#JE, KATIBA MPYA TANZANIA INAWEZEKANA?

 Kauli na matamshi ya Rais wa kiimla wa Tanzania kwa Rais aliyechaguliwa kidemokrasia wa kenya

tarehe 5 Mei 2026, mjini dodoma hayakubariki. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitoa kauli nzito zinazohusu ushirikiano wa kikanda katika kudhibiti demokrasia na uhuru wa maoni kwa vijana wa  (Gen Z) wa nchi za Kenya na Tanzania jambo ambalo limeibua mjadala mzito. Hapa tunajadili kwanini hasa Rais Samia alitoa ushauri huu kwa Rais William Ruto wa Kenya:

#1. Sababu za msingi kuhusiana na ushauri wa Samia Suluhu kwa Rais Ruto:

I) Kutofautisha Demokrasia na Fujo:

 Rais Samia amesema maandamano ya Gen Z Kenya siyo demokrasia bali ni "fujo" na "utovu wa adabu" unaotishia amani na utulivu wa nchi.

ii) Hofu na Woga wa Kuenea na kuendelea kwa Maandamano nchini Tanzania:

 Kuzuia vijana wa Tanzania kuiga harakati za vijana wa Kenya.  akisema: "Ruto hao vijana wa Gen Z wakileta mchezo watandike  nami huku kwangu wakijaribu nitawatandika bakora.

iii) Kulinda Mamlaka:

 Samia Suluhu ni mwoga wa mabadiriko na matamshi yake yanaonekana kama hatua ya kulinda serikali zilizopo madarakani (hasa Serikali ya CCM) dhidi ya shinikizo la vijana wanaotaka mabadiliko ya kiuchumi na uwajibikaji. 

iv)Utawala wa kidikteta:

Ni ishara ya utawala wa kiimla wenye lengo la kuzima Demokrasia na uhuru wa maoni. Ni dalili kuu kuonyesha kwamba Watanzania wanayo safari ndefu kuelekea demokrasia halisi.

v)Siasa za kinafiki:

 Kudumisha Siasa za unafiki zilizojaa ukandamizaji kwa kigezo Cha amani. Chama kinachotawala Tanzania (CCM) na watawala wamekuwa wakitumia kigezo Cha uvunjifu wa amani kuzima sauti huru za watanzania. Hii ndo dhana anayoitaka Samia Suluhu kumwambukiza Rais Ruto wa Kenya.

vi) Weledi wa Katiba:

Kukosa weledi wa tofauti zilizopo kati ya katiba ya Kenya na katiba kongwe ya Tanzania, Kulinganisha siasa za Kenya na Tanzania kuwa sawa.

v)Taswira ya mbele kwa Tanzania:

Kauli ya Rais Samia inavyoashiria nini kwa Demokrasia ya Tanzania kwa maoni yetu hii inaashiria utawala wenye viwango vya juu vya kuminywa Uhuru wa demokrasia.

vi)Lengo, dhima na Mwelekeo wa Utawala wa Samia 

 Kauli hizo zinaashiria kwa njia ya wazi bila kificho lengo ,dhima namwelekeo wa utawala wake kutovumilia upinzani mkali wa wanaharakati na maandamano, ikisisitiza amani ya kinafiki zaidi ya uhuru wa Demokrasia, uhuru wa maoni na mikusanyiko ya kisiasa. Hii ni licha ya katiba ya nchini hiyo kuruhusu uhuru wa maoni na mihadhara ya kisiasa lakini Wanasiasa wa upinzani Tanzania hawana uhuru wa kufanya kazi zao Kisiasa.

vii) Kutoaminika kwa Mchakato wa Demokrasia: 

Mtawalia wa aina ya Samia Suluhu ni vigumu kuaminika na wananchi anaowatawala pale anapoonyesha wazi kuiminya uhuru wa maoni. Hatua hii  kwa maoni yetu ni kama hatua ya kurudisha nyuma demokrasia na uhuru wa kiraia na kuimarisha utawala wa kiimla, na inatia doa juhudi za awali za kufungua nafasi ya demokrasia. 

#3. Matarajio kutoka kwa Utawala wa "Uchaguzi wenye Utata"

Kulingana na mazingira ya uchaguzi wa Oktoba 2025, matarajio yanaweza kuwa:

Utawala wenye Nguvu:

 Utawala unaojikita katika utulivu kwa kutumia vyombo vya usalama kukabiliana na upinzani, ukisisitiza kuwa "maandamano ni fujo".

Kufungwa kwa Nafasi za Kiraia: 

Kuna uwezekano wa kuongezeka kwa hatua za kudhibiti mitandao ya kijamii na uhuru wa kujieleza.

Uchumi na Maendeleo:

 Rais Samia anaonyesha taswira ya kujificha chini ya mwamvuli wa amani kuleta maendeleo huku akiminya demokrasia na uhuru wa kujieleza.

#4. Je, ni kweli Tanzania inaweza kupata Katiba Mpya chini ya Samia Suluhu?

Kupatikana katiba mpya Tanzania (2026-2028) ni ndoto: 

Licha ya kukubali mapendekezo ya Tume ya Jaji Chande, itakuwa vigumu sana kwa Samia Suluhu kutoa fursa ya kupatikana Katiba mpya Tanzania kutokana na hali halisi ya kauli na matendo yake.

Rais Samia alikubali mapendekezo ya tume aliyoiunda mwenyewe kuchunguza chanzo Cha machafuko, vurugu na vifo kipindi cha Okotoba 29 2025, na baadaye, na kupatikana katiba mpya ifikapo mwaka 2028. hata hivyo kauli na matamshi yake alipotoa ushauri kwa Rais Ruto wa Kenya alipoomba ushirikiano wa wa kuwapiga bakora wakuu zake inatoa picha halisi Kwamba ni mwoga wa mageuzi na hawezi kuienzi Demokrasia.

Ukweli wa Mchakato: 

Hata hivyo, uwezekano wa kupata katiba inayokidhi matakwa ya wananchi unashukiwa na wengi ikiwa utawala utaendelea kudhibiti uhuru wa maoni. Inaweza kuwa katiba inayokidhi matakwa ya utawala uliopo madarakani, kuliko ya upinzani. Hata hivyo haijaaminika bayana endapo hilo litatekelezwa hasa kwa kuzingatia Kwamba chama kinachotawala Tanzania (CCM) na utawala wa Samia hauko tayari kukabiliana na na changamoto za mabadiliko.

Hii ndo chanzo hasa Cha kuwepo kizuizini hadi leo mwanasiasa maarufu wa upinzani Tundu Lissu.

#5. Je, Rais Ruto anaweza kutekeleza ushauri wa Samia Suluhu?

i) Shinikizo la Umma: 

Katika muktadha wa Kenya, rais anakabiliwa na shinikizo kubwa la katiba inayolinda maandamano, kukusanyika, uhuru wa maoni ikiwa ni pamoja na uhuru wa mahakama tofauti na Tanzania.

Mazingira ya Kisiasa: 

Ingawa Ruto anaweza kutaka kudhibiti maandamano, utekelezaji wa "kuchapa watu bakora'' kama alivyoshauriwa na  Samia unaweza kuleta vurugu kubwa zaidi Kenya kuliko amani na utulivu. Kwa kufanya hivo Rais Ruto anaweza kupunguza uhalali wake (legitimacy).

 Hatukanushi kuwepo visa vya ukiukwaji wa Katiba au ukandamizaji wa haki lakini Rais Ruto hawezi kuutumia ushauri wa Rais Samia nchini Kenya, ila anaweza kutumia njia zingine mbadala.

Kwa mtazamo mwingine, Rais Ruto anaweza kuyapokea matamshi ya ya Samia Suluhu kama Kinga dhidi ya wakenya wanaoweza kukimbilia Tanzania kama kinga ya kuwadhibiti kwa kupata uungwaji mkono wa Samia Suluhu.

 Hata hivyo, ripoti za hivi karibuni 2026 zinaonyesha Rais Ruto anazidi kushirikiana na Viongozi wa Afrika Mashariki na kikanda katika masuala ya usalama.

Rais Ruto na harakati za Gen Z: 

Rais Ruto amewahi kuonyesha nia ya mazungumzo na Gen Z, licha ya kuwepo kwa vurugu na vifo katika maandamano ya hapo awali na anaonekana kiongozi mwenye kupenda mazungumzo zaidi na kuwaelewa vijana wa Gen Z.

#6) Mazingira ya kupatikana kwa katiba ya sasa ya Kenya ni Tofauti na Tanzania.

Samia Suluhu Hassan anaichukulia kwa wepesi katiba ya kenya tofauti na Tanzania. Ni vema kwa Samia Suluhu kujua mambo haya muhimu:

I) Katiba mpya ya Kenya haikupatikana kwa rehema ya watawala,  ilipatikana kwa umwagaji wa damu ya wakenya na si kwa kuwabembeleza au kuwapiga magoti watawala waliopo madarakani kama ilivyo Tanzania.

ii) Katiba mpya ya Kenya ilitengenezwa kwa mchakato madhubuti ambao haukutoa mwanya kwa vipengere vinavyowalinda watawala.

iii) Katiba mpya ya Kenya ilinakiliwa kwa viwango vya juu kutoka Kwa nchi zilizoendelea kidemokrasia hususan Marekani na Uingereza na kuhaririwa kwa viwango vya matakwa ya wakenya, ili kukidhi mahitaji ya wakenya hasa katika misingi ya utoaji wa haki.

iV) Viwango vya utii kwa katiba viko juu nchini Kenya ukilinganisha na Tanzania ambapo hata katiba iliyopo yenyewe haifuatwi na mahakama hazina uhuru wa kutoa haki ila zinaendeshwa na Serikali ama Rais wa nchi.

v) Ni kinyume Cha maadili kwa kiongozi mwenye hadhi ya Rais kumwalika Rais wa nchi jirani na kumshauri kwenda kuivunja katiba ya nchi yake ilimradi kudumisha Ukatili dhidi ya demokrasia na haki za msingi za raia.

vi) Samia Suluhu anapaswa kujua Kwamba Kuna damu ya wakenya ilimwagika kuipigania katiba ya sasa, Kuna mayatima walipatikana kutokana na mchakato huo, Kuna vilema na walemavy wa aina mbalimbali, Kuna watu waliopoteza makazi yao kutokana namharakati hizo.

vii) Nchi jirani ikiwemo Tanzania (na Rais wake) zinapaswa kuiheshimu katiba ya kenya inayolinda uhuru wa maoni, haki ya kukusanyika na kuandamana kwa hoja za msingi.

viii) Samia Suluhu anapaswa kujitafakari wapi anapoipeleka Tanzania, kujipima kwa misingi ya utoaji wa haki, hasa ni urithi gani (Legacy) atakaouacha kwa watanzania? Je watamkumbuka kama mchapa bakora? Dikteta na Mkandamizaji  wa demokrasia, muuaji wa wajukuu zake? 

Toa maoni yako


Post a Comment

Previous Post Next Post