Sakata la kuagizwa mafuta yasiyo na ubora limechukua
sura mpya baada ya kubainika dhahiri shahiri kwamba Waziri wa Nishati na Mafuta wa Kenya, Opiyo Wandayi aliidanganya kamati ya Bunge.Kinyume au kuachana na ripoti kwamba hakujua na hakujulishwa kuhusu sakata la uagizaji Mafuta yaliyo chini ya kiwango, ripoti mpya sasa inayoonyesha kwamba Waziri huyo alidanganya kamati ya bunge ya Nishati na Mafuta aliposema Kwamba mafuta ya ziada yaliyokuwa yameagizwa ambayo yeye aliyazuia yalikuwa hayajaingia kwenye vinu au Matenki ya Mafuta' ya Kenya.
Akijieleza mbele ya kamati hiyo akiwa na baadhi ya wajumbe wa Wizara yake, alisema mafuta hayo hayakuwa yamefika kwenye matanki ya Kenya, na kwenye mzunguko wa soko..
Wandayi aliambia Kamati hiyo ya Bunge mnamo Aprili 13, 2026, kwamba alijua kuhusu shehena hiyo isiyo ya kawaida ya nje ya makubaliano ya G-to-G mnamo Machi 30. Alisisitiza kuwa alichukua hatua kusimamisha shehena zingine na kumtaarifu Rais William Ruto alipogundua ukiukaji huo. Hata hivyo, ripoti za uchunguzi zinaonyesha kuwa mafuta hayo yenye sumu tayari yalikuwa yameshaingia sokoni wakati uchunguzi unapoendelea
Kukataa Kujiuzulu:
Wandayi amekataa shinikizo la kujiuzulu kufuatia sakata ya mafuta duni ya Ksh bilioni 4.8, akisisitiza kuwa hakuna msingi wa kisheria au utaratibu wa yeye kuondoka ofisini wakati uchunguzi ukiendelea. Imekuwepo desturi ya Viongozi kuhusika au kufanya ubadhilifu au kushindwa kuwajibika lakini Bado wakasalia maofisi.mwao. Kitendo Cha kudanganya kamati ya Bunge la Taifa si swala la kubeza.
.
Kukosekana Uwajibikaji
Wandayi aliambia kamati kuwa uingizaji wa mafuta hayo uliidhinishwa na Katibu wa Kudumu wa Petroli (Mohamed Liban) na maafisa wengine, ambao tayari wamejiuzulu. Anadai kuwa yeye kama Waziri, hakuwa afisa wa kiufundi anayesimamia kuidhinisha shehena hii maalum.
Shambulio la Mwanaharakati:
Ikumbukwe hapa kwamba Mwanaharakati wa haki za kibinadamu, Francis Awino, alishambuliwa kikatili jijini Nairobi mnamo Aprili 7, 2026, muda mfupi baada ya kuitisha kujiuzulu kwa Waziri Opiyo Wandayi. Wanaharakati na Wananchi walimshutumu Waziri huyo kwa kuandaa shambulio hilo ili kunyamazisha Sauti za kizalendo, ingawa madai haya hayajathibitishwa, lakini tukio lile lilifanyika baada ya kauli Ile kutolewa.
Shinikizo Kumtaka Ajiuzuru Laendelea
Kando na shambulio la mwanaharakati huyo, shirika la kutetea haki za binadamu la Focal Africa leo Tar 14 Aprili 2026, limezidisha wito wa kujiuzulu kwa Wandayi, likitaka uwajibikaji kwa umma.
Kuendelea Ofisini:
Licha ya sakata hiyo, maswali makali kutoka kwa wabunge, na kesi inayoendelea katika Mahakama Kuu ikitaka kusimamishwa kwake, Wandayi anasisitiza kuwa ana uwezo wa kutekeleza majukumu yake, akisema: "Hakuna sababu ya kunizuia' kuendelea na majukumu yangu". Lakini Ukweli huu unaoendelea kujidhihirisha ni 'bomu la petroli' kwa Waziri huyo.
Tunadhani ni muda mwafaka sasa Viongozi wawajibike kwa matendo Yao ya uzembe na kutowajibika.
