#JE, UNADHANI JAMES ORENGO ATAPEPERUSHA BENDERA YA UPINZANI 2027

 Huku Siasa za Kenya zikiendelea kushika kasi kuelekea uchaguzi

wa mwaka 2027, huenda Mwanasiasa mkongwe James Orengo akachuana na Rais Ruto ifikapo 2027. Hayo yamejibainisha kwenye mahojiano kati yake na Mtangazaji Nguli wa Citizen tv, Jeff Koinange kwenye Kipindi chake Cha JKL Jana tarehe 6 mei 2026.

Katika mahojiano hayo, James Orengo hakukanusha uwezekano wa kujitosa kwenye kinyang'anyiro Cha urais mwaka ujao. Mambo muhimu yaliyojitokeza kwenye mahojiano hayo ni pamoja na:

1.Orengo Amepinga Umoja wa ODM na Ruto:

 James Orengo, akiwa kiongozi wa kikundi cha Linda Mwananchi, 

I) Amekosoa vikali hatua ya baadhi ya viongozi wa ODM kujiunga na serikali ya "Broad-based" ya Rais William Ruto.

ii) Asema ODM Haipo  on "Sale": Orengo amesema kuwa chama cha ODM hakipaswi kugeuzwa kuwa chama cha kikanda au kuuzwa kwa UDA.

iii) Amepinga Siasa za kusifu na kuabudu, "Praise and Worship" Politics: Amesema hatakuwa sehemu ya siasa za kusifu serikali na anataka ODM imsimamishe mgombea wake wa urais 2027.Amekosoa Oburu Oginga: 

iv) Orengo amedokeza kuwa mabadiliko ya uongozi yanayofanywa na Oburu Oginga hayafai na hayafai kuangamiza ODM.

2. Orengo anajipanga kugonbea urais wa Kenya kupitia mrengo wake wa Linda Mwananchi. Hata hivyo, kuna upinzani mkali kutoka kwa kikundi cha Linda Ground (wanaounga mkono serikali) ambacho kinamuunga mkono Oburu Oginga au wengine.

Msimamo wake:

 Amesema kuwa ODM ni lazima iwe na mgombea urais na kwamba hataki UDA iendelee kutawala.

3. Mgawanyiko Luo Nyanza Oburu Oginga vs James Orengo:

Oburu Oginga, alishasema mapema kwamba yeye ndiye mgombea pekee atakayesimama kwa Chama Cha ODM, hasa endapo kitahitaji kuwa na mgombea.  Upo Uwezekano wa Mgawanyiko mkubwa,  Kuna hatari kubwa ya Luo Nyanza kugawanyika kati ya Linda Mwananchi (Orengo) na Linda Ground (Oburu/Wanga/Junet, Simba). Hii inaweza kudhoofisha kura za eneo la Nyanza.

Mtaji wa James Orengo: 

Orengo anatumia msimamo wake wa "kutofungwa na serikali" kuvutia wafuasi wa chini (grassroots).

4. Je, James Orengo anaweza kuungana na Rigathi Gachagua Rigathi Gachagua?Uwezekano ni mdogo wa Muungano wa kati yao ingawa wote wawili wanaonekana kupingana na serikali ya Ruto, hatuwezi kuondoa uwezekano wa wao kuungana hasa endapo watahitaji kumdhibiti Rais Ruto.

James Orengo amesema itakuwa "disappointment" (kukatishwa tamaa) kwa Kenya ikiwa Gachagua atachaguliwa kuwa rais 2027, maana yake si rahisi wao kuungana. Hata hivyo, wote wanaweza kupata nafasi ya kufanya kazi pamoja kama sehemu ya upinzani mpana (Opposition Alliance) dhidi ya Ruto. Rigathi Gachagua amedai anawasiliana na viongozi wakuu wa upinzani kuwa na umoja.

5. Wanasiasa gani Mashuhuri wanaweza kuungana na Orengo? Bila shaka Edwin Sifuna, Katibu Mkuu wa ODM, amekuwa akipinga ushirikiano na UDA, Babu Owino: Mbunge wa Embakasi Mashariki, ambaye pia anataka mabadiliko ya kizazi (generational change) na mrengo mkali.Otiende Amollo & Anyang' Nyong'o: Wanaotajwa kuwa na itikadi sawa na Orengo japo wote wanaonekana kutoka eneo moja la Luo Nyanza.

James Orengo inambidi kuweka mikakati wa jinsi atakavyovuna kura kutoka maeneo mengine ya nchi ili kupata ushindi.

6. Je, Orengo anaweza kuungana na Kalonzo Musyoka?  Bila shaka ana uhusiano mzuri na Kalonzo Musyoka, akimrejelea kama rafiki mwaminifu wa Raila. Kuna uwezekano mkubwa wa Orengo, Kalonzo, na Gachagua kuunda muungano mmoja dhidi ya Ruto, ikizingatiwa kuwa wote wameonyesha nia ya urais au wamekuwa wapinzani.

7. Je, James Orengo anaweza kuibuka Mrithi wa Raila Odinga? Orengo anajiona kama mtetezi wa itikadi za kweli za Raila (Principled Leadership).Hata hivyo, Oburu Oginga anajiona kama mrithi wa kisiasa wa ndugu yake (Raila), hasa katika udhibiti wa chama cha ODM. Japo hana mvuto wa walio wengi kwa nafasi ya Urais.

Hitimisho: 

James Orengo anaweza kurithi "Tibim" (mlengo mkali wa upinzani), lakini Oburu anarithi "Chungwa" (udhibiti wa chama).Muhtasari wa Hali (Mei 2026, Orengo anapambana kuhakikisha ODM haimezwi na UDA. 

Ikiwa atashindwa katika uteuzi wa ODM dhidi ya Oburu, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuondoka na kuunda chama kipya au kuungana na upinzani mwingine, hatua inayoweza kusababisha mgawanyiko mkubwa wa kura za Luo Nyanza.

Post a Comment

Previous Post Next Post