KWA NINI BAADHI YA WANAUME HUKATA MAWASILIANO NA WAPENZI BILA KUTOA SABABU

Hasa kwa akina dada, Je, uhawahi kuwa mhanga wa mpenzi wako wa kiume ambaye mmekuwa mkiongea

na kuwasiliana vema kukata Mawasiliano au kutoweka tu bila kutoka sababu yoyote? Jambo hili lishawatokea wanawake wengi ambao baada ya kuingia kwenye mahusiano hujikuta wameachwa na wapenzi wao bila kupewa maelezo yoyote. Unakuta mwanaume ghafla anasitisha kupiga simu, au kutuma.ujumbe au akipigiwa siku hapokei...

Kama umewahi kukumbwa na  hali hii je unazijua sababu? Baadhi yake ni kama hizi:-

1. Wanaume hupotea (ghost) kwa sababu mbalimbali, zikiwemo:

2.Uoga wa Mgongano: Wengi huona ni rahisi kupotea kuliko kueleza hisia zao za kutotaka kuendeleza uhusiano.

3. Kutokuwa na Hisia Kali: Wakigundua uhusiano hauna mustakabali, huamua kuondoka kimyakimya badala ya kuumia au kuumiza.

4. Kutokuwa Tayari kwa Wajibu: Wanaona wajibu wa uhusiano (commitment) ni mzito.

5. Wana Mtu Mwingine: Wanaweza kuwa wamepata chaguo lingine bora zaidi au wamerudiana na mpenzi wa zamani.

6. Kujikinga na Majuto: Wengine hupotea ili kuepuka hatia ya kumwambia mwenzao kuwa uhusiano umeisha. 

7. Kukwepa ahadinau majuku Fulani waliyokubaliana na mwenzi wake

8. Kushindwa kuyaweka wazi madhaifu au tabia Fulani ambazo wamezibaini kwa wenzi wao.

Kwa kifupi, mara nyingi ni njia ya kuepuka confrontation au kutokuwa na ukomavu wa kihisia.

Post a Comment

Previous Post Next Post