JE, RAIS RUTO SASA ANAIGA 'MTINDO WA MAGUFULI'?

 Hatua ya Rais William Ruto kumsimamisha mkandarasi anayejenga barabara ya Sosera

–Ekona–Ramasha katika kaunti ya Kisii/Nyamira hivi karibuni Tar 13-14, Aprili 2026 kwenye ziara yake eneo la kisii imeotoa sura mpya ya uwajibikaji. 

Rais Ruto amekosoa vikali ukosefu wa utendaji kazi na ucheleweshaji wa miradi ya maendeleo. Mkandarasi huyo amefutwa kazi kwa sababu ya uzembe, huku Rais akisisitiza kuwa fedha zilishatolewa lakini kazi haikuendelea. Taarifa zinasema mkandarasi huyo alipewa zabuni ya ujenzi wa Barabara hiyo tangu mwaka 2018 Rais Ruto akiwa Naibu Rais.

1. Mtindo wa Magufuli 

Hatua hii inaonyesha wazi nia ya Rais Ruto kuimarisha usimamizi wa miradi (supervision) ili kuonyesha utendaji kazi ("Kazi ni Kazi") kuelekea uchaguzi wa 2027. Kwa kusimamia ujenzi yeye mwenyewe ("field supervision"), anajaribu kurudisha imani ya wananchi inayoweza kuwa imetetereka kutokana na miradi iliyokwama, hatua inayofanana na mtindo wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli, wa 'kutumbua Majipu'

Hata hivo Rais Ruto hakufuatilia kumuuliza Waziri mwenye dhamana au Gavana wa kisii kwa nini hawakufanya ufatiliaji kujua kinachoendelea. Rais wa zamani wa Tanzania alikuwa na desturi ya kuwahoji mawaziri na wakurugenzi hadharani.

2. Barabara ya Sosera ni ya kiwango gani?

Barabara ya Sosera-Ekona-Ramasha inasimamiwa na serikali ya Kitaifa kupitia Mamlaka ya Barabara za Mashambani (KeRRA), ambayo iko chini ya Wizara ya Barabara na Uchukuzi. Mradi huu ulizinduliwa mwaka 2018 na Ruto alipokuwa Naibu Rais, ikimaanisha umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu. 

3. Jukumu la Waziri wa Barabara 

Tunahoji hapa kwamba Waziri anayehusika na Barabara, Davis Chirchir, alilijua hili?  Waziri wa Barabara na usafirishaji ndiye mwenye dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo iliyo chini ya Wizara yake. Ni  ukweli kwamba Rais hawezi kusimamia miradi yeye binafsi. Rais anaposhangazwa na miradi iliyokwama inaashiria kutowajibika na uzembe wa usimamizi wa karibu au taarifa za uongo zinazotolewa kwa wizara na maafisa wa chini.

Kutowajibika: hatua ya Rais kusimamisha mkandarasi (kwenye ziara ya kikazi) ni dalili tosha kwamba waziri na wizara ile husika hajafanya ukaguzi wa kutosha ("on-site inspection") au wamefumbia macho uzembe wa wakandarasi. Au pengine wanakula sahani moja na wakandarasi wazembe.

Ajali: za Barabarani 

Ni katika Wizara hiyohiyo ambapo Kumekuwepo maswali mengi kuhusiana na ongezeko la ajali za barabarani zinazogharimu maisha ya wakenya, bila kuona hatua za dhati zikichukuliwa. Hii ni Wizara ambayo Waziri mwenye dhamana anasimama kama Waziri kivuri, labda kwa kuaminika tu uhusiano wake na mamlaka ya uteuzi na sio kulihudumiwa Taifa. 

4. Miradi iliyodolola kote nchini:

 kuna miradi mingi nchini iliyokwama, na serikali imekuwa ikijitahidi kulipa madeni ya wakandarasi (Pending Bills) ili waweze kurejea kazini. Rais Ruto amesema analenga kuhakikisha miradi yote muhimu inakamilishwa ili kutimiza ahadi zake kuelekea 2027. 

Hitimisho 

 Hatua ya Rais Ruto ya sasa ni mbinu ya kisiasa na kiutendaji (politico-administrative move) kuonyesha "kasi mpya" ya maendeleo, huku akichukua hatua za kinidhamu dhidi ya wakandarasi na kutoa onyo kwa maafisa wa serikali wanaolala kazini, hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa mwaka kesho.

Post a Comment

Previous Post Next Post