Serikali ya Tanzania Iko kwenye mchakato wa kukifutia usajili chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kupitia Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.Chama hicho kipo kwenye msuguano mkali na Ofisi ya Msajili, ambayo imeelekezwa kuhakikisha chama hicho hakifanyi shughuli za Kisiasa, chama hicho kimepewa barua ya kujieleza (iliyotolewa Mei 7, 2026) kwanini kisichukuliwe hatua za kisheria, kufutiwa usajili au kutozwa faini. Chama kimetakiwa kuwasilisha maelezo hayo kabla ya Mei 20, 2026.
SABABU KUU:
#1. Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa inadai kuwa CHADEMA inakiuka masharti ya Sheria ya Vyama vya Siasa, hasa kutokana na kauli za viongozi wake (kama Makamu Mwenyekiti John Heche na wengineo) zinazotuhumiwa kuhamasisha maandamano nchi nzima na kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya mahakama kuhusiana na kesi ya Tundu Lissu. Msajili anadai kitendo cha kuhoji maamuzi ya mahakama ni ukiukwaji wa sheria. Madai ambayo hata hivyo yapo katika misingi ya kawaida ya harakati za chama chochote Cha siasa.
#2. Kuzuiliwa kizuizini kwa Tundu Lissu:
Hatua hii inachochewa/inatokana na Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa kizuizini na kesi yake kucheleweshwa. Hali hiyo imefanya mvutano huu umeongezeka zaidi tangu kukamatwa kwake na kuwekwa gerezani tangu Aprili 9, 2025, akikabiliwa na mashtaka ya uhaini na uchochezi.
Chama kimekuwa kikitumia majukwaa yake kushinikiza kuachiwa huru kwa Lissu, jambo ambalo Ofisi ya Msajili inalichukulia kama uingiliaji wa uhuru wa Mahakama. Je, msajili wa vyama vya siasa ndiye mwenye jukumu la kutetea au kuzisemea mahakama za Tanzania? Jibu ni hapana.
#3. Je, sheria na katiba ya Tanzania inaruhusu shughuli za vyama vya siasa?
Ndiyo. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 3, inatambua mfumo wa vyama vingi vya siasa. Hata hivyo sheria hiyo haifuatwi na Serikali ya Tanzania.
#4. Ni kifungu gani cha Katiba kinachoruhusu mikutano naihadjara ya siasa? Katiba ya Tanzania Ibara ya 20(1) inalinda uhuru wa kukusanyika na kushirikiana. Kwa ufafanuzi zaidi, sheria ya vyama vya siasa na kanuni zake (kama Kanuni za Kuratibu Mikutano ya Hadhara za 2023) zinasimamia utaratibu huo.
#5. Je, ni vizuri kuondoa sheria ya vyama vingi Tanzania ili ibaki na chama kimoja?Hata hivyo, kisheria na kikatiba, Tanzania ni nchi ya demokrasia ya vyama vingi. Kwa vile Sheria hiyo/katiba haifuatwi ni ushauri wetu kwamba kuliko kuihadaa Umma wa watanzania kwamba Tanzania ni nchi ya demokrasia, ni vema kifungu kile kifutwe ijulikane wazi kwamba nchi Ina siasa za chama komoja.
#6. Watanzania wafanye nini kukabiliana na ukandamizaji wa demokrasia?
Kisheria, njia zilizopo ni:
I) Kutumia Mahakama kudai haki. (Mahakama zisizo na uhuru)
ii) Kushiriki katika mijadala ya umma na Katiba. (Isiyokubalika na Serikali)
iii) Kutumia njia za amani za kisheria kupinga uamuzi usio wa haki.(Ambazo ni ngumu)
iv) Shughuli za Uanaharakati (Zinazokataliwa)
v) Asasi za Kiraia
#7. Kufungua kesi Nje ya Nchi:
Wanaharakati, vyama au Asasi za Kiraia wanaweza kufungula kesi za kisiasa nje ya nchi. Endapo mahakama za ndani zimeshindwa kutoa haki, wanaharakati au vyama wanaweza kupeleka kesi kwenye mahakama za kikanda au kimataifa,
kama vile:
I) Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) (Arusha, Tanzania) kesi hizo zinaweza kupelekwa kupitia taasisi binafsi zenye hadhi.
ii) Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACJ) (Arusha, Tanzania).Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC).
Hata hivyo Kuna mwanya kiasi kidogo kwa mahakama za Tanzania hasa baada ya Mahakama nchini humo hivi karibuni (Aprili 2026) kuondoa zuio la Serikali kwa vyama vya siasa kufanya mikutano yao.
#8. Nini hali halisi (status) ya kesi ya Tundu Lissu hadi Mei 15, 2026?
Tundu Lissu bado yuko mahabusu tangu kukamatwa kwake Aprili 9, 2025.
Kesi yake ya uhaini na uchochezi (inayotokana na maneno dhidi ya uchaguzi wa 2025) inaendelea katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya jopo la majaji watatu.
Mashahidi wa Jamhuri wanaendelea kutoa ushahidi, huku Lissu akilalamikia kuchelewa kwa haki na mazingira ya kizuizini.
#9. Nini mazingira yanayosababisha kuchelewa kwa kesi ya Tundu Lissu?
Ushahidi Mkubwa:
Kesi hiyo ni ya uhaini na inahusisha mashahidi wengi wa jamhuri (shahidi wa 7 ameanza kutoa ushahidi kufikia Februari 2026).
Mapingamizi ya Kisheria:
Mawakili wa pande zote wamekuwa wakiweka mapingamizi mbalimbali.
Mchakato wa Rufaa:
Baadhi ya hatua zimekuwa zikihitaji maamuzi ya Mahakama ya Rufaa.
Hali ya Kisheria:
Kesi za uhaini zina taratibu ngumu na zinazochukua muda mrefu za kisheria.
Toa maoni yako kwa makala hii...
