Katibu Mkuu wa Cha Cha UDA, Hassan Omari ,ameyateka majukumu ya msemaji Mkuu wa Serikali ya Kenya, Isaack Mwaura, aliyeteuliwa
na kula kiapo halali Cha Utumishi kwa nafasi ya msemaji rasmi wa Serikali ya Kenya.Hivi karibuni imekuwa jambo la kawaida kumwona Hassan Omari akiibuka mbele ya yombo vya habari kuueleza au kufafanua Mambo ambayo kimsingi yalipaswa kutolewa maelezo na msemaji rasmi wa Serikali.
Ipo Mifano mingi ila tuchukulie huu wa hivi juzi tarehe 19 mei 2026, amejitokeza kwenye Vyombo mbalimbali vya habari kuelezea sababu za ongezeko la bei ya mafuta. Hassan Omari alifafanua sababu kadhaa ikiwemo misukosuko na hali ya vita ya Mashariki ya kati kuwa sababu kuu ya kupanda kwa bei ya mafuta huku.akiitetea Serikali ya Kenya kwanza kwa juhudi zilizokwisha fanyika kunusuru hali. Aidha aliwasuta wapinzani wa Serikali kuhamasisha upotoshaji wa hali halisi.
Hoja yetu hapa ni kwamba maelezo yoyote muhimu au ufafanuzi kwa Umma wa Kenya unapaswa kutolewa na msemaji wa Serikali ambaye hata hivyo aidha kwa kutowajibika au kwa Sababu nyingine ameonekana kuwa kwenye usingizi wa pono na kutokujua kinachoendelea nchini.
Upekuzi wetu hatukuweza kubaini endapo ni kwa Sababu ya kutowajibika, kutoambiwa chamkusema au kuwepo tu ofisi kwa mfano ilimradi ofisi isibaki wazi.
Tunapomwona Katibu Mkuu wa chama kinachotawala kwa muundo wa Ushirikiano na vyama vingine akiisemaea Serikali , maana yake vile vyama vingine vinavyounda muungano ule vinao makatibu wakuu ambao wanaweza kujitokeza na kusema yao. Hii Ina maana ya kuweza kuleta mkanganyiko wa kauli za Serikali kwa Wananchi wake.
Chama Cha UDA kilishindwa kutawala Nchi kwa peke yake, hivyo kiliungana na vyama vingine kuunda Serikali ya Kenya kwanza, baadaye Serikali ya Kenya kwanza pia ilishindwa kuhimili vishindo vya upinzani na kuunda( Broad--based government) Serikali ya shirikisho la Kenya Kwanza na Chama Cha Orange Democratic Movement, kwa mantiki hiyo muungano wa vyama hivyo unaounda Serikali ya sasa hauwezi kutegemea Hassan Omari kuwa Msemaji. Ndo maana ya kuwepo msemaji wa Serikali na siyo wa chama.
Kwa maoni yetu tunadhani ifike mahali Hassan Omari asalie kukisemea chama cha UDA na sio maswala nyeti yenye maslahi mapana ya kitaifa.
Toa maoni yako....
