo ya karibu na Hifadhi ya Taifa ya Kenya (Kenya National Archives) na katikati ya jiji la Nairobi (CBD) ili kuzuia kuvurugika kwa biashara na usalama.

Kusababisha Usumbufu na Kuzuia Trafiki:

 Baadhi ya waliokamatwa walishtakiwa kwa kosa la kusababisha vizuizi barabarani na kuwataabisha watumiaji wengine wa barabara.

Hofu ya Uhalifu na Vurugu:

 Polisi walijibu haraka kutawanya makundi madogo wakihofia kuwa maandamano hayo yangeweza kuingiliwa na uhalifu au uharibifu wa mali.

Kenya ni miongoni mwa nchi ambamo baadhi ya watu/raia hutumika nafasi ya maandamano kuharibu au kuiba Mali za watu wakakati wa maandamano. Hali hii ni changamoto kubwa kwa jeshi la Polisi kutoa vibali vya kufanyika kwa maandamano.

Ulinzi wa Maeneo Muhimu:

 Hatua hizo ziliambatana na uwepo mkubwa wa polisi maeneo ya kimkakati ili kuzuia waandamanaji kufikia maeneo nyeti. 

Hata hivyo, haki ya maandamano ya amani inatambuliwa na Katiba ya Kenya, lakini polisi mara nyingi hutumia sheria ya usalama kama kisingizio cha kuzuia maandamano kwa kigezo Cha kuhatarisha amani au kutofuata utaratibu wa notisi.

Taarifa zinasema baadhi ya watuhumiwa wameachiwa kwa dhamana katika vituo mbalimbali vya Polisi ikiwemo Nairobi, machakosi, na karatina. Hata hivo Kuna baadhi Yao ambao bado wanashikiliwa na polisi ili kukamilisja uchunguzi.

Post a Comment

Previous Post Next Post