Aliyewahi kuwa kada na mkereketwa wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alikatiwa dau na kuhamia chama
Cha CCM hatimaye ameomba kurelerea chama chake chanasili.Katika maneno yake, Peter Msigwa amenukuliwa akisema na tunamnukuu, ''Nimefikiri na kutafakari kwa muda mrefu baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki, utu na dhuluma dhidi ya uhai wa binadamu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025. Siwezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya tena,
Kwa dhamira yangu binafsi, leo nimejiondoa rasmi kutoka CCM na kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za CHADEMA.
Kwa Watanzania wote, na wanachama wa CHADEMA wale walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wangu wa awali, naomba radhi kwa dhati pale nilipokuwa kinyume na matarajio yetu ya pamoja katika safari ya kutafuta haki, utu na demokrasia ya kweli"
Haya hivyo kumekuwepo na mawazo na hisia mchanganyiko miongoni mwa watanzania hasa wanachama wa chadema huku wengine wakisema akubaliwe kurudi na wengine wakikataa kumkaribisha tena Msigwa kwa madai ya kukisaliti chama.
Haya hivyo uamuzi wa Msigwa unaonekana kupokelewa na wanachadema kama pigo kwa Chama Tawala cha CCM ambacho kinatuhumiwa kwa kuwashinikiza au kuwanunua Wanasiasa magwiji wa chadema kuhamia CCM.
Huku wimbi la chadema likianza kushika kasi, inatarajiwa wapo wengi watakaofuata mkondo wa Msigwa.
Toa maoni yako...
